Uchaguzi 2020 Amnesty International yazitaka UN, AU, SADC and EAC kuibana Tanzania, Rais na Waziri Mambo ya Ndani kuhakikisha Uchaguzi huru na wa haki

Fatou bensouda anatroti anajiandaa kama namuona vile
 
Unajua,hata wewe uliyeleta hii mada ulipaswa kuona mbali.Hivi huoni kwamba Amnesty International ilitakiwa kuibana UN kuibana Marekani kwanza ambako haki za binadamu zinaminywa kila kikicha na haki ni mbaya zaidi?Hivi huoni kwamba America is degenerating fast into a failed state.Mbaya zaidi Trump ameshasema hata heshimu matokeo ya uchaguzi.Democrats nao wanafanya kila mbinu chafu kuiba kura kwa sababu uchaguzi umeshaanza.Jambo la ajabu ni kwamba sijasikia Amnesty International wakiitaka UN iibane Marekani ili kuwe na uchaguzi huru na haki,huku ikionekane wazi kwamba Marekani hali ni mbaya zaidi.Mimi frankly sioni shida Tanzania Waache double standards zao,their hands off Tanzania,hatuwahitaji!
 
Ccm sikio la kufa
 
Sheria za Tanzania zilizotungwa na Bunge halali la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haziwezi kufutwa kwa matakwa ya shirika binafsi la nje.
Nadhani sheria zetu huenda zisiwe na shida sana ila shida ikatokea kwenye utekelezaji wake - sasa ni vizuri tuchukuwe ushauri wao (kama upo mzuri) ili kuwa na taifa lenye mshikamano

Prof Mukandala amewahi kusema hivi " baba wa nyumba waweza kuwapa nyama na samaki kila siku lkn bado ndani ya familia kukakosa utulivu". So, tuwe na mambo ya kujifunza ikiwa ni pamoja na:-
(I). Kukubali kukosolewa - kwamba siku sote tuchukulie kuwa kukosolewa kunakufanya mtawala ajifahamu kariba yake na kutafuta njia ya kujisahihisha;

(ii). Kutolewa Uhai na kusababishiwa ulemavu - hii libaki kuwa kusudio la muumba wetu "Mungu" - hata kama binadamu wenzetu watuudhije tusiruhusu damu zao kumwagika i.e Bensaanane, Kanguye, Masabo, Lissu nk nk

(iii). Ushindani wa kisiasa: - turuhusu ushindani wa kisiasa unaojengwa na utoaji hoja ili mwisho wa siku vyama vyote vitii mamlaka ya raia na wananchi ktk uchaguzi. Nchi nyingi zinazoendelea zina matatizo makubwa ya kupoka, kukandamiza, na kudhurumu haki za wapigakura kipindi cha uchaguzi.

Ninayo mengi lkn muda nao ni tatizo lkn sote tuendelee kuipenda nchi yetu
 
Shirika la Kimataifa la Utafiti wa masuala ya Siasa kutoka China limepinga vikali ripoti ya Amnesty International kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania na kudai ni ripoti iliyoegemea upande mmoja. Shirika hilo limehoji taratibu na vigezo vilivyotumiwa na Amnesty kuhoji makundi hayo ya watu na taasisi walizotaja kwenye utafiti wao. Shirika hilo limeenda mbali zaidi na kudai kuwa japo Amnesty wanajitanabaisha kama taaisisi inayotetea haki, hawaoni haki iliyotumika hapo kwenye utafutaji wa maoni.

Shirika hilo limeshangazwa na Amnesty kudai kuwa kumekuwa na matukio ya utekaji, ukamataji na unyanyasaji wa wapinzani kipindi cha kampeni ambapo imeonyesha kuegemea upande mmoja wakati wapo wanachama na wafuasi wa CCM waliouawa na kuumizwa na wapinzani.

Shirika hilo limesema utafiti wa Amnesty ni upotoshaji wa wazi kabisa wenye lengo la kuitumbukiza nchi ya Tanzania katika matatizo makubwa. Ni wazi kuwa taasisi ya Amnesty inafanya haya kwa maslahi fulani. Amnesty imelalamika kuhusiana na Vyombo vya Habari kufungiwa huku ikisahau Tanzania ni nchi huru na ina sheria na taratibu zake kwa watu au taasisi zinazokiuka sheria za nchi.

Kwa mwenye akili timamu lazima ashangae haya yanayoendelea kutoka kwa Taasisi inayojiita inatetea Haki na Demokrasia kwa wote bila ubaguzi ya Amnesty International.

Baada ya uchaguzi wa 2015 na John Pombe Magufuli kushinda Urais alianza kazi kwa kishindo na kufanya mengi makubwa ambayo hayakutegemewa katika Ulimwengu ya karne ya 21. Utendaji wa Magufuli uliibua makundi, kwa upande mmoja wakisifia kupatikana Kiongozi bora na imara asiyeyumbishwa anayeweza kuikomboa Afrika tena toka mikononi mwa wakoloni mamboleo na kwa upande wa wezi wa rasilimali za Watanzania ukiacha maumivu makali.

Makundi yenye maumivu yameamua kujitokeza hadharani kupambana na Magufuli yakitumia watu na vyombo mbambali vya habari, wanaharakati, taasisi zisizo za kiserikali, wanasheria na wanasiasa kumkwamisha na kumchafua Magufuli.

Mataifa hayo sasa yameamua kutumia uchaguzi huu kuhakikisha Magufuli harudi madarakani kwani amekwamisha mambo yao mengi na yanatumia watanzania wenzetu kuihujumu nchi yetu kwa maslahi binafsi.

Bila aibu Amnesty International imediriki kutoa makala ya kumshambulia Magufuli wakidai kuwa wapinzani wamekuwa wakionewa. Nasema ni aibu kwani kama Amnesty inasimamia haki kwa wote ilitakiwa kukemea pia mauaji ya vijana na wafuasi wa CCM yaliyofanywa na vijana wa CHADEMA tena ambao wamekiri kufanya matukio hayo.

Amnesty walitakiwa kukemea tukio la wafuasi wa CCM kukatwa mapanga ndani ya Msikiti na mwananchama wa ACT Wazalendo.

Amnesty walitakiwa kukemea suala la vijana wa CCM kushambuliwa maeneo mbalimbali ya mwili na wafuasi wa CHADEMA kama mikoa ya Arusha, Morogoro, Njombe, Mbeya na kadhalika.

Swali fikirishi, ina maana Amnesty wanatetea tu wanachama wa CHADEMA? Hii ni taasisi maalumu kwa ajili ya CHADEMA? Je wana maslahi gani kwa CHADEMA ikiingiia madarakani?

Wakati huu ndio tunaona mashirika ya kipumbavu kabisa kama hili la Amnesty linalojaribu kuleta machafuko nchini kwa kivuli cha kutetea haki. Ni haki gani wanayotetea angali watanzania wameuawa bila hatia au kwa kuwa si wafuasi wa CHADEMA?

Amnesty International wanapaswa kufahamu tu kwamba Watanzania sasa wameamka, John Pombe Magufuli ameamsha watanzania. Hawako tayari tena kuona rasilimali zao zikifaidisha watu wa mataifa mengine na ambao wametukandamiza kwa kipindi kirefu.

Amnesty wanatakiwa wajue kuwa mipango yao na nia ovu waliyonayo inajulikana na haitafanikiwa dhidi ya Tanzania. Mungu aliyetuponya na Covid19 ndiye huyo huyo atakayetuepusha na wabaya wetu. Kamwe Tanzania haitaingia kwenye machafuko kama wanavyopanga na tutaendelea kuwa na amani chini ya John Pombe Magufuli.

*Niwaombe watanzania wenzangu, tuwe makini sana na hizi taasisi, wanasiasa na watanzania wenzetu ambao wamejitoa kutumika kwa maslahi ya mabeberu. Tuwakatae kwa nguvu watatuangamiza.*

*Shime Watanzania, tarehe 28/10/2020 twende tukapige kura kumchagua mzalendo wa kweli JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI kiboko ya mabeberu*
 
CNN, VOA, DW, Amnesty Internation ni Vibaraka wa Mabeberu tangu siku nyingi sana.
Hawa ndio husababisha maasi mengi Duniani.
Marekani waliifanya nini ilipoivamia IRAQ na kuua wengi wasio na hatia miaka ile.
 
JAMANI IVI MNAFAHAMIANA NA MA.ADMIN WA JF?? MIMI NIKIMUITA TU MTU MPUMBAFU NAKULA BAN YA WIKI, YANI MWENZENU SINA RAHA KABISA NA PIA SIKO HURU UMU JANVINI, YOTE MAISHA
Lazima ufahamu Chadema wameiteka JF au kuinunua kabisa.
 
Return from exile!!makubwa haya !! Kwa hiyo alikuwa mkimbizi?? Tangia lini?hivi mnajua sheria za kuwa mkimbizi zikoje?? Nani alimpa ukimbizi? Ndiyo maana tunasema huyu katumwa kuvuruga amani ya nchi
 
Eti Maccm hayataki TunduALissu alale Chato, yaani ni hivi mtake msitake leo TL atalala chato, nyie si mnajikuta watalaam wa kutoa roho za watu basi jaribuni leo muone, nyambafuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninamuonea huruma yule jamaa mwizi wa PhD. Ataitwa mahakama ya kimataifa ataongea kisukuma english 0, kiswahili 0. Itakuwaje?
 
Reactions: BAK
Ikitokea unaandika,unafuta mara kadhaa nibora ukaacha kuchangia huo uzi

Nimeachana na uzi huu
 
JAMANI IVI MNAFAHAMIANA NA MA.ADMIN WA JF?? MIMI NIKIMUITA TU MTU MPUMBAFU NAKULA BAN YA WIKI, YANI MWENZENU SINA RAHA KABISA NA PIA SIKO HURU UMU JANVINI, YOTE MAISHA
Wewe toa hoja, Matusi ya Nini? Tatizo humna hoja ndiyo Mana mnaishia kupanic na kutukana watu. Toka huko upande wa DHURMA, pigania HAKI ndiyo utaishi kwa Amani siyo tu humu JF Bali hata Mitaani.
 
Ni Mbinyo mbinyo, mwaka huu 2020 CCM haichomoki kupitia rafu zake.

waTanzania wasema sasa basi! Jumuiya za kimataifa wapo upande wa waTanzania watakaochagua mabadiliko.
Ukisema Watanzania una maana gani?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…