Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ndio yuko sahihi,enda ukawaambie kilichofanya usitoe mahari kama mlivyokubaliana coz bila maelezo itakuwa ni kama umeachukulia poa wazee na mvi zao na wanaweza kukugeuza zuwena
 
Wewe unajilazimisha kwa huyo Mwanamke kiufupi humpendi,kama uliweza kuthamini kumsaidia rafiki yako kuliko kupeleka mahali maana yake jambo LA rafiki yako lilikuwa muhimu na thamani zaidi kuliko kutoa mahali.

Nakuhakikishia huyo Mwanamke ukimuoa lazima atakuja kulipiza kisasi kwa aibu ulihompa.

Ushauri wangu,naona ndoa yenye migogoro mingi hapo badae ukiamua kuendelea kuwa na huyo Mwanamke.
Sijawahi na sitawahi kuamini kua mwanamke atakuwa wathamani kwangu kuliko watu walionizunguka miaka ya nyuma kabla hata ya mimi kumjua yeye. Mchango wahao watu ikiwemo wazazi, ndugu na marafiki wachache wamuhimu ndio wamenifanya yeye anione mimi leo wamaana hata kukubali mimi kumuoa. Wewe waweza niona namuita rafiki ukaona simple ila hujui alinisaidia step gani ya maisha. Sitamdharau mwanamke ila kamwe hatapita thamani ya hao watu maana in this times, relationships are superficial and have no deeper meaning kama hapo awali.
 
Ila wewe mbona ishu yako ndogo ..mimi kuna mwana yeye sio tu aliahirisha ila hata manzi ake hakumwambia..Kikeni huko wamejiandaaa kishenzi mavyakula na vilaji kama unavyojua wachaga!.. e bwana eeh!!. Mshkaji hakutokea kabisaaaaaa wala manzi ake hakumwambia kitu yan ilikua bonge la soo na aibu kwa dem..ndugu jamaa walishajaa kupokea mahali na kumwona jamaa ila ikawa tee!!.

Wanawake sas wasivyo na akil wakat mwingine, manzi aliporud dar wakaendelea kuishi na mshkaji..sijui waliyamaliza vp? [emoji23][emoji23][emoji23]
Khaaa[emoji1][emoji1][emoji1]jamaa anajiamini nini??ana bahati hajawafanyia wahehe wangejitundika ukoo mzima
 
Mbona simple man

"Jaman samahani mambo yangu yalikaa vibaya ndo maana sikuja na masmahanini zaidi Kwa kushindwa kuja kuwajulisha kama nimekwama ila leo nimefika rasmi tulimalize hili swala"

Jifunze ku-lower ego

Vitu kama samahan, naomba, nilikosea, nisamehe, ahsante vinasaidia sana kujenga uhusian mzuri na wengine

Wengi IQ kubwa alafu Emotional intelligence ipo chini sanaaaaa..

Kwenye ule Uzi wako nilikashauri kitu Kwa ulivojibu nikajua tu you have na ku-deal na emotions za wengine
kwenye maisha inatakiwa emotional quotient (EQ) mtu asie na EQ basi IQ haina maana
 
Jamaa ulichemka Sana

We endekeza tu maneno ya watu kukataa ndoa na kuleta ujana. Kitu unasahau ni kuwa Hao unaowaona marafiki zako leo hutakuja kuwaona kesho ukiwa unaumwa unavaa pampers.

Ujana huwa unawasumbua Sana, stori nyingiiiii ila hamjui ya mbele yenu.

Wewe ulijitolea kuacha kutoa mahali na kujenga familia yako ambayo kimsingi ndio rafiki wako wa kweli na kumsaidia mshkaji, subiri sasa utakuja kuona Nani Atakuwa upande wako katika maisha yako.
Duh Karne hii una mawazo ya zamani. Nina jamaa yangu alikuwa na mke wa Miaka mingi. Jamaa akaugua Figo muda mrefu. Mwanamke akamuuguza mpk akachuka akamkataa jamaa. Mapenzi ya kusaidiana yalikuwa zamani. Sasa hivi tafuta hela tu unaona umuhimu wake.
 
Mkuu hujakosea hata kidogo,
Kama ulitoa taarifa hautaweza kutoa mahari kwa muda ule tatizo liko wapi?

We mchape mimba mambo mengine yata flow yenyewe.
 
Ila huyo mwanamke hana akili pamoja na kumuaibisha bado kajileta mfyuu zake
No, kijana ndo kazingua. Huyo demu inaonyesha ni mtu piece na anajitambua. Sometimes, unaangalia faida ya jumla kuliko kushindana na watu ambao bado wanajitafuta.

Ladies mnapitia changamoto ya umri. Kuna namba zikisoma demu yoyote inapasa awe alert na kufanya maamzi . Sasa ukishindana na hawa vijana ambao bado wanashawishika na kauli mbiu "kataa ndoa" utakwama sana.
 
Mi naona wewe na huyo mwenzio ni pipa na mfuniko. Mmekutana wote watu wa gesi yani af mna EGO za ajabu yani.

Umeharibu shughuli, watu wajiandae na kupika na mapambo kuwa unaenda kutoa mahari waitane ndugu halafu huendi bila kutoa taarifa yeyote. We ni mduanzi kwa hilo tu.

Demu wako pia namlaumu na namuona chizi tu sababu hajielewi. Huwezi kumwambia mtu tuachane af ukae kimya baada ya mwezi unaomba msamaha. Na kuamua kukubembeleza kabisa kuwa ukaombe msamaha na kwao. Huyo demu kama ni mchaga andika maumivu in advance.

Pia jua huo ni mtego kwako kwamba ukishaoa lazma atakunyoosha tu. Jua
kuna kamati ilishakaa na kumshauri
na ameamua kujifanya fala ili akujaze kwenye target ila nachokiona hio ndoa haitaisha migogoro. Lazma atakulipizia huyo demu hana tofauti na Evelyn Salt
 
We ni mwanaume mwenzangu, kwenye hili ulikosea sana, na hata bila binti kukwambia, unabidi uombe radhi kwa wazazi wa uyo binti.

Imagine dada yako amewaita kwaajili ya hilo tukio, alafu shemeji kazama mitini, we kama kaka ungejisikiaje?

Kuna mambo mengine sio uanaume, ni ujinga na upumbavu.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Sio upendo, amekosa pakwenda au pakuegemea. [emoji23][emoji23][emoji23] mwanamke anayekubali kurudi kwa mwanaume hata baada ya janga kutokea usifikiri ni upendo, tena kwa kizazi chetu ndio kabisaa. Huyo amekosa pakwenda, akipapata anasepa, akupende kwani amekuzaa[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji2960]
 
Sijawahi na sitawahi kuamini kua mwanamke atakuwa wathamani kwangu kuliko watu walionizunguka miaka ya nyuma kabla hata ya mimi kumjua yeye. Mchango wahao watu ikiwemo wazazi, ndugu na marafiki wachache wamuhimu ndio wamenifanya yeye anione mimi leo wamaana hata kukubali mimi kumuoa. Wewe waweza niona namuita rafiki ukaona simple ila hujui alinisaidia step gani ya maisha. Sitamdharau mwanamke ila kamwe hatapita thamani ya hao watu maana in this times, relationships are superficial and have no deeper meaning kama hapo awali.
Wewe umechangia jambo la msingi na la maana kwa kutumia akili na matendo ya wanadamu wa nyakati hizi........

Naona wachangiaji wengi wamechangia kwa hisia kali huku wakizifungia akili zao kuweza kuiona uhalisia.......

Nadhani mtoa mada ameweka wazi hilo jambo kwa mwenzi wake ili wajadiliane kabla ya kuchukua hatua na mpenzi mara moja akaona ni dharau pasi na kujadiliana na akaona bora waachane......sote tunajua mwanamke akifikia hatua hiyo hakuna linaloendelea na vurugu lake........

Mimi binafsi siwezi kuacha kuokoa maisha ya rafiki yangu kipenzi au mwanadamu mwenzangu kwa ajili ya jambo la starehe kama ndoa ambalo linaweza kupangwa wakati mwingine.........

Wote wanaangalia upande mmoja wa kijana pasi na kuangalia upande wa pili uliokataa majadiliano ili kufikia muafaka....pengine kwenye hayo majadiliano wangepata option zingine za kumsaidia rafiki huku jambo la mahari likienda kama kawaida.........

Siku zote siwezi kuacha maisha mtu wangu wa karibu yanaangamia huku naona kisa pesa niliyonayo nimepanga kupeleka mahari......

Juhudi za kufikisha ujumbe kwa wazazi na wazee zilitakiwa zifanywe na wote wawili baada ya kukaa na kujadiliana kama wapendanao na kufikia makubaliano......sio zifanywe na mmoja........

Katika kukwazana kila mtu ana kiwango na aina yake ya kupokea matatizo.... pengine mtoa mada alighafirika na kuchanganyikiwa baada ya mpenzi wake kumtakia kuwa tuachane.......unapataje nguvu ya kwenda ukweni hali ya kuwa sababu kuu au kiunganishi chake kimeshavunja daraja kati ya wewe na ukweni kwenyewe......??

Yote kwa yote mambo ya wawili hasa wapenzi sio ya kuyatolea maamuzi ya moja kwa moja na kuhukumu kwani hao watu wanafanya mengi sana......
 
Kingine ambacho sijaelewa. Kama yeye ndo karudi kuomba msamaha basi yeye ndo ana burden ya kuongea na wazazi sio wewe. Wewe uliyeombwa sasa una power. There no way uombwe msamaha then uwekewe sharti😂. Nisamehe lakini sharti.... Wewe mwenye kusamehe ndo uweke sharti la kusamehe.
 
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha.

Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea.

Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.

Kabla sijatoa maamuzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
Sasa we nyau km mahari tu umeshindwa utaweza majukumu ya ndoa?
 
No, kijana ndo kazingua. Huyo demu inaonyesha ni mtu piece na anajitambua. Sometimes, unaangalia faida ya jumla kuliko kushindana na watu ambao bado wanajitafuta.

Ladies mnapitia changamoto ya umri. Kuna namba zikisoma demu yoyote inapasa awe alert na kufanya maamzi . Sasa ukishindana na hawa vijana ambao bado wanashawishika na kauli mbiu "kataa ndoa" utakwama sana.
Exactly
 
ujue maisha ni safari ndefu sana!
Mleta uzi ni type ya wale watu wana overconfidence
watu wenye kujiskia flani hivi kwamba maisha wameyapatia kwahiyo huyo mwanamke ni kama kuwa nae ulikua unamsaidia tu. ( ndio mana maamuzi yako ni sheria)
Wewe ndo wewe yani ...
matendo ya huyo dada yanakuongezea utukufu zaidi...[emoji1]

ni jamii ya watu wenye shida kwenye makuzi yao, inayopelekea upungufu wa Busara
Upo sahihi sana mkuu
 
Back
Top Bottom