Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Jamaa ulichemka Sana

We endekeza tu maneno ya watu kukataa ndoa na kuleta ujana. Kitu unasahau ni kuwa Hao unaowaona marafiki zako leo hutakuja kuwaona kesho ukiwa unaumwa unavaa pampers.

Ujana huwa unawasumbua Sana, stori nyingiiiii ila hamjui ya mbele yenu.

Wewe ulijitolea kuacha kutoa mahali na kujenga familia yako ambayo kimsingi ndio rafiki wako wa kweli na kumsaidia mshkaji, subiri sasa utakuja kuona Nani Atakuwa upande wako katika maisha yako.
Umemaliza Kila kitu
 
Hapa tunapangwa

Tukio la kutoa mahari halitokei ghafla, kuna ndugu wanahusishwa ambao ndo haswa hupeleka mahari.
 
Wengi wamekwambia,
Lower your ego,
Mtoa mada unatabia ya kujisikia,
Tengeneza na huyo dada na familia yake
 
Mbona simple man

"Jaman samahani mambo yangu yalikaa vibaya ndo maana sikuja na masmahanini zaidi Kwa kushindwa kuja kuwajulisha kama nimekwama ila leo nimefika rasmi tulimalize hili swala"

Jifunze ku-lower ego

Vitu kama samahan, naomba, nilikosea, nisamehe, ahsante vinasaidia sana kujenga uhusian mzuri na wengine

Wengi IQ kubwa alafu Emotional intelligence ipo chini sanaaaaa..

Kwenye ule Uzi wako nilikashauri kitu Kwa ulivojibu nikajua tu you have na ku-deal na emotions za wengine
Mkuu kuna. watu hawajui kuomba samahani hata kidogo,yani anaona akiomba msamaha ni ujinga ndo type ya huyu Sasa,yani anaona kila a na achofanya yupo sahihi,lakini pengine hata malezi yanachangia,yawwzekana huyu ni wale waliolelewa upande mmoja,sidhani kama angetoka kwenye familia inayoelewka angefanya hivyo,kwani hata wazee wake wangemshauri.
 
Pampasi za kutoka wapi? ni busara sana kutokufikiria mambo ya namna hiyo. Una uhakika kwamba nikiumwa yeye ndo atakua msaada? let's be objective,,,
Nimesoma alichoandika mshikaji nimegundua kwamba watu wengi wanaanzisha familia kwasababu tu wanaogopa kuwa wapweke huko baadae wakizeeka, watu hawana retirement plan, na nimegundua kwamba watu wengi relationship zao zipo controlled na external power inayotoka kwa ndugu ndio mana wanaona jamaa kuchelewa kulipa mahari ni kosa kubwa sana na ni gumu kusameheka, hapa sasa najiuliza mapenz ya watu wawili yako wapi?.. Hakuna mapenz sikuiz ni maigizo tu ili kuwaimpress watu ambao ukianza kuishi na mwanamke ukipata matatizo hawachangi hata kumi, i just don't understand the whole narrative of the whole dowry paying... Ile hela kwanini inawavurugaga sana ndugu kwanini wanaiwekaga kwenye plan zao kama yakwao vile? Umaskini mbaya sana wazee, wale wazee wa kataa ndoa tuanze kukataa umaskini kwanzaaa
 
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha.

Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea.

Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.

Kabla sijatoa maamuzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
1. Humpendi huyo dada, laiti kama ungekuwa una mpenda usinge chukulia jambo hili kirahisi hivyo.
2. Bado hujapevuka (Mature) na unaendesha maisha yako kwa kufuata makundi rika (Rafiki).
3. Heshima yako kwa watu wazima ina mashaka. Nadhani una kiburi fulani hivi cha kijinga.
 
Usijali. Nenda kwa nia ya kuwaelewesha kilichotokea. Kwanza big up sana. Ulichukulia shida ya rafiki kama dharula kuliko swala binafsi ambalo lingesubiri. Mwenzi wako mbinafsi na inawezekana aliwajaza sumu kwao ndio maana anataka uombe msamaha. Waeleze how it went
Wanawake huwa ni wabinafsi mkuu yan hata kama rafiki ako au mdogo wako angekuwa anadharula ya kutokwa na uhai na ukachukua decision ya kuahirisha jambo lake kunusuru uhai wa ndugu yako bado angekasirika, mkuu be very careful when you do major decisions especially when you incorporate women, us men are built different fuwk the 'all human beings are equal', women are selfish to the maximum, hata kama kungekuwa na msiba angetaka jambo lake litimie kwanza. Wanawake wote wanaocoment hapa wanamwona jamaa kama kakosea sana yan kama ana murder case na kakutwa guilty, lets say jamaa kesho kakutwa na tatizo kubwa unaweza kuta hata huyo mwanamke hawez kumsaidia na hao ndugu zake wanaobwata saivi ndio usiseme msaada akaja kuupata kwa jamaa alomsaidia. All in all ukioa mwanamke ukiacha pussy anayokupa anaweza kuofer nini mezani hili ni lakuzingatia sana...
 
.......kuna mawili katika hili, 1.inawezekana mtu akataka kutoa mahari lakini bado hajui nafasi ya mke/mpenzi/familia katika maisha ya mwanaume halisi, lakini pia hujui nafasi ya rafiki katika maisha yake 2.kuna watu pia wanapoingia katika mahusiano tayari wanaonekana kujiona wao ni wathamani zaidi kuliko mwenzie wake(hali ya kujisikia nakujiona bora na kwamba unaweza fanya maamuzi yoyote hatakama ni ya kumuumiza au kumdhalilisha mwenzio, wazee wa kujiona wako sahihi ktk kila jambo)........Sasa basi kama mtu ana tabia mbili hizo naona bado hajawa matured enough to be in marriage, watu wadizaini hii huingia kwenye ndoa then soon wanaanza kusema kataa ndoa......
Ushauri: omba msamaha vizuri kabisa ukiwa na mahari mkononi plus faini....bibie yupo sahihi kabisa kuweka masharti coz kashagundua kuwa anadeal na mtu ambaye pengine dishi limecheza tayari.....
😂😂😂😂😂😂 Eti dish limecheza 😂😂😂😂😂
 
Wewe muharibifu uwe wa mwisho kuchangia🤣🤣🤣🤣
Mkuu kaongea ukweli mchungu 😂😂😂😂😂😂😂 kuna mawili ni either anakuonea huruma au she is running out of options... And your the only option available baaaasi....
 
kwenye maisha inatakiwa emotional quotient (EQ) mtu asie na EQ basi IQ haina maana
Basi jamaa ni kiongozi mzuri sababu ili uwe kiongozi mzuri na una decisions nzuri EQ inatakiwa i surpass IQ, the decision alifanya as it stands ni the best sababu aliweza kumsaidia jamaake na mpenz wake wamepatana and i hope for the best wata resolve kila kitu...kiongozi mzuri anahitaji EQ nzuri...
 
Usiombe.Nyote hampendani muache tu huyo dada,karudi kwako kwa sababu hana option nyingine sio kwa upendo,
Vile vile na wewe humpendi,ungekua unampenda usingeweza kuhairisha suala la kutoa mahari ungepeleka hata nusu.
 
Huu mchango ningekuwa mod ningeuweka juu kabisa..... Huyu kijana ni moja wa wale wavulana wanao jisikia na kujiona wao ni kila kitu....

Huyu hata baada ya michango ya mawazo alopewa atabaki kama alivyo kwakuwa bado anajiona yupo sahihi....

Mungu saidia hili balaa lisije kwenye familia yetu au ukoo wetu... Mungu saidia pia hiyo familia iwe ya waelewa wasiruhusu binti yao kuingia kwenye hili shimo..... Mungu pia naomba huyo binti ufungue ufahamu wake maana hapa hamna kitu 🚮🚮
Mungu saidia huyu mtu ajifunze kuwafikiria wengine kwa mtazamo chanya. Mungu saidia watu wako wachangie mada kwa utulivu. Tuendelee kuchangia!
 
Nimesoma alichoandika mshikaji nimegundua kwamba watu wengi wanaanzisha familia kwasababu tu wanaogopa kuwa wapweke huko baadae wakizeeka, watu hawana retirement plan, na nimegundua kwamba watu wengi relationship zao zipo controlled na external power inayotoka kwa ndugu ndio mana wanaona jamaa kuchelewa kulipa mahari ni kosa kubwa sana na ni gumu kusameheka, hapa sasa najiuliza mapenz ya watu wawili yako wapi?.. Hakuna mapenz sikuiz ni maigizo tu ili kuwaimpress watu ambao ukianza kuishi na mwanamke ukipata matatizo hawachangi hata kumi, i just don't understand the whole narrative of the whole dowry paying... Ile hela kwanini inawavurugaga sana ndugu kwanini wanaiwekaga kwenye plan zao kama yakwao vile? Umaskini mbaya sana wazee, wale wazee wa kataa ndoa tuanze kukataa umaskini kwanzaaa
umemaliza
 
Kwani uliahidi kutoa mahali Kwa mshenga na wazazi wake Au uliongea na huyo mchumba ako wawili tu?
 
Back
Top Bottom