Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Tuanze na uchunguzi huru wa takukuru...periodmengine yatafuata.....Mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Simba, Amri Kiemba, ameweka wazi maoni yake kuhusu uongozi wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, akieleza kuwa huu ndio wakati muafaka kwake kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wapya kuendeleza mchezo huo.
Akizungumza kwa mtazamo wa kiuongozi na maendeleo ya soka nchini, Kiemba amesema kuwa Karia ameshatekeleza mengi katika kipindi chake akiwa madarakani, lakini sasa hali ya mambo inaonyesha wazi kuwa amefikia ukingoni na hana tena msukumo ule ule wa awali.
"Kwa mtazamo wangu, huu ni wakati sahihi kwa kiongozi aliyeko madarakani kama Karia kutofikiria kuendelea. Kwa sababu tayari ameshakamilisha mengi na anastahili kupumzika kwa heshima. Hili ni jambo la busara sana kwa kiongozi yeyote ambaye ameshatumikia kwa muda mrefu"
Aliongeza kuwa kuna hatari ya kuvunjika kwa heshima na hadhi ambayo tayari imejengwa, endapo kiongozi ataendelea kung’ang’ania madaraka licha ya dalili kuonyesha kuwa ni wakati wa kuondoka.
Kiemba amesisitiza kuwa pamoja na kuwa ni haki ya Karia kuamua kuendelea au la, ushauri wake ni kwamba apishe damu mpya yenye ari mpya, ili kuendeleza msingi mzuri aliouacha.
Kauli ya Kiemba imekuja wakati mvutano na mjadala kuhusu uongozi wa TFF ukizidi kushika kasi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo uliopangwa kufanyika Agosti 16, 2025 jijini Tanga.
Ndolanga alikuwa mtu mzito kuliko Karia lakini Serikali ilipomchoka alishindwa uchaguzi pamoja na kuwanunua wajumbe wote nchi nzima.Tulijua tu zile heka heka za kuikosoa TFF na Bodi yake ilikuwa ni mpango wa kujitengenezea njia ya kuja kugombea uraisi.
Karia sio mpinzani rahisi kwenye box la kura
Kenneth Kaunda alistaafishwa na CIA kihuni mno. Kwa mujibu wa spy mkuu wa zamani wa Zambia ni kuwa miezi 6 kabla ya uchaguzi tayari serikali ya Kaunda ilikuwa inaendeshwa kihuni na walioko nje ya serikali.Hizo busara ni za akina Mandela na Nyerere pekee. Karia atakuwa kama Kenneth Kaunda hadi astaafishwe kwa lazima.
Mimi naona hakuna Rais wa TFF ambaye hatalaumiwa wakati wa uongozi wake kwa sababu ya u-Simba na u-Yanga. Tenga alijitahidi ila naye mwishoni alianza kulaumiwa.Wallace Karia ajifunze kwa watangulizi wake. Baada ya mihula yao miwili, waliondoka madaraka kwa hiyari. Na yeye afuate nyendo zao. Asisubiri kuondolewa kwa nguvu, na kwa aibu.
Na wala asijione ana maajabu ya kuliongoza milele hilo shirikisho la mpira wa miguu nchini! Hayo maajabu hana.
Safari hii wadau wa michezo tunatamani kuona mpira wa miguu ukiongozwa na wenye mpira wao.
Ally Mayay Tembele, ni wakati wako huu wa kuzirejesha zile enzi za Leodgar Chilla Tenga, ambapo TFF iliheshimika na wadau wote wa michezo; ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.
We jamaaa kuna wkt unakuwaga mtu kumbe unajua nguvu za Serikali!!!!!!!Ndolanga alikuwa mtu mzito kuliko Karia lakini Serikali ilipomchoka alishindwa uchaguzi pamoja na kuwanunua wajumbe wote nchi nzima.
Nyerere alistaafishwa bila kupenda na uchumi mbovu.Hizo busara ni za akina Mandela na Nyerere pekee. Karia atakuwa kama Kenneth Kaunda hadi astaafishwe kwa lazima.
Na hizi mbanga za ku mix politics na soccer inaenda kutengeneza demise kwenye mpira wetu.Ndolanga alikuwa mtu mzito kuliko Karia lakini Serikali ilipomchoka alishindwa uchaguzi pamoja na kuwanunua wajumbe wote nchi nzima.
Karia yupo pale kwa mipango.Wallace Karia ajifunze kwa watangulizi wake. Baada ya mihula yao miwili, waliondoka madaraka kwa hiyari. Na yeye afuate nyendo zao. Asisubiri kuondolewa kwa nguvu, na kwa aibu.
Na wala asijione ana maajabu ya kuliongoza milele hilo shirikisho la mpira wa miguu nchini! Hayo maajabu hana.
Safari hii wadau wa michezo tunatamani kuona mpira wa miguu ukiongozwa na wenye mpira wao.
Ally Mayay Tembele, ni wakati wako huu wa kuzirejesha zile enzi za Leodgar Chilla Tenga, ambapo TFF iliheshimika na wadau wote wa michezo; ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.