TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

Kuna mahali baada ya same kabla ya Mwanga sijui wanaita Mgagao wanachoma sana Mbuzi, pale pana maji wakati wa mvua zinaweza piga milimani, maji yanakuja kimya kimya, ukikutana nayo barabarani huna Bahati!

Sahihi Kabisa

Sema barabara ya Dar to Arusha ni nzuri Sana tofauti na barabara ya Dar to mwanza, hasa maeneo ya Morogoro to Dodoma,
Na dodoma to Singida.
Barabara mbovu sana
 
Kila siku huwa nasema hapa kusafiri katika barabara za Tanzania ni HATARI na kutembea na KIFO.

Waafrika hasa watanzania bado hawawezi kutumia barabara kwa usalama.

Mijitu inajiendea tu, pakachu pakachu kama mapanya.
lugha yako Kali ndugu
 
Sahihi Kabisa

Sema barabara ya Dar to Arusha ni nzuri Sana tofauti na barabara ya Dar to mwanza, hasa maeneo ya Morogoro to Dodoma,
Na dodoma to Singida.
Barabara mbovu sana

Dar to Arusha ni barabara nzuri sana, ila Ukifika njia panda nyakati za saa 12 au 1 jioni Kama wa enda Arusha ina boa sana kwa jama, malory mpaka umalize Boma mpaka Kia inaachia, inaanza tena Kuwa ngumu baada ya kile kilima cha kikatiti kuelekea maji ya chai
 
Dar to Arusha ni barabara nzuri sana, ila Ukifika njia panda nyakati za saa 12 au 1 jioni Kama wa enda Arusha ina boa sana kwa jama, malory mpaka umalize Boma mpaka Kia inaachia, inaanza tena Kuwa ngumu baada ya kile kilima cha kikatiti kuelekea maji ya chai

Sahihi Kabisa
 
Automatic majukumu nayo ni stress mtu anapiga gia huku simu na maelekezo kibao toka juu na malalamiko toka kwa staffs ni trouble concentration ya barabarani inapungua,rest in peace Nko
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

Hili eneo la Same limechukua maisha ya watu wengi sana toka kitambo....wazee wa maeneo yale walitujuza kwamba wakati wa ujenzi wa barabara ya lami...ile ya kwanza kuna mdau aliingia mitini na vifaa vya kufanyia matambiko,,,,,,,matokeo yake ndio hayo...na jinsi tunavyo dharau mila na tamaduni zetu itaendelea kutugharimu sana....labda kwa sababu huyu aliyefariki sasa ni mkubwa inaweza kuwaamsha kiakili na kifikra......nakumbuka hapa kuna rafiki yangu ni marehemu kwa sasa Dr.Mathew Mandara gari yake ilibebwa na upepo ikaruka kama karatasi umbali wa kama mita 70 mwanae Lulu alifia hapohapo(R.I.P)
 
Hizi kweli ni ajali za kawaida? Unaweza kuwa wewe unaendesha kwa umakini lakini midereva mengine ni selfish yanaendesha hovyo hovyo bila kufuata sheria ama yana stress na yamelewa na kusababisha ajali kupoteza maisha na kujeruhi na kuleta huzuni kwenye jamii.

Pia miundo mbinu ya bara bara zetu siyo nzuri.

Pia vyombo vya usafiri magari.

Mwendo kasi pia inachangiaga sana kwenye ajali.

Yani ni kama wote sasa hivi tukitumia barabara tunaishi kwa kubahatisha.

Mungu awalaze zayuni.
Double lane hazikwepeki,ukienda America mostly north every high way ni double lane na sky flyover za kutosha,hapa dhahabu na madini kibao,bibi anapeleka Zenji,tuboreshe Barabara zetu zimepitwa na wakati na zote Zina.mashimo.
 
Mwenyezi Mungu awape pumziko lenye amani.

Ila Wakuu barabarani tuwe wapole na makini sana hasa wale wa magari yenye ving'ora kwenye dashboard.

Nimeshuhudia mara kadhaa wakifanya overtaking kwenye alama ya pundamilia, na kutanua bila sababu za msingi.

Ajali na kifo havitambui vyeo na uchumi wako.

NB: Ushauri hauna uhusiano na tukio kwenye uzi.


Ni kweli wabongo wengi wanaendesha vibaya sana magari.
Yaani huwaambii kitu 👌👌
Mwendokasi balaa.
Sijui wana matatizo gani?!
Yaani utasema ni Watu hawana cha kupoteza , wana-bet for life 🤔🤔🤔

overtaking za hatari hawajali wala nini.
Always huwa nasema Mwenyezi aendelee kutunusuru na tuepuke mwendokasi ili akitokea wa kutaka kutusababishia Basi kufa na afe mwenyewe au wenyewe.

Hawataki kufuata sheria na hekima za jinsi ya kuendesha gari kiusalama kwa masafa marefu.
Inasikitisha mno lakini mwisho wa siku mchuma janga atakula na wakwao.
Tujitafakali kwa kweli.
Hulka mbaya sana ya kuzoea na kupenda mwendokasi.
 
Hicho kipande cha Same, Hedaru , Makanya kote huko natembea na 140 mpk 180 and sometimes nakopa 180+... know your car limitations..

Gari ikiwa imetaga (Ground clearance ni ndogo) upepo hauwezi kukuhamisha, ila likiwa juu (Ground Clearance kubwa) lazima ikutoe, hapa sasa inategemea na weight x speed x direction ya upepo..

Tukirud ktk dhana ya Aerodynamics kuna namna ya kufanya chombo kipae ni kwenda against wind.. sasa kiuhalisia upepo unaokatiza huwa hauna shida, shida inakuja pale unapopishana na gari nyingine inayokuja kasi, inagenerate upepo ambao unakutana nao wewe head to head hivyo inatengeneza lifting mechanism bahati mbaya ikishalift gari kwa kiwango flan unakutana na upepo unaokatisha (Cross wind) ambao utakusogeza either kulia or kushoto hapo sasa ndio unakuta mtu anatoka nje ya barabara au anajaa upande ambao sio wake..

Trick: Kimbia uwezavyo ila ikifikia unapishana na gari nyingine punguza mwendo mpk apite ndio uendelee na flat-foot..
 
Huyu jamaa kama vile namjua anafanyia kazi hazina pale posta kalibia na jengo la twiga wamepakana na mwalimu bank

Na juzi juzi nilimuona akiwa na mfuko akitoka kuhemea vitu

Ni mshua flan hivi mrefu mrefu maji ya kunde hanaga noma na mtu kabisa

Kama ni huyo apumzike kwa aman sana
 
Back
Top Bottom