Na Mwamba wa Kaskazini
Tarehe 28/10/2019 nimecheka sana! nimesikia BBC wanaharakati eti wamezindua ripoti ya kuhusu mambo ya Tanzania wakiwa Kenya.
Huu ni woga na kutojiamini kwa kiwango cha kisulisuli kabisa. Na haya ni matokeo ya kutumika, kupangiwa agenda usizoziamini na kuwa wakala wa mabeberu.
Upuuzi kama huu nitashangaa Serikali yetu makini ikipoteza muda kuujibu, ni rubbish tupu, takataka kabisa. Hebu angalia haya kuhusu ripoti hiyo:
1. Unahoji watu sijui 70 na ushee kueleza hali ya eti kuna hofu nchini katika nchi yenye watu milioni 60 then unaconclude eti "hakuna uhuru."
Watu wako zao busy wanajenga reli wako busy Stiglers, wako busy viwandani, masokoni halafu wewe eti unaibuka tu ukiwa Nairobi "kuna hofu Tanzania!!!!!!?
2. Mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo ni shushushu Muthoki Mumo aliyewahi kuja nchini kinyemela akijifanya Mtalii. Iliwahi kusikika kuwa alistukiwa, akatimuliwa. Huyu ni mvunjifu wa sheria, leo anaandika kudai sheria???
3. Ripoti inahoji kupotea Gwanda haihoji kupotea na hata vifo vya mamia ya wananchi waliokufa au kupotea Kibiti[emoji849]. Mtu aliyeaga familia yake kuwa anasafiri na ni mtu mzima.
4. Ripoti inahoji Kabendera kubadilishiwa mashtaka haihoji watuhumiwa wengine wanaobadilishiwa mashtaka kila siku kwa mujibu wa sheria. Inasema Kabendera ni Mwandishi wa nchi za Nje aliyekamatwa Tanzania. Hivi ukifanya mambo kwa maslahi ya nchi nyingine si ujasusi huo!!!
Huyo Kabendera alikuwa anawafanyia nini mpaka atetewe peke yake kuliko mamia ya watu walioko kortini? Tutajua tu.
AMNESTY mnafeli wapi?? Nilikuwa nawaheshimu sana ila kwa ripoti hii mliyotumia katuni za kuchora badala ya picha mmethibitisha nia yenu ilikuwa na walakini.
5. Ripoti yenu inahoji mnaowaita wapinzani walioshtakiwa Mahakamani haihoji watu wenye chama kinachoongoza dola kibao walioko kortini au waliopata kufikishwa kortini kama akina Mramba, Yona, Badwel, hata Kangi Lugora. Ripoti yenu ikae kando, ni ya kipuuzi mtu.
Mwisho kituko cha karne, wameandika eti Tanzania inakataza _false news_ hivyo sheria zake ni kandamizi, kwa hiyo mlitaka hili Taifa liwe na Fake News?
Waandishi wote wa habari akiwemo aliyesoma report Shushushu Muthoki Mumo, nchi zao zinakataza _Fake News_ , lakini katika report wanafeli wapi kwa kuitaka Tanzania ilegeze mafake news? na Wanasiasa uchwara wanaishabikia! Uwezo wa kufukiri mdogo kabisa.
Nyie ni wapumbavu na malofa, in Mzee Mkapa's voice, hampaswi hata kujibiwa. Nchi lazima isonge mbele!