Amos Makala apokelewa Wilayani Karatu, afanya mazungumzo na Viongozi wa CCM na serikali kutoka Ngorongoro

Amos Makala apokelewa Wilayani Karatu, afanya mazungumzo na Viongozi wa CCM na serikali kutoka Ngorongoro

Hana Cha maana huyo anadandia dandia matukio tu. km wasanii wa bongo movie
 
Kwa sera na ajenda zipo mlizonazo CHADEMA mpaka muogopwe? Hivi kwanini huwa mnakosa akili na ufahamu kiasi hicho? Kwanini mnakuwa vipofu wa akili na macho? Hivi CHADEMA iliyojichokea na kupoteza muelekeo inaanzia wapi kuwa tishio kwa CCM hoi iliyo imara na madhubuti kila uchao???
Jibu hojaa weee
Acha matusii ,mkishikwaga pabaya ndio mnakuwa na matusii ,cheki huyo mwenzako amepewa demands notice tuu anabwabaja tuuu

Nawee naweza kukupa notice utoe ushahidi kama nimekosa akili.
Sasa kama hatuna akili na sera

Muambie mwenyekiti wako unayemlamba miguu atoe siku moja tuu hata kwa LEMA aende ngorongoro afanye mkutano mmoja tuu
Kama hamjapoteana na kuanza kuteka watuu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi,uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa CPA Amos Makala Amepokelewa kwa shangwe, nderemo na vifijo vingi sana na maelfu ya wananchi wa Karatu katika uwanja wa mazingira bora wilayani Karatu.

Ambapo ni muendelezo wa ziara yake katika kupokea ,kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.ambapo imeshuhudiwa maelfu ya wananchi wakifurika na kumiminika kwa wingi kama mchanga wa baharini kumlaki mtaalamu na nguli huyu wa Mahesabu hii ni kutokana na imani kubwa sana waliyonayo wananchi kwa CCM chama ambacho kimebeba matumaini ya mamilioni ya watanzania.

Lakini vilevile Mheshimiwa CPA Amos Makala ambaye amewahi kuwa mhazina wa CCM Taifa ameweza kuzungumza pia na viongozi wa CCM pamoja na serikali kutoka Ngorongoro.

Ikumbukwe wakati viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa ziarani maeneo mbalimbali Nchini,kama tunavyoshuhudia naibu katibu mkuu Bara naye akiwa ziarani mkoani singida ,huku naye naibu katibu mkuu Zanzibar naye akiwa ziarani,.hali imekuwa ni ya kusikitisha na kutia huzuni sana kwa CHADEMA chama kilichojikatia tamaa na kupoteza matumaini.

Hakuna mikutano wala ziara wala nini zinazofanywa na viongozi wa CHADEMA.hii ni kutokana na kushindwa na kuishiwa sera na ajenda za kuzungumza kwa wananchi.ndio sababu unaona chama kimekata pumzi na kupoteza muelekeo kabisa.

Kwa hakika CCM ndio nguzo kuu ya Taifa letu na chemchemi ya matumaini ya mamilioni ya watanzania.hakuna Tanzania yenye maendeleo na utulivu pasipo CCM madarakani.ndio sababu kwa usikivu wake CCM inaendelea kuaminika na kuaminiwa na watanzania na kuungwa mkono kila uchao.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Sensema hiii hiii
 
Back
Top Bottom