Amos Makalla: Sisi tunatatua kero Kisayansi, hatupigi kelele

Huyu jamaa sijui ana matatizo Gani ,mtu mzima lakini hajitambui.
 
Kauli kama hizi zinaonyesha CCM walivyo na mashindano. Yaani kuna CCM ya wenye kelele na wasio na kelele. Fanyeni kazi msaidie watanzania acheni kujilinganisha nyie kwa nyie
 
hatuwezi kupiga kelele sana, mambo mengine yanahitaji faragha, ndio maana tunatatua kero zetu kisayansi, kimyakimya tunatangaza tumefanya moja mbili tatu.
Yale yale ya Shukuru Kawambwa alisema anafanya kazi kama mchwa wakati huo akikutana na wataalamu wa elimu anawaambia hiyo wizara haielewi kabisa
 
Dongo lingine hili kwa Makonda dadeq
 
Unajua serikali inavyofanya kazi lakini?
Hembu taja kero 10 ambazo makonda alifanikiwa kuzitatua na sasa hazipo tena. Anza na ile ya kuahidi kutoa matrekta ili barabara za kawe zitengenezwe
Twende kazi
Nyamitako alikuwa anafanya sanaa za majukwaani tu hakuna kero hata moja aliyotatua kwa vile hakuwa na uwezo huo.
 
Makonda alikuwa anasikiliza lakini si kutatua, ni mara ngapi amehoji wahusika wafanyie kazi na hawajafanyia? Wakaishia kumuangalia tu? Hizi ni politics tu ila kwa style tofauti
 
Huyu jamaa hajijui tu..
Cheengaa...!🤣🤣😂
 
Kifupi wewe haumpendi Makonda binafsi kutokana na ubishi unaoujenga kwa hoja za wazi zenye ushahidi wa kuonekana.

Katika mjadala huu walio wengi wanamfagilia Makonda kwa mfumo wake wa kushughulikia kero za watu.

Kwa Tz tulipofikia sasa, kero za watu si za kuchukuliwa poa kama unavyodhania wewe.

Maana yake ni kwamba, kero zilizostahili kuchukuliwa hatua na viongozi wateuliwa, kero hizo hazichukuliwi hatua yoyote hadi chama kinapoingilia ndiyo raia wanapata ufumbuzi wa kero zao, angalau kwa kuwaelekeza panapostahili kuzipeleka.

Wewe unaliongeleaje hilo!

Na hili la raia kufurahia kila Makonda alipotia mguu wake nalo unalichukuliaje pia?

Toa mfano wa ufanisi wa viongozi wenye mrengo wa siasa za namna ya Makala wanaokubalika na wananchi.

Sasa wewe kaza fuvu lako kupingana na hadhira inayomuunga mkono Makonda kwa utendaji wake bora kabisa unaoungwa mkono na 90% na Raia wote wapenda maendeleo.
 
Hiyo ndio ya wenye akili, yule popo alikuwa anatafuta kiki kwa kuwapumbaza wajinga
 
We ndio zuzu la huyo bashite. Ametatua kero ipi
 
Bashite alikuwa anafanya komedi hakuna kero alitatua we bwege
 
Kama miaka sitini imepita lakini bado mnatatua kero za madawati, vyoo, umeme, dawa hospitalini, barabara, makazi bora n.k. basi hiyo inabidi mbadilishe hiyo sayansi.

Amandla...
 
Makonda alisema mawaziri wawe wanatoa ripoti zao Kila baada ya mwezi. Mtaje hata waziri mmoja aliyetii hiyo amri ya muhalifu.
 
TUNAGUGU
 
Kijembe kwa Makonda
 
Dongo kwa bumunda bashite
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…