Hapo Miaka ya 2000-2008 pamemwaga wengi Sana.
Kuna mahali baada ya same kabla ya Mwanga sijui wanaita Mgagao wanachoma sana Mbuzi, pale pana maji wakati wa mvua zinaweza piga milimani, maji yanakuja kimya kimya, ukikutana nayo barabarani huna Bahati!
lugha yako Kali nduguKila siku huwa nasema hapa kusafiri katika barabara za Tanzania ni HATARI na kutembea na KIFO.
Waafrika hasa watanzania bado hawawezi kutumia barabara kwa usalama.
Mijitu inajiendea tu, pakachu pakachu kama mapanya.
Sahihi Kabisa
Sema barabara ya Dar to Arusha ni nzuri Sana tofauti na barabara ya Dar to mwanza, hasa maeneo ya Morogoro to Dodoma,
Na dodoma to Singida.
Barabara mbovu sana
WameruSasa nnko ni nan? Ni wachaga
Dar to Arusha ni barabara nzuri sana, ila Ukifika njia panda nyakati za saa 12 au 1 jioni Kama wa enda Arusha ina boa sana kwa jama, malory mpaka umalize Boma mpaka Kia inaachia, inaanza tena Kuwa ngumu baada ya kile kilima cha kikatiti kuelekea maji ya chai
On the way to Arusha 2021 nipo na Audi A4 saloon 2.0 quattro nilikuwa naenda hadi 240 km/hr Sitafanya huo ujinga tenaEneo la Same,Huko Kilimanjaro,linahitaji maombi
Mmeru huyu alikuwa anawahi X-MasR.i.p MANGI inauma sana
Ndio, kagonga Tata bus, upande WA dereva yaani Prado nimeidharau kwenye usalama, bus limeumia kidogo Tu!Kuna taarifa kuwa amegongana na bus! Kuna ukwelj au ?
Hili eneo la Same limechukua maisha ya watu wengi sana toka kitambo....wazee wa maeneo yale walitujuza kwamba wakati wa ujenzi wa barabara ya lami...ile ya kwanza kuna mdau aliingia mitini na vifaa vya kufanyia matambiko,,,,,,,matokeo yake ndio hayo...na jinsi tunavyo dharau mila na tamaduni zetu itaendelea kutugharimu sana....labda kwa sababu huyu aliyefariki sasa ni mkubwa inaweza kuwaamsha kiakili na kifikra......nakumbuka hapa kuna rafiki yangu ni marehemu kwa sasa Dr.Mathew Mandara gari yake ilibebwa na upepo ikaruka kama karatasi umbali wa kama mita 70 mwanae Lulu alifia hapohapo(R.I.P)Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.
Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.
βMipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,β imeeleza taarifa hiyo.
Tambiko mila desturi na tamaduniKipande cha Makanya to Same kinakuwaga na viajali vya Hapa na pale wakati Njia imenyooka barabara nzuri.
Nafikiri tatizo ni upepo mkali eneo hilo
Double lane hazikwepeki,ukienda America mostly north every high way ni double lane na sky flyover za kutosha,hapa dhahabu na madini kibao,bibi anapeleka Zenji,tuboreshe Barabara zetu zimepitwa na wakati na zote Zina.mashimo.Hizi kweli ni ajali za kawaida? Unaweza kuwa wewe unaendesha kwa umakini lakini midereva mengine ni selfish yanaendesha hovyo hovyo bila kufuata sheria ama yana stress na yamelewa na kusababisha ajali kupoteza maisha na kujeruhi na kuleta huzuni kwenye jamii.
Pia miundo mbinu ya bara bara zetu siyo nzuri.
Pia vyombo vya usafiri magari.
Mwendo kasi pia inachangiaga sana kwenye ajali.
Yani ni kama wote sasa hivi tukitumia barabara tunaishi kwa kubahatisha.
Mungu awalaze zayuni.
Tunaishi tukijua tutakufa; tunakufa tukijua bado tunaendelea kuishi.Alijiandaa kwenda kusheherekea krismas na familia yake kumbe ndio alikuwa anakifata kifo chake......pole nyingi Kwa familia
Mwenyezi Mungu awape pumziko lenye amani.
Ila Wakuu barabarani tuwe wapole na makini sana hasa wale wa magari yenye ving'ora kwenye dashboard.
Nimeshuhudia mara kadhaa wakifanya overtaking kwenye alama ya pundamilia, na kutanua bila sababu za msingi.
Ajali na kifo havitambui vyeo na uchumi wako.
NB: Ushauri hauna uhusiano na tukio kwenye uzi.
Pale ni kama bonde la uvuli wa mauti.Nimepita sana hayo maeneo nikidrive kwenda Moshi......Nikifikaga mitaa ya Makanya kuelekea Same- Mwanga huwa nakuwa mpole