"Amevunja kanuni na utaratibu wa chama,hatufai!kamati kuu imeridhia hatoteuliwa kuwa mtia Nia wa urais"!

Ulichoandika kingekuwa na ukweli, 2015 rais angekuwa Membe. Huyo ndiye alikuwa chaguo la rais Kikwete, wajumbe wakasema hapana.
Tofauti yake sasa hivi watatoa fomu moja tu ya uraisi, kama ilivyokuwa kwa Magufuli kipindi cha pili,
Lakini wakitoa fomu nyingi, Mh Samia atakuwa kwenye kipindi kigumu sana, hasa ikizingatiwa wajumbe wengine wanatoka CCM,

Hapo ndio atajionea rangi halisi ya kina January, Madelu Nchemba, Nape, nawengineo
 
Ndoto sio lazima itimie lakini hii hata mimi imenishtua sana Hadi jasho limenitoka!
Mkuu kuna baadhi ya nyuzi zako sio za kuchukuliwa poa. Hii tunaita ni tip tip tap tip of wat kinaenda kutokea.

Binafsi nakiaminia sana CCM kwenye maamuzi yasiyotarajiwa.

Huku ile kauli ya sikio halivuki kichwa huwa naona inatekelezwa ipasavyo. CCM ni lidude fulani kubwa, ukiona kama vile unaliendesha ujue umeachiwa tu, ila likiamua utaindoka kwa vyovyote vile.

Mifano ipo mingi, kuna wale wabishi wasioona mbali waendelee.
 
Waa
Waambie ukweli Hawa mapimbi hawaelewi chochote!
 
Utaambiwa tu CCM ni imara inademokrasia inaruhusu mwenye nia achukue fomu. Hili chama liacheni tu. Rejea kauli za Jakaya, huwa zimejaa utata sana zinauma na kupuliza. Leo utaona ni wewe tu, kesho labda labda, πŸ˜€πŸ˜€
 
.
 

Attachments

  • photo_2021-08-11_09-06-26.jpg
    53.4 KB · Views: 2
Mama HAJAFELI kabisa. Kwanza yeye ndiye amefanya kazi kubwa ya kumaliza miradi mikubwa. Magufuli alianzisha tu na akafariki akiwa ameacha karibu kila mradi chini ya 36% ukiacha njia 6 za Kimara-Kibaha.

Nyie mnasema kwa vile mumekariri na mnamchukia kwa Uislamu wake na Uwanamke wake.

🚨Chukua hii, 10 kubwa za Rais Samia Suluhu🚨


𝐡𝑦; πΊπ‘’π‘‘π‘Ÿπ‘’π‘‘π‘’ π‘€π‘œπ‘™π‘™π‘’π‘™


1. Alikuta hifadhi ya chakula nchini mwaka 2021 ukiwa tani 250,000, lakini hivi sasa ni 500,000.


2. Alikuta utoshelevu wa mbegu ukiwa 22% mwaka 2021, lakini sasa ni 78%.


3. Katika kipindi chake cha miaka mitatu, Rais Samia Suluhu ameanzisha miradi mipya ya umwagiliaji yenye ukubwa wa hekta 543,3566.


4. Alikuta hali ya upatikanaji wa maji safi na salama ukiwa 76,6% katika maeneo ya vijijini, sasa ni 90%, tunatoboa 100% kabla ya 2030.


5. Hadi kufikia May 2024, vijiji 11,973 sawa na 97.2% ya vijiji vyote, vimefikiwa na umeme, kazi ya Rais Samia Suluhu hii.


6. Ameongeza Bajeti ya TARURA kutoka Tsh 710.31bn/- 2021 hadi Tsh 841bn/- 2024, Mama anajali barabara za vijijini na mitaani.


7. Serikali yake Mama Samia Suluhu, imenunua ndege mpya saba (7), na kufanya shirika letu kuwa ndege 16.


8. Mama huyu, alikuta ujenzi wa SGR LOT 1 ilikuwa 83.55% na LOT 2 ilikuwa asilimia 57.57% mpaka sasa vipande vyote viwili (Dar - Dom) vimekamilika.


9. Mama huyu, ametekeleza miradi mipya ya maji vijiji 1633 (haijawahi kutokea), na mjini 231 |(haijawahi kutokea), hii nazungumzia miradi mikubwa sio kitoto.


10. Kupitia Diplomasia ya Uchumi wa Mama huyu, mwaka 2020 nchi yetu ilikuwa inasajili miradi ya uwekezaji 207 kwa mwaka, lakini chini yake, hivi sasa tunasajili miradi mikubwa 526.
#MamaYukoKazini


NB: Ukinunua uwe na sababu.
 
Utaambiwa tu CCM ni imara inademokrasia inaruhusu mwenye nia achukue fomu. Hili chama liacheni tu. Rejea kauli za Jakaya, huwa zimejaa utata sana zinauma na kupuliza. Leo utaona ni wewe tu, kesho labda labda, πŸ˜€πŸ˜€
Hawa wanaimba mapambio ndio hao hao wanaoutaka urais,
Wakitoa fomu zaidi ya moja tu, hutasikia Tena Mama anaupiga mwingi,
Utasikia sasa ni zamu ya Tanzania Bara, huko wana Rais wao,
 
Nani kakudanganya CCM inataka watu waadilifu? Hiyo 2015 JPM alichaguliwa sababu ya pressure ya upinzani not necessarily sababu ni msafi. Pia ni incumbent president so fomu itakua moja tu mnamkataje? Then akiondolewa rais fisadi unadhani CCM wanataka rais mkali? Ili waibe wapi?
 
Ni kweli. Samia atapita kwa kishindo, kwasabb anakula na wenzake. Kaacha bucha wazi kila mtu anakata steki kwa ukali wa kisu chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…