Amnesty International and Human Rights Watch: Hali ya ukandamizaji wa vyombo vya habari, watetezi wa haki za binadamu na vyama vya upinzani waongezeka

Amnesty International and Human Rights Watch: Hali ya ukandamizaji wa vyombo vya habari, watetezi wa haki za binadamu na vyama vya upinzani waongezeka

Jamani tusiwalaumu waandishi wa habari. Wamiliki wao wameishawakataza kuandika habari yoyote ya kuikosoa serikali. Aidha, uhai wao uko hatarini, kumbukeni hakuna stori yenye thamani kuliko uhai.
 
Uzuri ni kwamba UJUMBE UMEFIKA na umekugusa na kukusugua ipasavyo! Unawashwa eeeh, jikune ukaoge...
 
jamani tusiwalaumu waandishi wa habari,wamiliki wao wameishawakataza kuandika habari yoyote ya kuikosoa serikali,aidha uhai wao uko hatarini,kumbukeni hakuna stori yenye rhamani kuliko uhai
Dah! Kwa ninavyojua kazi ya uandishi wa habari ilivyo, yaani unaogopa kukosoa halafu unazidi kujiita mwandishi wa habari. Basi huyo si mwandishi wa habari, ingefaa afanye kazi zingine.
 
Taasisi moja imehoji watu 80 nyingine watu 68 kisha imekuja na majibu kwa ajili ya watu milioni 45.

Simaanisha waliyoyasema hayapo ila sample yao ni ambayo chuo niliruhusiwa kuitumia kwa idadi ya watu wasiozidi 150.

Pia mimi mihangaiko yangu hainipi muda wa kuangalia TV au kusikiliza radio lakini juzi nilikua sehemu zile fremu hii ina kelele ya subwoofer na inayofuata na inayofuata na hapo nilisikia hii ishu ya Amnesty ikiwa inasomwa kama kichwa cha habari.

Sikufuatilia ni radio gani as hii siyo mara ya kwanza Amnesty kuinyyoshea kidole Tz na Tz siyo nchi ya kwanza kunyooshewa kidole na Amnesty.
 
Vyombo makini vya habari nchini vimepuuuza kwa sababu inawezekana waliyoandikwa kwenye ripoti ni tofauti na hali halisi!

Ni sawa na mtu kutoka nje aandike habari kuhusu nyumba yako halafu eti ukulazimishe kuwa aliyoandika ni kweli wakati wewe ndiye mwenye nyumba na unaishi kwenye nyumba hiyo.
 
Tanzania inageuka kuwa North Korea nyingine.Mtawala ndio kila kitu!
 
Vyombo makini vya habari nchini vimepuuuza kwa sababu inawezekana waliyoandikwa kwenye ripoti ni tofauti na hali halisi!

Ni sawa na mtu kutoka nje aandike habari kuhusu nyumba yako halafu eti ukulazimishe kuwa aliyoandika ni kweli wakati wewe ndiye mwenye nyumba na unaishi kwenye nyumba hiyo.
Wewe lini utaacha kumsifu na kumuabudu Jiwe?Kama vyombo Vya habari vingepuuza basi vingeandika kuikandia hiyo ripoti.Kukaa kimya ina maana kuna kitu hakipo sawa .
 
Wewe lini utaacha kumsifu na kumuabudu Jiwe?Kama vyombo Vya habari vingepuuza basi vingeandika kuikandia hiyo ripoti.Kukaa kimya ina maana kuna kitu hakipo sawa .
Na wewe utaacha lini kutomsifu na kutomuabudu Jiwe?

Nani alikuambia upuuuzi hujibiwa na mtu asiyempuuzi? Upuuzi hupuuuzwa kama walivyopuuza wanahabari makini/vyombo vya habari makini ripoti ya kipuuzi!
 
Navipongeza vyombo vyetu vya habari hiyo taarifa haina tofauti na ile inayosema tanzania kuna ebola kila siku wanatuchafua kwa habari za uongo.
 
Ukiripoti habari hizi chombo chako kinakutana na rungu la dola.
Vyombo vyetu vya habari vimekuwa vya kusifia Kila kitu, hata matamko ya wachawi na waganga tunayapongeza na kuyapa uzito front page
 
Watu wanaogopa kutekwa,tutarajie kupata habari za mapambio tu anayoyataka mkuu
 
Na wewe utaacha lini kutomsifu na kutomuabudu Jiwe?

Nani alikuambia upuuuzi hujibiwa na mtu asiyempuuzi? Upuuzi hupuuuzwa kama walivyopuuza wanahabari makini/vyombo vya habari makini ripoti ya kipuuzi!
Kwahiyo Mahiga aliesema Serikali itajibu ripoti hiyo ni mpuuzi...kama riziki yako ipo kwa kumlamba viatu Magufuli sio wote wako ivo
 
Kuna Mambo Hayakushupaliwa uko nyuma, Clouds tv wanatangaza habari ya birthday ya magufuli utafikiri nayo ni habari inapewa promo utafikiri ina faida yeyote kwa nchi mbona wakina kikwete hawakupewa promo kama uyu?

watu wanasombwa na mafuriko media zipo busy na birthday duh.
 
Ya zimbambwe yalianza hiv hiv watu walichekelea sana lakini vikwazo walivyowekewa wanasaga meno endeleeni kupuuza msifikiri hawaoni
Mkuu unajua ulichokiandika kuhusu kuwekewa vikwazo Zibambwe?

Unaujua Muktadha wa kufanya utafiti wa Amani?

Kuna haja gani ya kupoteza mda kujibizana na Taarifa iliyotengenezwa na genge la Wachache tu?
 
Kwahiyo Mahiga aliesema Serikali itajibu ripoti hiyo ni mpuuzi...kama riziki yako ipo kwa kumlamba viatu Magufuli sio wote wako ivo
Kwa hiyo kama Mahiga amesema? Hoja ni kujibu na sio kusema atajibu. Kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti.

Acha kuniwekea maneno. Ni wapi nimesema wote wanalamba viatu vya Magufuli?

Kama nalamba viatu vya Magufuli, tatizo lako ni nini? Huu ni uamuzi wangu na sikuwahi kukuomba ushauri!

Jikite kwenye mada achana na maisha yangu!
 
Eti sheria zote zifutwe. Wakati hizo sheria hazipo je zilitusaidia kuleta maendeleo kama haya yanayofanywa na serikali ya JPM.

Tena nashauri ziongezwe sheria na zipewe ukali zaidi ili wapuuzi wachache kama waliomzushia kifo Mh. Rais wakamatwe vinzuri na kupewa adhabu kali.

Ni ujinga kuendekeza the so called uhuru usiokuwa na mipaka.
"Maboso" =Makapi/machicha ya local bear....
 
Back
Top Bottom