"Amevunja kanuni na utaratibu wa chama,hatufai!kamati kuu imeridhia hatoteuliwa kuwa mtia Nia wa urais"!

"Amevunja kanuni na utaratibu wa chama,hatufai!kamati kuu imeridhia hatoteuliwa kuwa mtia Nia wa urais"!

Rais nchi hii yuko juu ya hata hao wazee wa ccm. Hakuna uwezo wa kumtoa kwa mizengwe maana ccm yote kama chama inategemea madaraka hayo ya urais kubaki madarakani.
Labda wampige bomu la MTWARA. Hata CCM hawamtaki Bi mkubwa but huyo ni wenu. Labda mumpige Moshi wa mtwara km JPM

Mama na jiwe nachagua jiwe
 
Mwenyekiti wa kamati kuu ndo yeye, na akiwa mkutanoni yeye ni amri jeshi mkuu - anaweza pia kuahirisha uchaguzi akiona mnataka kuleta chokochoko. Yule mjumbe kwa kwanza kutoa hoja kwamba HAFAI kwenye kikao yaani apae mbiguni baada tu ya kuiwasilisha

Tunawaambia kila siku katiba mpya kwa Tanzania mpya HAMTAKI.

Haya sasa, mwemyekiti wetu anaitaka 5.
Ni kweli anaitaka tano lakini hao anaowaaamrisha wakigoma kuamrishwa itakuaje!? Nawaza TU,hii ni ndoto!
 
Huyo Kada mwenyewe naye anautaka huo Ukubwa, maana hata Mwaka 2015 aligombea ila kura za Wajumbe hazikutosha tu.

Kuna Mipango ya chini Chini kutaka kumuondoa huyo aliyepo, na wakongwe wakiongozwa na huyo uliyemtaja pamoja na yule Profesa wa Jalalani wanaendelea na Mipango ya kumuondoa japo aliyepo ameshakusanya nguvu kubwa ya hela kumsapoti kuelekea 2025, ingawa kwenye majukwaa hana mvuto wa ushawishi.
 
Wakuu

Nilipata wasaa wa kumtembelea kada mkongwe sana wa chama chetu Cha mapinduzi juzi huko isimani mkoani Iringa,tukapata wasaa wa kujadili mawili matatu juu ya mwenendo wa chama chetu kuelekea uchaguzi mkuu 2025!

"Kanuni tulizotumia mwaka 2015 wakati wa uteuzi wa hayati jpm ndizo tutazitumia 2025,uadilifu ndio msingi mkuu wa uteuzi was jina la mgombea wetu na SI vinginevyo!

Ugawaji wa Rushwa ya wazi na kuanza kampeni mapema plus ubadhirifu ndio kanuni pekee itakayotumika siku ya mkutano mkuu"

"Mtajwa ameshaonyesha dalili za kukiuka kanuni ameshagawa rushwa za pikipiki na bajaji zenye majina yake pia ameanza kampeni tangu mwaka 2021 Kwa kutamka hadharani atagombea na ushahidi wa wazi kabisa wa piki piki zenye picha yake ameshagawa hiyo ni rushwa ya uchaguzi na chama kimeamua kumuengua mapema kabisa,Mwambieni asijisumbue kwasababu amejiaharibia sifa zote za utia nia"

Nilipomuuliza kwamba desturi yetu inasema lazima ashike mara mbili na sio moja kwanini asiteuliwe!!?

"Ni Huwa anapewa mara mbili lakini amekiuka kanuni Kwa kutoa rushwa wazi wazi Tena bila kificho hiyo ni kuikosea CCM kama taasisi kongwe hapa nchini"

Bado natafakari Ndoto hii nilioiota usiku wa kuamkia leo!

Tusubiri tuone kitakachojiri 2025!
Mkuu wa kamati kuu ni yeye. Sasa kamati kuu ipi? Acha uongo. Magufuli alisema nilimtaka Mwinyi. Msoga et al wakamleta huyu mama for their benefit. Hawatakwepa kwa dhambi hii.
 
Mama HAJAFELI kabisa. Kwanza yeye ndiye amefanya kazi kubwa ya kumaliza miradi mikubwa. Magufuli alianzisha tu na akafariki akiwa ameacha karibu kila mradi chini ya 36% ukiacha njia 6 za Kimara-Kibaha.

Nyie mnasema kwa vile mumekariri na mnamchukia kwa Uislamu wake na Uwanamke wake.

🚨Chukua hii, 10 kubwa za Rais Samia Suluhu🚨


𝐵𝑦; 𝐺𝑒𝑡𝑟𝑢𝑑𝑒 𝑀𝑜𝑙𝑙𝑒𝑙


1. Alikuta hifadhi ya chakula nchini mwaka 2021 ukiwa tani 250,000, lakini hivi sasa ni 500,000.


2. Alikuta utoshelevu wa mbegu ukiwa 22% mwaka 2021, lakini sasa ni 78%.


3. Katika kipindi chake cha miaka mitatu, Rais Samia Suluhu ameanzisha miradi mipya ya umwagiliaji yenye ukubwa wa hekta 543,3566.


4. Alikuta hali ya upatikanaji wa maji safi na salama ukiwa 76,6% katika maeneo ya vijijini, sasa ni 90%, tunatoboa 100% kabla ya 2030.


5. Hadi kufikia May 2024, vijiji 11,973 sawa na 97.2% ya vijiji vyote, vimefikiwa na umeme, kazi ya Rais Samia Suluhu hii.


6. Ameongeza Bajeti ya TARURA kutoka Tsh 710.31bn/- 2021 hadi Tsh 841bn/- 2024, Mama anajali barabara za vijijini na mitaani.


7. Serikali yake Mama Samia Suluhu, imenunua ndege mpya saba (7), na kufanya shirika letu kuwa ndege 16.


8. Mama huyu, alikuta ujenzi wa SGR LOT 1 ilikuwa 83.55% na LOT 2 ilikuwa asilimia 57.57% mpaka sasa vipande vyote viwili (Dar - Dom) vimekamilika.


9. Mama huyu, ametekeleza miradi mipya ya maji vijiji 1633 (haijawahi kutokea), na mjini 231 |(haijawahi kutokea), hii nazungumzia miradi mikubwa sio kitoto.


10. Kupitia Diplomasia ya Uchumi wa Mama huyu, mwaka 2020 nchi yetu ilikuwa inasajili miradi ya uwekezaji 207 kwa mwaka, lakini chini yake, hivi sasa tunasajili miradi mikubwa 526.
#MamaYukoKazini


NB: Ukinunua uwe na sababu.
Ulivyoingiza mambo ya dini na uwanamke wake nikaishia kusoma hapo, hata sioni sababu ya kukujibu bado upo gizani sana.
 
Chama Cha Mapinduzi hakina moral authority ya kujinasibisha kuwa kinatumia kanuni za uadilifu,katika kupata wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.Wajinga pekee ndo wataamini huo upumbavu.
 
Wazee walikabidhiwa hii nchi wapo ,na viongozi wa dini wapo Mimi na wewe tupo tunafeli wapi sasa
Hakuna cha wazee walio kabidhiwa hili taifa,hizi ni hadithi ya vijiwe vya kahawa.Hivi kwa akili ya kawaida kabisa unaona taifa hili lina watu wazima kichwani ? kwa namna taifa hili lilivyo.Leo hii Tanzania inahofia kanchi kadogo kama Rwanda, vichekesho.
 
Ndoto kivipi wakati umeshatuambia ulipata wasaa wa kumtembelea yule jamaa wa jimboni Isimani, kule Iringa?

Anyway, all in all, huyo mama hafai tena kuwa kiongozi wa hili taifa, ana tuhuma nyingi zisizofaa mtu wa hadhi yake kuwa nazo.

Kuanzia zile za kule X zilizotolewa na Mange, rushwa ya wazi kama ulivyoonesha hapo juu, kushindwa kulinda rasilimali zetu, viburi kwa watendaji wake wanaojiona miungu watu wasiogusika hata wakosee vipi, ufisadi miongoni mwa wasaidizi wake na yeye mwenyewe..

Simply amefeli pakubwa kuliongoza hili taifa, ndio maana awamu hii chawa wana sauti zaidi ya mtawala, hii maana yake mtawala hajitambui, hajui anachofanya, wala hawezi kutolea maelezo tuhuma zinazoikabili serikali yake, anaongoza taifa kwa kubahatisha ameamua kujiita chura.
Wazi
 
Ulivyoingiza mambo ya dini na uwanamke wake nikaishia kusoma hapo, hata sioni sababu ya kukujibu bado upo gizani sana.
Wala usijibu wewe ni mtu wa chuki kwa kila anachofanya Samia. Watasoma wengine ili wajuwe ukweli
 
Back
Top Bottom