Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amos Makalla, ameeleza kupata ukakasi mkubwa kuhusu hatua ya kiongozi ambaye ni mwanasheria na anayejua haki na demokrasia, lakini anakataa kutumia haki yake ya kupiga kura. Hili limejitokeza baada ya Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, kutotimiza wajibu wa kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika Novemba 27.
Akizungumza leo Oktoba 22 wakati akipokea ripoti ya Uandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam, Makalla amesema, "Nionesheni mahali popote Tundu Lissu akijiandikisha. Inaingia kwenye rekodi kuwa hatopiga kura katika nchi hii kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Lakini tutarajie kelele za kuhoji matokeo, wakati hata kura yake hana."
Pia, Soma:
+ Tundu Lissu mbinafsi, hajajiandikisha kupiga kura awapigie wengine lakini 2025 atataka watu wampigie kura
+ Amos Makalla: Tulipokuwa tunajiandaa na Uchaguzi wenzetu walikuwa kwenye Maandamano!