Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

ujue maisha ni safari ndefu sana!
Mleta uzi ni type ya wale watu wana overconfidence
watu wenye kujiskia flani hivi kwamba maisha wameyapatia kwahiyo huyo mwanamke ni kama kuwa nae ulikua unamsaidia tu. ( ndio mana maamuzi yako ni sheria)
Wewe ndo wewe yani ...
matendo ya huyo dada yanakuongezea utukufu zaidi...[emoji1]

ni jamii ya watu wenye shida kwenye makuzi yao, inayopelekea upungufu wa Busara
🙂🙂 namshukuru Mungu kwamba sipo labelled hivi na jamii inayonizunguka. Hata wewe tukikutana leo utabadilisha msimamo huu. Bado naamini nilifanya jambo jema, kosa ni kuniacha bila kukaa chini na kujadili kwa pamoja then anarudi anataka mimi niombe msamaha kwao.
 
Kama ulikubaliana na mlipanga kabisa tarehe wewe ukamgeuka then ana haki ya kudai ufanye hayo. Ni fedheha na aibu kubwa kama wazazi wanajiandaa kupokea posa na mahari ya binti yao halafu unawakata kitoto inakuwa ni kama umewafanyia mzaha na utu uzima wao.

What if kama waliwapa taarifa ndugu wa familia kushiriki hafla hiyo nyeti kisha wewe ukawafanyia huo uhuni. Nadhani unatakiwa kulinda heshima yako kwanza kwa kumuomba radhi mpenzi wako kisha na watume tena wazee na maelezo yaliyojitosheleza kuwaelekeza huko ukweni ni kwann ulishindwa kwenda kama ulivyoahidi kisha kutoa ahadi mpya ambayo itafanyiwa utekelezaji.

Hapo umejenga picha mbaya ukweni kuwa haupo makini na hauwaheshimu wazee.
 
Mkuu kuna. watu hawajui kuomba samahani hata kidogo,yani anaona akiomba msamaha ni ujinga ndo type ya huyu Sasa,yani anaona kila a na achofanya yupo sahihi,lakini pengine hata malezi yanachangia,yawwzekana huyu ni wale waliolelewa upande mmoja,sidhani kama angetoka kwenye familia inayoelewka angefanya hivyo,kwani hata wazee wake wangemshauri.
Nimelelewa kwaa baba na mama. Washika dini hasa. From a lovely family,,,
 
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha.

Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea.

Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.

Kabla sijatoa maamuzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?

Mwanaume kuomba omba ushauri hata Kwa mambo madogo ni dalili ya kuwa hajakomaa.

Ukisha-cancel kitu au aki-cancel MTU kitu huna haja ya kukirejesha
 
Wote mnaomponda mshkaji kwa kumsaidia jamaa yake hamna akili, kuna baadhi ya marafiki ni bora kuliko ndugu hata mimi ingetokea situation kama hiyo kwa jamaa flani ningefanya ivo ivo, mnaosema mke atakusaidia siku unamatatizo inamaana hamjui kuwa kuna wanawqke hukimbia familia kipindi cha shida?
 
soma kwa makini sana comments za toughlendon_1
wengine hao wanakupoteza uyakanyage, huyo mwanamke karudi sababu hana options nyingine
Tuwe wakweli tu mkuu unadhani angekuwa na jamaa anaemwona anamwelekeo angerudi? Mater fact kashajaribisha mahusiano mengine kaona hayafanyi kazi sasa atarudije kwa mwana inambidi aombe msamaha na sababu mahusiano ya watanzania wengi yanaendeshwa na ndugu ni wazi ndugu ndio walimwambia ampige chini jamaa hafai atafute mtu mwingine sasa ili waweze justustify kwamba wamerudiana kwenye mahusiano jamaa inabid awaombe ndugu msamaha...mbona hesabu rahisi hizi.. Mwanamke kashindwa kwingine kaamua kurud sababu wewe ndio last resort basi. Watakuja wanawake hapa watapondea hii ishue ila nimesoma koment zao nyingi wao ndio wakwanza kumshangaa mwanamke mwenzao anawezaje kufanya alichokifanya meaning kwamba wanakuaga na option nyingi mwanamke mwenzao anakosaje mtu mwingine kama wewe umefanya kosa kama hilo wanamshangaa karudije kwako sasa basi jibu lake hawawez kukupa mimi nakupa jibu AMESHINDWA KWINGINE WEWE NDIO OPTION YA MWISHO, na ishue ya wanawake na desperation ya ndoa huwa nashindwa kuielewa...
 
Mwanaume kuomba omba ushauri hata Kwa mambo madogo ni dalili ya kuwa hajakomaa.

Ukisha-cancel kitu au aki-cancel MTU kitu huna haja ya kukirejesha
Jamii forums ni jukwaa huru. Si kwa ajili ya wakomavu pekee. Hata sisi ambao hatujakomaa kupitia mawazo ya wengine tunajifunza. Kuwa mwanaume hakunifungi kusikia hoja za wengine.
 
Wote mnaomponda mshkaji kwa kumsaidia jamaa yake hamna akili, kuna baadhi ya marafiki ni bora kuliko ndugu hata mimi ingetokea situation kama hiyo kwa jamaa flani ningefanya ivo ivo, mnaosema mke atakusaidia siku unamatatizo inamaana hamjui kuwa kuna wanawqke hukimbia familia kipindi cha shida?
Vyema sana..
Kwanza usioe kaka ni utumwa.

Bora umemsaidia rafiki, ndoa zilikua zaman enzi za mababu zetu.
 
Jamii forums ni jukwaa huru. Si kwa ajili ya wakomavu pekee. Hata sisi ambao hatujakomaa kupitia mawazo ya wengine tunajifunza. Kuwa mwanaume hakunifungi kusikia hoja za wengine.

Kama Jambo Dogo kama hilo linakushinda mpaka uombe ushauri, ni bora usubiri Akili ikomae ndio uingie ndoani, maana Kwa Akili hizi ndoa itakushinda mapema Mno.

Mtu unashindwa kujua kipi kitangulie kipi kifuate,
Kwa sababu ya ubinafsi wako ndio maana ukamkatili huyo mtoto wa Watu Kwa kisingizio cha rafiki yako sijui anamatatizo gani.

Tafsiri yake ni kuwa hata ukioa utatanguliza mambo ya marafiki kuliko Familia yako(Mkeo na watoto),

Hata huyo Mchumba wako ni hamnazo, yaani Bora ungetoa sababu ya mzazi anaumwa lakini kumbe ni matatizo ya rafiki yako.
Mkuu nafikiri bado hujajiandaa kuwa na Familia.
 
Acha ubwege wewe, pesa zako, unapanga kuwapunguzia matatizo kwa kumnunua huyo mtu umlete kwenu halafu unapangiwa masharti. Usiombe kabisa msamaha, panga tarehe nyingine ya kwenda kuwapa chao wakukabidhi hiyo bidhaa muwe mmemalizana. Bibie akiona haijakaa sawa achana naye atafute bwege mwingine
 
Kama Jambo Dogo kama hilo linakushinda mpaka uombe ushauri, ni bora usubiri Akili ikomae ndio uingie ndoani, maana Kwa Akili hizi ndoa itakushinda mapema Mno.

Mtu unashindwa kujua kipi kitangulie kipi kifuate,
Kwa sababu ya ubinafsi wako ndio maana ukamkatili huyo mtoto wa Watu Kwa kisingizio cha rafiki yako sijui anamatatizo gani.

Tafsiri yake ni kuwa hata ukioa utatanguliza mambo ya marafiki kuliko Familia yako(Mkeo na watoto),

Hata huyo Mchumba wako ni hamnazo, yaani Bora ungetoa sababu ya mzazi anaumwa lakini kumbe ni matatizo ya rafiki yako.
Mkuu nafikiri bado hujajiandaa kuwa na Familia.
nakazia
 
Kawadharau sana wazazi wa binti. Halafu kakosa busara, kawaida jambo kama hilo humwambii binti, unatuma wazee. Mahari huwa haimalizwi. Unatuma wazee hata na elfu hamsini wazee wanajua namna ya kuhandle haya mambo na wangemshauri nn cha kufanya. Bora wasioe tu.
Wazee hutumwa kwa wasichana waliojitunza wenye bikra zao
 
Kama Jambo Dogo kama hilo linakushinda mpaka uombe ushauri, ni bora usubiri Akili ikomae ndio uingie ndoani, maana Kwa Akili hizi ndoa itakushinda mapema Mno.

Mtu unashindwa kujua kipi kitangulie kipi kifuate,
Kwa sababu ya ubinafsi wako ndio maana ukamkatili huyo mtoto wa Watu Kwa kisingizio cha rafiki yako sijui anamatatizo gani.

Tafsiri yake ni kuwa hata ukioa utatanguliza mambo ya marafiki kuliko Familia yako(Mkeo na watoto),

Hata huyo Mchumba wako ni hamnazo, yaani Bora ungetoa sababu ya mzazi anaumwa lakini kumbe ni matatizo ya rafiki yako.
Mkuu nafikiri bado hujajiandaa kuwa na Familia.
1. Nisubiri nikomae 2. Sijui kipi kitangulie 3. Nina ubinafsi 4. mchumba wangu ni hamnazo 5. sijajiandaa kuwa na familia 6. jambo dogo kama hilo linanishinda
Toa ushauri ili nisiendelee kuwa katika haya unayoyafikiria kuwa yapo
 
Alafu ATI mpaka ashauriwe akaombe Msamaha ni kwamba hajui kuwa amefanya Makosa, hajali, na bila Shaka hampendi huyo Binti WA Watu.

Ashamtia aibu Binti wa Watu Huko kwao, lakini Hilo kwake halioni Kwa vile hajafanyiwa yeye.

Alafu angefanyiwa yeye angekuja hapa kupiga mayowe Wanawake ni wabaya.
Tabia za ubinafsi, kutojali hisia za wengine ni moja ya tabia Mbaya zinazotesa wengi katika jamii.

Kwa Sisi tusioweza kuvumilia huwaga hatuchelewi kujibu mapigo.

Ndio maana nikiwaambia Wanawake watafute Pesa wajitegemee waachane na kuhudumiwa naonekana mchawi na Mchukia Wanawake wakati tayari nimeshasoma Gap na kujua jamii yetu ni yanamna gani.
 
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha.

Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea.

Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.

Kabla sijatoa maamuzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
Kama ulitoa ahadi lakini ulipobadili mawazo haukutoa taarifa, wanakuona haupo serious. Kama hukutoa taarifa ulikosea.
 
Wazee hutumwa kwa wasichana waliojitunza wenye bikra zao
Wazee hawatumwi kwa wasichana. Wanatumwa kwa wazazi wa msichana. Hakuna sababu yoyote ya kuwakosea heshima wazazi kwa sababu binti yao hana bikra. Kama unahitaji mwenye bikra tafuta mwenye bikra.
 
Alafu ATI mpaka ashauriwe akaombe Msamaha ni kwamba hajui kuwa amefanya Makosa, hajali, na bila Shaka hampendi huyo Binti WA Watu.

Ashamtia aibu Binti wa Watu Huko kwao, lakini Hilo kwake halioni Kwa vile hajafanyiwa yeye.

Alafu angefanyiwa yeye angekuja hapa kupiga mayowe Wanawake ni wabaya.
Tabia za ubinafsi, kutojali hisia za wengine ni moja ya tabia Mbaya zinazotesa wengi katika jamii.

Kwa Sisi tusioweza kuvumilia huwaga hatuchelewi kujibu mapigo.

Ndio maana nikiwaambia Wanawake watafute Pesa wajitegemee waachane na kuhudumiwa naonekana mchawi na Mchukia Wanawake wakati tayari nimeshasoma Gap na kujua jamii yetu ni yanamna gani.
Busara ni kujenga hoja zenye mantiki katika mada iliyowekwa. Kufikiria mambo mengine nje ya mada na kujenga mitazamo hasi ambayo haipo ni kupoteza muda na kujitwika mambo yasiyo na tija. Kama elites, tushauriane kwa staha. Mambo unayoyaona madogo na yasiyohitaji kujadiliwa, kwa wengine ni inshu kubwa. Tuendelee kushauriana!
 
Back
Top Bottom