Habari wakuu,
Siku ya juzi kuna mashirika au taasisi hizo za kimataifa ziliinyoshea vidole Tanzania kuhusu haki za binadamu,uhuru wa kujieleza na Uhuru wa kisiasa.
Tangu habari hizi ziripotiwe kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya nje, huku Tanzania sijaona,sijasikia chombo chochote cha habari kikiripoti habari hii,au kuchambua habari hii kupitia mijadala.
Nimekaa na kujiuliza maswali yafuatayo:
1. Je, ni kweli vyombo vya ndani vimebanwa na mamlaka ndiyo maana hawawezi kuripoti habari kama hizi?
2. Je, huu ni uzalendo wa kutoripoti habari zinazoichafua Tanzania?
3. Je, kutoripotiwa habari hizi na vyombo vya ndani, hakuwezi kudhibitisha kuwa Tanzania hakuna Uhuru wa vyombo vya habari?
4. Hakuna mwandishi aliyefika kwenye mamlaka ya serikali kuhoji yaliyomo kwenye ripoti hiyo ili serikali itoe maoni ili mwandishi abalance stories?
5. Kwa nini vyombo vya habari vya Kenya vipo open sana kuliko vya Tanzania?