Chee4
Member
- May 17, 2021
- 35
- 125
Nilipokuwa Katibu Mwenezi wa CCM tuliwaambia watanzania wawe makini na CHADEMA, tuliwaambia wawe makini na chama kinachoendeshwa kisanii kwa hoja mpechempeche na propaganda nyepesi, muda ni mwalimu mzuri, leo ukweli unajianika na CHADEMA wanaumbuka. Chama kimepoteza mvuto, Press zisizo na tija kila kukicha, tunakosea sana kukiita Chama kikuu cha Upinzani.
Nilisikiliza press ya rafiki yangu Mnyika kufuatia mahojiano ya Mama yetu mpendwa Samia na BBC, hadi mwisho wa press yake sikuelewa alilenga kusema nini, analalamika Rais kaingilia Uhuru wa Mahakama, while Rais alisema 'la mahakamani sio lake', halafu hapohapo anasema wanamuomba Rais afute kesi ya Mbowe, kama sio kuchanganyikiwa ni nini? Wasimshinikize Rais wetu kuingilia Uhuru wa Mahakama ili wapate la kusema. Tumewashtukia.
Leo Mwenyekiti nae katoa Boko la mwaka kutokea Ukonga, jambo la ajabu kuhusu salamu za Mbowe ni kwamba CHADEMA wana msemaji na viongozi wengine, lakini taarifa kwa Wanachama inatolewa na James Mbowe, Mwanafamilia asiye na cheo pale ufipa, Ndio maana tuliimba sana kuwa CHADEMA ni Saccos ya Bwana yule. Chama hakina taratibu, kinaendeshwa kama magenge ya mihadarati (Cartels) ya huko Mexico. Si bora kifutwe tu.
Halafu hawa watu walisema Mbowe kakamatwa kwasababu ya Katiba Mpya, kumbe Mbowe mwenyewe anajua walinzi wake walikamatwa mwaka mmoja uliopita, amekiri kwa maneno yake, Swali la kujiuliza ni moja tu, kama kweli Mbowe hakuhusika na Ugaidi kwanini CHADEMA hawajawahi kuzungumzia issue ya walinzi wa Mbowe kukamatwa hata siku moja? Kama kweli Mbowe hakuhusika, hao walinzi wake wangetetewa kama Dreva wa Lisu na Mdude kwanzia walipokamatwa.
Akili za kuambiwa changanya na zako, IGP Sirro aliwashauri wanachama wa CHADEMA waende wakamuulize Mwenyekiti wao kuhusu kesi inayomkabili, lakini wakakaidi halafu wakalipa watu wakaandamane Mahakamani, wakadhibitiwa, sasa leo Mbowe kupitia salamu zake kakiri kutambua kesi, kakiri anakabiliwa na kesi ya Ugaidi, nguvu za kusema Mbowe sio gaidi zinatoka wapi? Wamezoea kupinga kila kitu sasa wanapinga hadi msimamo wa Mwenyekiti wao.
All in All, Bwana yuke kachemka kutuma salamu ambazo zinakinzana na madai ya wanachama wa chama chake na chembechembe za kadharau uongozi wa Chama chake kwa kumpa taarifa Mwanae (Mtoto wa ndygu yake) wakati wakina John Mrema hawana cha kufanya, wanazurura tu kwenye bar za Mikocheni.