Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Simba, Amri Kiemba, ameweka wazi maoni yake kuhusu uongozi wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, akieleza kuwa huu ndio wakati muafaka kwake kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wapya kuendeleza mchezo huo.
Akizungumza kwa mtazamo wa kiuongozi na maendeleo ya soka nchini, Kiemba amesema kuwa Karia ameshatekeleza mengi katika kipindi chake akiwa madarakani, lakini sasa hali ya mambo inaonyesha wazi kuwa amefikia ukingoni na hana tena msukumo ule ule wa awali.
"Kwa mtazamo wangu, huu ni wakati sahihi kwa kiongozi aliyeko madarakani kama Karia kutofikiria kuendelea. Kwa sababu tayari ameshakamilisha mengi na anastahili kupumzika kwa heshima. Hili ni jambo la busara sana kwa kiongozi yeyote ambaye ameshatumikia kwa muda mrefu"
Aliongeza kuwa kuna hatari ya kuvunjika kwa heshima na hadhi ambayo tayari imejengwa, endapo kiongozi ataendelea kung’ang’ania madaraka licha ya dalili kuonyesha kuwa ni wakati wa kuondoka.
Kiemba amesisitiza kuwa pamoja na kuwa ni haki ya Karia kuamua kuendelea au la, ushauri wake ni kwamba apishe damu mpya yenye ari mpya, ili kuendeleza msingi mzuri aliouacha.
Kauli ya Kiemba imekuja wakati mvutano na mjadala kuhusu uongozi wa TFF ukizidi kushika kasi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo uliopangwa kufanyika Agosti 16, 2025 jijini Tanga.