Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Katika taarifa yao waliyoitoa kwa Umma, shirika lisilo la kiserikali la Amnesty international linalojihusisha na haki za kibinadamu limeona uwezekano wa mamlaka za Kenya kulazimika kumrejesha Mwanasiasa wa Upinzani, Godbless Lema au familia yake kwenye mateso ya kisiasa au uwezekano wa kufungwa Tanzania.
Mkurugenzi wa Amnesty International nchini Kenya, Irungu Houghton amesema kanuni ya kimataifa iliyoridhiwa na sheria za Kenya hairuhusu Kenya kuwarudisha watu kwenye mipaka kwenye nchi ambayo wamo kwenye mateso au hatari.
Karibuni, Godbless Lema alikimbilia nchini Kenya na mkewe na watoto watatu akiomba hifadhi kutoka serikali ya Kenya. Lema na familia yake walivuka mpaka wa Namanga Novemba 8, 2020. Amnesty inaamini yupo chini ya polisi eneo la Kajiado, Kenya. Wakili wake, Prof. George Wajackoyah pia amethibitisha uwezekano wa kurejeshwa.
PIA, SOMA: Godbless Lema akamatwa Kajiado akitorokea Kenya yeye na familia yake. Kurudishwa nchini kesho Novemba 9, 2020