Naheshimu sana michango yenu na napenda kuishia hapa. Kwangu mimi, kuwajali watu wengine walio katika shida ambazo ninazimudu ni ibada kwangu. Ndoa ikishindikana leo, itafanyika kesho. Kama si kwa huyu basi ni kwa mtu mwingine. Sina shaka! huyu mahusiano yetu hayatakuwepo tena. Nimeyavunja rasmi this morning. Nitajipa nafasi, si kwa lengo la kukua maana nimekua na akili imekomaa haswa. Imani yangu ni kwamba nitakutana na mtu mwenye mtazamo ule ninaoutaka, ikitokea hajapatikana wala hakuna shida. Ninaishi na nitaishi kwa kuwajalii wengine.
😂😂😂
Kusaidia Watu bila Akili nako ni upunguani.
Ndio maana Manzoni nikakuambia wewe bado haujakua Kiakili, ndio maana hata hujui maana ya Familia.
Familia ndio kitu cha Kwanza Kwa mwanaume na Mwanamke mwenye utimamu wa Akili.
Huwezi sema unasaidia wengine ATI Kwa kisingizio cha ibada huku ukivunja ahadi na Binti uliyekaa naye kwenye mahusiano muda mrefu.
Unajiangalia wewe pekeako Kwa sababu wewe ni mbinafsi.
Hauangalii ni muda gani umempotezea Binti WA watu tena Bora yeye angekuwa amekukosea Ila wewe ndio umemkosea,
Yeye kakasirika ndio maana akakumaind lakini Kwa vile wewe unakiburi hukutaka kujishusha na kuomba Radhi.
Ninyi ndio wale wanaume wa humu JF ambao mnapenda muonekano Kwa nje ni Wema Kwa kuwajali watu wa nje(marafiki ikiwemo wa JF) Kwa kujifanya mnamichango ya kistaarabu kumbe ndani ni Mbwa mwitu.
Si unaona, huku unajifanya mstaarabu Sana unapotoa comments zako lakini unayoyafanya Huko kwenye Maisha halisi mfano Kwa hiyo Mchumba wako ni ushenzi uliopitiliza.
Hata kama utaamua ku-move on muombe Msamaha hiyo Mrembo wa Watu, ili uendelee na Maisha yako Kwa Amani.
Kumpotezea mtoto wa Watu muda na kupeana ahadi na viapo kisha kuvivunja Kwa sababu za kijinga ni usaliti wa Hali ya juu.
Na Dawa ya wasaliti inafahamika,
Ni hayo tuu.