Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Karagwe

Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Karagwe

Nahisi kama nchini inaweza kubadilika kwa muda mfupi...

Bado maneno ya Padre Kitima na Mufti Mkuu au angekuwepo yule Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, simkumbuki jina, mweupe hivi, nadhani angetoa neno. I wish hizi taasisi za kidini zitoe maneno ya busara mapema.
Wanajiandaa lazima watakuja na neno
 
View attachment 3211239
1. Tundu Lissu siyo Donald Trump. Wanafanana ukali wa maneno lakini hawafanani ujinga wa kisiasa. Wote walipigwa risasi, zikawaongezea kura zao.

2. Lissu ni hukumu isiyo na rufaa kwa watawala wanaotumia risasi badala ya hoja. Rudisheni risasi mfukoni, nendeni shule mjifunze hoja. Wamarekani walitumia risasi, sasa wanaongozwa na “kichaa mstaarabu”.

3. Tundu Lissu siyo Trump. Kwa Trump mihimili inajitegemea na ina nguvu katika kufanya kazi. Hapa kwetu, mihimili inategemea kusemwa na kusimangwa ndipo ifanye kazi.

4. Mmemsahau Spika Makinda? “Mwanangu Lissu, hebu tusaidie tunaondokaje hapa”. Natamani Tulia atulie mbele ya Makinda apate twisheni ya kufanya kazi na Lissu.

5. Lissu na Freeman wameelewana, lakini wapambe wao wamenuniana. Tatizo lilikuwa moja; Lissu aliwamudu wapambe wake; Freeman wapambe walimmudu.

6. Yaliyotokea ni somo kwetu: Wapambe wa Lissu waliweza kumuambia ni wakati gani sahihi wa kuingia uwanjani, lakini wapambe wa Freeman hawakuweza kumwambia ni wakati gani sahihi wa kutoka uwanjani.

7. Kama kuna makosa yoyote Freeman aliyafanya kwa muda wa miaka 21 aliyoongoza Chadema, basi makosa yake yote ameyafuta kwa kubonyeza kitufe kimoja tu: kuendesha uchaguzi kwa uwazi na kukubali matokeo.

8. Lissu kachukua 'mkopo mkubwa’ na wenye riba kubwa sana, lakini kazungukwa na vibaka. Je atamudu kurejesha mkopo huo?

9. Neno langu kwa Mbowe: Umejenga heshima kubwa, umeondoka kwa heshima kubwa. Ilinde heshima hiyo. Ukistaafu, staafu.

10. Neno langu kwa Lissu: Mahaba ya kutongozea ni tofauti na mahaba ya kuishi na mke katika ndoa. Jitathmini.!
"Mahaba ya kutongozea ni tofauti na mahaba ya kuishi na mke katika ndoa" Kwako Lisu zingatia hili!
 
Machache ya kujifunza:

1. Uchaguzi huu umefuatiliwa kwa miezi miwili mfululizo. Hata CCM walipokua kwenye kitchen party yao Dom walikua wanachungulia simu kujua kinachoendela Chadema. Tuilinde imani kubwa Watanzania waliyoonesha kwetu.

2. Mchuano wa Freeman na Lissu umeifanya Chadema kupata promo kubwa na kujibrand bila wasanii wala celebrities.

3. Chadema imefundisha demokrasia kwa vitendo. Fomu ya Mwenyekiti haikutolewa moja kama hati ya kifo. Yeyote aliyejipima na kuona anaweza kuongoza, alipewa fomu, akiwemo rafiki yangu Odero aliyeambulia kura moja.

4. Uchaguzi umeendeshwa kwa uwazi na kura kuhesabiwa hadharani. Freeman amefundisha somo la demokrasia kwa vitendo. Kule Chama chakavu wasingekubali Mwenyekiti wao aondoke kwa kura 31 tu, wangepindua meza. Lakini Freeman ni muumini wa haki na ameheshimu demokrasia. Respect to him 🙏🏽.

5. Chadema tumeset golden standards kwenye viwango vya Free, Fair, Credible and Transparent election. Hakuna Chama chochote kimewahi kufikia kiwango hiki cha uwazi. Kwa sasa vyama vingine vikifanya chaguzi vitapimwa kwa viwango vyetu. Sisi ndio SI unit.

6. Mbunge mmoja amedai eti wajomba zake Wachagga wamepigwa kwenye huu uchaguzi. Hivi tunataja makabila kwani tunatambika? Acheni ufala. Kwenye uchaguzi wa kisiasa mtu apimwe kwa hoja zake sio kabila lake. Kama wachagga wamepigwa, je "Strategist" wa Lissu, Godbless Lema ni Mkikuyu? We "Mpwa" tunakuonya acha ushamba kutaja makabila kwenye mambo serious. Tulikua hatufanyi tambiko, bali uchaguzi. Au tukupe laana ya ujombani ukose jimbo?

7. Kwenye press yangu ya tar.12 nilisema watu waweke akiba ya maneno. Usinene ukamala. Nilisema baada ya uchaguzi kuna watu watatamani kuyameza maneno yao lakini haitawezekana.

8. Ni bahati mbaya wapambe waliongea mengi kipindi cha kampeni na kuifanya CCM ichukue notes ambazo wanaweza kuzitumia baadae dhidi yetu.

9. Kwenye press yangu nilishauri Mwenyekiti atakayechaguliwa aunde Post Election Mediation committee itakayotibu majeraha yaliyojitokeza wakati wa kampeni.

10. Watanzania wanatupenda, wanatuamini. Tukilinde chama chetu kwa wivu mkubwa. Kikifa itachukua miaka mingi kupata chama kingine kitakachoaminika kama hiki. #StrongerTogether 💪🏽
Credit: Malisa G.J
1737645942687.jpg
 
View attachment 3211239
1. Tundu Lissu siyo Donald Trump. Wanafanana ukali wa maneno lakini hawafanani ujinga wa kisiasa. Wote walipigwa risasi, zikawaongezea kura zao.

2. Lissu ni hukumu isiyo na rufaa kwa watawala wanaotumia risasi badala ya hoja. Rudisheni risasi mfukoni, nendeni shule mjifunze hoja. Wamarekani walitumia risasi, sasa wanaongozwa na “kichaa mstaarabu”.

3. Tundu Lissu siyo Trump. Kwa Trump mihimili inajitegemea na ina nguvu katika kufanya kazi. Hapa kwetu, mihimili inategemea kusemwa na kusimangwa ndipo ifanye kazi.

4. Mmemsahau Spika Makinda? “Mwanangu Lissu, hebu tusaidie tunaondokaje hapa”. Natamani Tulia atulie mbele ya Makinda apate twisheni ya kufanya kazi na Lissu.

5. Lissu na Freeman wameelewana, lakini wapambe wao wamenuniana. Tatizo lilikuwa moja; Lissu aliwamudu wapambe wake; Freeman wapambe walimmudu.

6. Yaliyotokea ni somo kwetu: Wapambe wa Lissu waliweza kumuambia ni wakati gani sahihi wa kuingia uwanjani, lakini wapambe wa Freeman hawakuweza kumwambia ni wakati gani sahihi wa kutoka uwanjani.

7. Kama kuna makosa yoyote Freeman aliyafanya kwa muda wa miaka 21 aliyoongoza Chadema, basi makosa yake yote ameyafuta kwa kubonyeza kitufe kimoja tu: kuendesha uchaguzi kwa uwazi na kukubali matokeo.

8. Lissu kachukua 'mkopo mkubwa’ na wenye riba kubwa sana, lakini kazungukwa na vibaka. Je atamudu kurejesha mkopo huo?

9. Neno langu kwa Mbowe: Umejenga heshima kubwa, umeondoka kwa heshima kubwa. Ilinde heshima hiyo. Ukistaafu, staafu.

10. Neno langu kwa Lissu: Mahaba ya kutongozea ni tofauti na mahaba ya kuishi na mke katika ndoa. Jitathmini.!
Neno langu kwa Lissu: Mahaba ya kutongozea ni tofauti na mahaba ya kuishi na mke katika ndoa. Jitathmini.!
 
Hoja namba nane nilishaisema humu jukwaani lakini Wafuasi wa Lissu walishindwa kunielewa na wakapinga kwa kutukana katusi. Nilisema kwa kuandika andiko humu jukwaani kuwa Lissu amezungukwa na watu wa Hovyo sana.

Sasa ndio mjue kuwa mimi naishi mbele ya wakati. Ipo siku mtanielewa vizuri na kuanza kububujikwa na machozi ya majuto kwa kutofanyia kazi ushauri wangu.
 
Back
Top Bottom