Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
1. Nisubiri nikomae 2. Sijui kipi kitangulie 3. Nina ubinafsi 4. mchumba wangu ni hamnazo 5. sijajiandaa kuwa na familia 6. jambo dogo kama hilo linanishinda
Toa ushauri ili nisiendelee kuwa katika haya unayoyafikiria kuwa yapo
1. Nimekupa ushauri kuwa usubiri Kwanza ukomae,
2. Ujue nini maana ya Familia.
Mkeo ndio wewe, Watoto wenu ndio matunda yenu. Ni lazima uwe na upendo na uweze kulinda familia yako Kwa gharama yoyote.
3. Usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwenzako. Tafsiri yake Acha Ubinafsi.
Fikiria wewe ndio umetoa taarifa kwenu kuwa kuna Mchumba atakuja umtambulishe, Ndugu wote wanajua na pengine wamejiandaa, alafu mwisho wa siku huyo Binti anakuambia amepata ushuru, unaulizia udhuru gani ukitegemea taarifa ya maana, ATI demu wako anakuambia sijui rafiki yake kapata matatizo, utamuelewa?
4. Kuomba Msamaha ni dalili ya MTU anayejitambua, mwenye upendo, anayejali na MTU mnyenyekevu kuwa amekosea.
Kama huwezi kuomba Msamaha ATI mpaka uambiwe sijui ubembelezwe hiyo ni dalili ya kutojitambua, uchanga na kutokukomaa.
5. Kuwa mwanaume ni kuwa na Akili.
Kuiona Jana na Leo kisha kuikadiria kesho(maono)
Sio kila Jambo uombe ushauri, ni dalili kuwa Bado Akili yako haijaweza kujisimamia na huna uwezo wa kuwa Baba.
Kumbuka ukiwa Baba, Mkeo ataitegemea Akili yako kutatua matatizo yake na familia.
Sasa kama Akili haijakomaa Mkeo atapata wapi wa kumtegemea kimawazo?
Mwisho, usidhani nimekukandia, Ila najaribu kuongea Kwa Lugha Kali ili upate uchungu uweze kunielewa kirahisi