Ana mtoto wa miezi mitatu, pia anaujauzito wa wiki tatu

Ana mtoto wa miezi mitatu, pia anaujauzito wa wiki tatu

We lea watakuwa tu ilimradi zingatia lishe kwa huyo mtoto na mama yake maana mama bado hajarecover kushika mimba baada ya kujifungua ni rahisi sana maana mama anaweza akawa hajaona siku zake akajipa moyo na mimba ikatungwa wacha watu wabeze hawajui shughuli yake.
 
hiyo ni kawaida na huwa inatokea sana tu,saa nyengine kama unajisahau na kufikiria mimba haitoingia hapo hapo.watoto watakua pamoja hao.atakuwa amejifunza akijifungua salama,atakuwa muangalifu zaidi
 
Dah kwa kweli akili ilikuwa imevurugika sana jana baada ya taarifa...sikutaka kuchukua wazo lolote toka ktk kichwa changu nikaamua wacha kwanza nipate ushauri.

angalau kuanzia hapa naweza juwa nini cha kufanya, nashukuruni sana, pili sikutegemea kabisa kama angeweza shika ujauzito, kwakweli imenishtua sana.

tatizo jingine ni kwamba, sasa mtoto akinyonya anaharisha, hiyo miezi mitatu iliyobakia mpaka afikishe sita itafika kweli? kama akiendelea na hali hii...hapa nifanye nini...
 
Miezi mitatu alitakiwa awe hata hajaanza kuona siku zake za mwezi. Lakini kwa ajili ya wivu wake na kiherehere chake ameanza kufanya uzembe mapema sana. La maana matunzo ya hali ya juu yanatakiwa kwa mama na mtoto wa miezi mitatu akifanya ujinga ama yeye ama mtoto/watoto watapotea.

Wivu gani tena huo jamani wadada, ala hata kukauka ulishakauka kweli, loh.
 
Dah kwa kweli akili ilikuwa imevurugika sana jana baada ya taarifa...sikutaka kuchukua wazo lolote toka ktk kichwa changu nikaamua wacha kwanza nipate ushauri.angalau kuanzia hapa naweza juwa nini cha kufanya, nashukuruni sana, pili sikutegemea kabisa kama angeweza shika ujauzito, kwakweli imenishtua sana.tatizo jingine ni kwamba, sasa mtoto akinyonya anaharisha, hiyo miezi mitatu iliyobakia mpaka afikishe sita itafika kweli? kama akiendelea na hali hii...hapa nifanye nini...
Mwangalieni kwa hizi siku tatu kama bado anaendelea kuharisha aache kumnyonyesha na atumie maziwa ya ng'ombe atakuwa tu na mwenye afya bora mbona watoto wanaozaliwa mamayake ana HIV wanakulia maziwa ya ng'ombe na wana afya nzuri tu.usiogope baba be strong!
 
Wana Jf,

Naomba kila mmoja ajaribu kuvaa huu uhusika, kisha nipe ushauri.. Mke ana mtoto wa miezi mitatu lakini kapata ujauzito na sasa wiki tatu, utafanya nini wewe kama baba au mama? Ushauri gani unafaa ana mambo gani inabidi kuzingatiwa katika wakati kama huu?

Kwa hiyo ni assumption tu,au?

Mimi nimefikiria hivi:
Kwa hali ya kawaida mara nyingi ujauzito unafikiriwa ikiwa mama amepitisha siku zake(MP),kwa hiyo mama huyu atakuwa amepitisha siku zake kwa wiki tatu tu! Inawezekana eeh?!

Mara nyingi dalili za ujauzito zinaanza baada ya mwezi mmoja na kuendelea.Kwa hiyo huyu mama atakuwa ameona dalili kabla ya mwezi mmoja kupita!Inaweka kuwa abnormal pregnancy,wengine wanaita molar pregnancy.

Ni weli inawezekana,ila huyu atakuwa ni miongoni mwa akina mama wachache sana chini ya jua hili wenye bahati hiyo!

Najiuliza amejuaje kama ni mjamzito.

Kwangu mimi naichukulia kama assumption,so na majibu yanatakiwa kuwa assumptions!
 
Mungu ndio anaumba, usihofu si ajabu huyo kijacho siku moja akawa ndio rais wa tz.
 
ni bahati mbaya na poleni sana,ila wote hapo mnastahili kulaumiwa hasa mwanamke kwa kuwa shughuli yake anaijua vizuri ile kitu sio ya masighara kuanzia mimba kujifungu na mpaka mtoto umesota ki ukwee,na huyu alikuwa bado hajapona vizuri kabisaaa!na je alijifungua kawaida au kwa oparesheni?
 
baada ya mwezi 1 na nusu, ligi inaendelea baada ya mapumziko ya.... kwa kuwa imetokea haina neno wajipange tu na mambo yataenda sawa. Pia hakuna mimba ya bahati mbaya labda rape! Mimba karibu zote ni kusudiwa kwa mitindo tofautitofauti
 
Mbona jambo la kawaida.......mtafutie msaidizi wa kazi za nyumbani mimba na ulezi si shughuli ndogo
 
Kwa hiyo ni assumption tu,au?

Mimi nimefikiria hivi:
Kwa hali ya kawaida mara nyingi ujauzito unafikiriwa ikiwa mama amepitisha siku zake(MP),kwa hiyo mama huyu atakuwa amepitisha siku zake kwa wiki tatu tu! Inawezekana eeh?!

Mara nyingi dalili za ujauzito zinaanza baada ya mwezi mmoja na kuendelea.Kwa hiyo huyu mama atakuwa ameona dalili kabla ya mwezi mmoja kupita!Inaweka kuwa abnormal pregnancy,wengine wanaita molar pregnancy.

Ni weli inawezekana,ila huyu atakuwa ni miongoni mwa akina mama wachache sana chini ya jua hili wenye bahati hiyo!

Najiuliza amejuaje kama ni mjamzito.

Kwangu mimi naichukulia kama assumption,so na majibu yanatakiwa kuwa assumptions!

Mrimi mimba na dalili zake zinajulikana zikiwa na week 2 na hata ukipima unaweza kujua
 
Miezi mitatu alitakiwa awe hata hajaanza kuona siku zake za mwezi. Lakini kwa ajili ya wivu wake na kiherehere chake ameanza kufanya uzembe mapema sana. La maana matunzo ya hali ya juu yanatakiwa kwa mama na mtoto wa miezi mitatu akifanya ujinga ama yeye ama mtoto/watoto watapotea.

Wivu gani tena huo jamani wadada, ala hata kukauka ulishakauka kweli, loh.

Jamani na sie wengine tunategemea kuwa wazazi siku za usoni na tunaamini Mungu ni mwema atatupa katoto. Sasa my question is mke akijifungua salama bila kufanyiwa operation ama akijifungua kwa operation inatakiwa kufanya tendo la ndoa baada ya muda gani? Na pia mbona naskia kuwa mama akijifungua inakuwa vigumu kuzitambua siku zake za hatari sasa ni njia gani rahisi kutumia.Nasema hivo kwa kuwa mimi mke wangu alishasema kuwa kwake condom ni mwiko na ni dhambi.Sasa kutokana na hilo si jamani naweza kukutwa na bwana pespi.Please mwenye uelewa wa haya mambo aje anifafanulie na mimi nipate uzoefu wa kukaa na mama aliejifungua kwa umakini na uangalifu zaidi
 
Dah kwa kweli akili ilikuwa imevurugika sana jana baada ya taarifa...sikutaka kuchukua wazo lolote toka ktk kichwa changu nikaamua wacha kwanza nipate ushauri.

angalau kuanzia hapa naweza juwa nini cha kufanya, nashukuruni sana, pili sikutegemea kabisa kama angeweza shika ujauzito, kwakweli imenishtua sana.

tatizo jingine ni kwamba, sasa mtoto akinyonya anaharisha, hiyo miezi mitatu iliyobakia mpaka afikishe sita itafika kweli? kama akiendelea na hali hii...hapa nifanye nini...

wakwangu wamepishana hivyo sikupanga but niliamua kubeba msalaba wangu, clinic nilishauriwa niendelee kum,nyonyesha mdogo lakini kama ataonyesha kuharisha nimwachishe. bahati nzuri haikumuathiri, nilihakikisha yule mkubwa anapata lishe kamili na kwakweli both wamekua vizuri they are my big girls now 9 na 8yrs baadhi ya watu wanafkr ni twins! zingatia ushauri wanao watakua vizuri na ww kama baba usinonyeshe kupanic maana mama at the moment amechanganyikiwa zaidi yako!
 
Mrimi mimba na dalili zake zinajulikana zikiwa na week 2 na hata ukipima unaweza kujua

Mkuu unatumia kipimo na dalili gani kupata definitive diagnosis ya mimba ya wiki mbili?Hebu tupeane somo kwa faida ya wengi.
 
Mkuu unatumia kipimo na dalili gani kupata definitive diagnosis ya mimba ya wiki mbili?Hebu tupeane somo kwa faida ya wengi.
Kwanza dalili nyingi za mimba zinafanana na menstrual period ikivuka siku ambazo ulitarajia kupata hedhi lazima mtu atashtuka na kipimo cha pili ni pregnancy test kifaa kipo kinauzwa pharmacy vilevile process ya implantation inaanza siku ya kumi toka yai likutane na mbegu kunakuwa na maumivu ya tumbo na wakati mwingine damu hutoka kama matone kwa mwenye ufahamu anatambua mapema.
 
Na vipi mama akijifungua anatarajia tena kuanza mp baada ya muda gani?
 
Na vipi mama akijifungua anatarajia tena kuanza mp baada ya muda gani?

Mama akijifungua inachukua siku kazaa,miezi hata mwaka mlang6 wa uke unakuwa mkavu,mama anapoanza kusikia mlango wa uke umeanza kuloa hapo atajua siku za hatari zimefika ndo mana mama anatakiwa kuwa makini wk 3 baada ya kujifungua anatakiwa kuandaa kalenda ya siku zake kwa wale wanaonyonyesha
Full time inawachukua hata mwaka ndo anaona siku zake tofauti na wengine lakini pia miili inatofautiana hii njia ya kutambua ukavu na kuloa anaimudu zaidi anayetumia njia ya asili ya uzazi wa mpango.
 
inabidi awaone wataalam mapema wampe ushauri na muda wa kumnyonyesha mtoto pia utunzaji wa mimba yake huku akijitahidi kuhudhulia Clinic,ni kazi ya ziada hiyo ,lakini mungu atawatunza na kuwapa afya njema ,pia ajitahidi kupata mlo wa kutosha kwa mtoto anayenyonya kwa ajili ya maziwa,yeye mwenyewe na mtoto tumboni,
 
Back
Top Bottom