- Thread starter
- #41
Mbona unajichanganya sasa!Basically Kalamu hivyo ndivyo mataifa/serikali yalivyo/zlivyo, na hapa kwetu ni ngumu sana kutofaitisha chama na serikali au taifa. Viko well connected, mpaka tutakapo badili katiba
Upande mmoja unasema "ndivyo mataifa/serikali yalivyo/zilivyo....."; na hapo hapo unasema "...mpaka tutakapo badili katiba." Huko kwingine nako wanasubiri "kubadili katiba", ili wasiwe kama tulivyo sisi na walivyo wao sasa hivi?
Tatizo lako (lenu) ni kutafuta ku'justify' maovu yanayofanywa na hawa watu waovu kabisa kwa sababu mnazozijuwa wenyewe.
Kama unaona kitu hakifai, sema wazi hakifai, usianze kutafutiza visababu vya kueleza kwa nini ni lazima iwe hivyo. Hili ndilo tatizo ambalo huwa napata shida kubwa katika kujadili lolote na watu wa aina hii, inabaki tu kuzungshana, kona hii, baada ya ile; mkitoka huko kunazuka kona nyingine! Mtindo wa hovyo sana wa kujadiliana kwa kutafuta kuchoshana tu.
Ni sababu hizi hizi ndizo zinazoleta vurugu kila mara katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati; kwa sababu hakuna kujadiliana na kufikia mwafaka na kuaminiana juu ya mlicho kubaliana. Ni utamaduni wa hovyo sana.