Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC), Itikadi Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema siasa sio ugomvi wala vita, hivyo amepongeza kuona kiongozi wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) akiwatambulisha wagombea wa CCM.
Makalla amesema hayo leo Novemba 24,2024 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ukonga Wilaya ya Ilala Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
“Sikushangaa jana kuona kiongozi wa kitaifa wa TLP akiwatambulisha wagombea wa CCM sijashangaa kuona kiongozi wa Vijana TLP taifa katika mkutano huu,” amesema CPA Makalla.
Ameongeza viongozi hao wamejitokeza kuunga mkono CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na kukubali juhudi zilizofanywa na chama hicho katika maendeleo sehemu mbalimbali nchini.
Makalla amesisitiza kupitia mikutano ya kampeni ambayo wanaifanya nchi nzima bado wanaendelea kupokea maelfu ya wanachama kutoka vyama vya upinzani, hivyo inaonesha wazi imani wananchi waliyonayo kwa CCM ni kubwa.
Aidha, Makalla amesema kuwa viongozi hao ni watu muhimu sana katika masuala ya ulinzi na usalama huku akieleza ushirikiano waliowahi kumpatia kutatua tatizo la ‘Panya rodi’ alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
Sambamba na hayo, Makalla amesema CCM wanatembea kifua mbele kwa ajili ya kiongozi wao ambaye ni mwenyekiti kitaifa Rais Samia Suluhu Hassan na 4R zake na fedha anazozitoa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Akizungumzia maendeleo yaliyofanywa na serikali ya CCM katika jimbo hilo amesema maji safi ya bomba yalikuwa ni historia na hadithi za kusadikika kwa wananchi wa eneo hilo lakini mbunge wao kupitia tiketi ya CCM, Jerry Silaa aliwapigania kuhakiisha wanapata miradi ya maji safi.
Makalla ameongeza akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alipata nafasi ya kusimamia ujenzi wa madarasa ya UVIKO na katika jimbo la Ukonga walipata bahati ya kupewa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mengi zaidi kuliko majimbo yote.
Chanzo: Habari Leo