TANZIA Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

TANZIA Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

Mzee wa misiba stevenyerere hajachangamkia fursa bado?!!!
 
TANZIA: Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.

“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,''
View attachment 830443
View attachment 830484
View attachment 830455
Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.

Pia soma >
Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend
Mzee Majuto atangaza rasmi kuacha kuigiza, sasa kumrudia Mungu wake
Mwakyembe Kuivaa kampuni iliyomdhurumu Mil 25 Mzee Majuto.
Haya ndio maisha halisi anayoishi mzee Majuto
--
Wasifu
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.


Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
Sikuwahi kujua jina halisi la mzee majuto kumbe aitwa Amri Athumani....R.I.P baba yetu
 
Sababu hii Kila Mwanaume ana Tezi Dume ambayo kazi yake ni Kuzalidha Mbegu za Mwanaume,Sasa huwa likiwa kubwa ndo Tatizo,Na huwa linakatwa,
Kabla ya hapo linapimwa in terms of Cm na Volume/Length.
Tezi dume (Prostate gland ) haizalishi mbegu za kiume (sperm)

Tezi dume huzalisha maji maji yenye alkaline kwa ajili ya kuzifanya mbegu ziweze kusurvive pia kuzikinga na acid iliyo kwenye uke wa mwanamke

Mbegu za kiume huzalishwa na korodani (testes)
Watu wengi wamekuwa wakichanganya cancer ya tezi dume (Prostate cancer) na Mabusha /busha (elephantiasis of the scrotum)
 
Inna lillah wainna ilayh raajuun!! Allah ampe kauli thabiti
 
May his soul rest in peace.

Forever he 'll be in our thoughts & hearts.
 
Raha ya Milele umpe Ee Bwana, na Mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani. AMINA
 
R.I.P. huyu mzee atakumbukwa sana kwa kweli, ni mtu pekee katka maisha yang sijawah sikia mtu akimsema vbaya, yan hata mara moja. A legend with Zero haters. Kile kicheko chake tu mi nikikumbuka daaaa...... Watu wakufurahsha dunia wanaondoka tunaachiwa ma zinjatropus wanaojibatiza majina kila asubuh.
Tokea enzi za kina bi chau na marehem mzee small aisee
 
Pumzika kwa amani mzee Majuto! Hii dunia kweli tunapita
 
[emoji24] [emoji24] [emoji24] ,very sad for the King Majuto death streaming updates, Upumzike kwa Aman.
Your among Legends
 
Back
Top Bottom