Anaandika Mwabukusi (advocate)

Anaandika Mwabukusi (advocate)

Nafikiri Samia anatoa onyo hata kwa watumishi wenye kinga, wasipokuwa machawa, wakatoa maoni ambayo hayapendi wanaweza kuishia jela.

Kosa la kumbambikizia, kosa lina dhamana, Mzee wa watu miaka 75 atakimbilia wapi? Wamtesa na kumkomoa tu. Hii serikali wamekosa utu kabisa na kulewa na madaraka.
 
Hii nchi ni ya Ajabu sana, wanamfanyiaje huyu mzee aliyekuwa Balozi wetu huko Sweden? Yaani maana yake ni kwamba Raisi mstaafu (balozi muwakilishi) hana kinga ya mashtaka? Taaabu tupu.

NB: Balozi ni muwakilishi wa nchi kama alivyo Raisi ndio maana wana kinga ya mashtaka wakiwa na hadhi ya ubalozi.. sasa sijui, kama hiyo kinga huwa inavulika mtu akiacha kuwa balozi. kama kinga inavulika maana yake hata Raisi akistaafu, kinga yake pia haipo. Hawa prosecutors wanatengeneza precedent ya hatari sana kwa maraisi na mabalozi siku za mbeleni huko.
Hatutaki hizo kinga ndiyo zinatusumbua, hoja ni Mzee anastahili dhamana au hapana. Upelelezi haujakamilika kwa nini apelekwe mahakamani.
 
Kuna wakati ninajihoji na kujiuliza kuhusu mfumo wetu wa Haki Jinai najisikia Aibu sana kuwa Mwanasheria .

Ukijiuliza logic ya uwepo wa sheria inayokataza bayana kupelekwa kwa mashtaka Mahakamani kabla upelelezi haujakamilika na kwamba anaweza kuwepo mtu ambaye kasoma sheria ila anaamua kuinajisi na kuigeuza Mahakama kama Kokoro la kubeba kila aina ya takataka ..

Tunajidhalilisha na kudhalilisha mfumo wetu wa Haki jinai...Iam very ashamed personallView attachment 3213473y.
Hakuna mahalama Tanzania,ila ipo siku tutapata mahalama za haki MUNGU ATATENDA TU wala tusihofu.
 
Hatutaki hizo kinga ndiyo zinatusumbua, hoja ni Mzee anastahili dhamana au hapana. Upelelezi haujakamilika kwa nini apelekwe mahakamani.
tuko pamoja mkuu Wing, hiyo ndiyo point yangu pia, mtu kafikia hadhi ya kuiwakilisha nchi na leo ananyea debe? Ni ajabu sana kwa viongozi wetu kumtendea huyu former ambassador kwa kiasi hiki-- too low kwa kweli.
 
Nafikiri Samia anatoa onyo hata kwa watumishi wenye kinga, wasipokuwa machawa, wakatoa maoni ambayo hayapendi wanaweza kuishia jela.

Kosa la kumbambikizia, kosa lina dhamana, Mzee wa watu miaka 75 atakimbilia wapi? Wamtesa na kumkomoa tu. Hii serikali wamekosa utu kabisa na kulewa na madaraka.
Ndio maana kuna post ile ya Azam nikashauri kwamba kwa fukuto na vuguvugu linaloendelea nchini basi serikali ingeangalia haya maswala kwa jicho la tatu kabla ya kila kitu kuonekana udini hata kama kweli wahusika wana kosa.

Inawezekana kweli mzee kwa matamshi au maandiko yake katishia usalama wetu, lakini kwa umri wake na heshima ambayo alikua nayo basi ilikua ni busara kuitwa na viongozi wakubwa wa serikali kupitia viongozi wa dini akakanywa na kuonywa yakaisha. Ila sio kumkomoa.

Huwezi jua nyuma yake wapo wangapi ambao wamekaa mbali tu wanaangalia mchezo. Tukumbuke Slaa ana influence toka kipindi akiwa anagombea urais akiwa Chadema so more possible wapo wenye ushawishi wanaoumia kwa hili linalotokea.

Serikali yetu tukufu imuachie huru huyu mzee!!!
 
Binafsi sio mwanasheria ila hili la kumkamata mtu na kumuweka mahabusu halafu unakuja kusema ushahidi haujakamiliki naliona ni jambo la ajabu sana, kipi kinapaswa kuanza kati ya kukamata au kuchunguza na kukusanya ushahidi wa kutosha halafu ndio ukamate.
kwani hawa jamaa wanataka ushahidi gani tena mwanzo walidai wamemkata Dr. slaa kwa kuchapisha taarifa za uongo huko kwenye mtandao wa X na hizo post wote tuliziona si ndio ushahidi wenyewe huo wa kudhibitisha hayo madai yao...mm nionavyo hapa wanamkomoa na kumtesa tu..ni bora mfumo mzima wa upelezi wa mashtaka nchini ufumuliwe wote na hicho kichaka cha "upelelezi haujakamilika na kichaka kingine cha anyimwe dhamana sababu ya usalama wake" vivyekwe vyote kwani vinatumiwa na wahuni wenye vyeo na madaraka na wenye pesa kuwanyanyasa na kuwakomoa wasiowapenda au wanao wakosoa..na itapendeza zaidi wanasiasa wote RC,DC,DED,RAS,CCM,Mawaziri waondolewe kwenye mfumo wa kutoa amri nchini kwenye haki jinai kwani hawa amri zao nyingi ni za dhuluma na uonevu za ashughulikiwe fulani.. ila amri zibaki kwa rais,VP na PM..na iwe marufuku ma RPC na walio kwenye mfumo wa kutoa order kupokea amri za wanasiasa wenye visasi na kukomoa wenzao sio wanaagiza tu kamata fulani kisha wanawapa kazi idara ya mashtaka na mahakama kusajili kesi zisizo na kichwa huo ushahidi wataupata wapi ndo kama hivi kuaibisha idara zetu za haki nchini zinaonekana za ovyo kisa wapuuzi wachache wanaojiona miungu watu.!
 
Nilimsikia Balozi Dr. Slaa anasema hajataarifiwa kimaandishi na serikali haifanyi kazi kwa mdomo bila taraifa ya maandishi. Pia maana yake ni kwamba Kinga za Maraisi wastaafu hazina maana yeyote, maana ni kutamka tu au kupitisha sheria huko Bungeni kwamba kinga imefutwa na wanapelekwa rumande... inabidi wawe makini sana kwa wanacho kifanya. Kina gharama siku za mbeleni huko kwa mtindo huu... Huyu mzee kachoka , hata tembea yake lakini bado wanaye... wamuache apumzike kwa kweli
Immunity isn’t unlimited. Hamkumbuki kesi ya Professor Mahalu (former Tanzanian ambassador to Italy)? Hata hivyo, Dr. Slaa anaonewa tu!
 
Kuna haja yakuhakikisha Kinga za marais na baadhi ya viongozi wa serikali na taasisi za usalama zinaondolewa mara moja.

Kuwaondolea Kinga kutawafanya wawe makini na mfumo wa Sheria na matendo yao wawapo gerezani.
Nguvu ya Kinga inafanya baadhi ya viongozi kutumia mamlaka yao vibaya wakiamini hakuna chakuwafanya.
ni kweli lakini wahuni wetu badala yake wameongeza VP,PM,Spika na Jaji mkuu eti nao hawashtakiwi..na hiyo kinga ya rais ndio wahuni wengi wenye vyeo na madaraka ndio wanajifichia..ikifutwa hio kinga kwa rais awe anahojiwa na kushtakiwa naamini rais hatolea ujinga na uzembe wa walio chini yake waje kumuharibia yeye au hata kufungwa kwa uzembe wao hatovumilia upuuzi wa mtu anaetaka kumuingiza shimoni
 
Hii nchi ni ya Ajabu sana, wanamfanyiaje huyu mzee aliyekuwa Balozi wetu huko Sweden? Yaani maana yake ni kwamba Raisi mstaafu (balozi muwakilishi) hana kinga ya mashtaka? Taaabu tupu.

NB: Balozi ni muwakilishi wa nchi kama alivyo Raisi ndio maana wana kinga ya mashtaka wakiwa na hadhi ya ubalozi.. sasa sijui, kama hiyo kinga huwa inavulika mtu akiacha kuwa balozi. kama kinga inavulika maana yake hata Raisi akistaafu, kinga yake pia haipo. Hawa prosecutors wanatengeneza precedent ya hatari sana kwa maraisi na mabalozi siku za mbeleni huko.
Hizo Kinga zao wanazotengeneza Kila bunge kumbe ni buree kabisa

Aibu kwao
 
Ndio maana kuna post ile ya Azam nikashauri kwamba kwa fukuto na vuguvugu linaloendelea nchini basi serikali ingeangalia haya maswala kwa jicho la tatu kabla ya kila kitu kuonekana udini hata kama kweli wahusika wana kosa.

Inawezekana kweli mzee kwa matamshi au maandiko yake katishia usalama wetu, lakini kwa umri wake na heshima ambayo alikua nayo basi ilikua ni busara kuitwa na viongozi wakubwa wa serikali kupitia viongozi wa dini akakanywa na kuonywa yakaisha. Ila sio kumkomoa.

Huwezi jua nyuma yake wapo wangapi ambao wamekaa mbali tu wanaangalia mchezo. Tukumbuke Slaa ana influence toka kipindi akiwa anagombea urais akiwa Chadema so more possible wapo wenye ushawishi wanaoumia kwa hili linalotokea.

Serikali yetu tukufu imuachie huru huyu mzee!!!
Kosa la kusema uongo halina Dhamana? Uongo aliousema ni upi kwamba amepewa taarifa na vyombo nyeti kwamba Samia na Mbowe wanawasiliana, Samia amempa Mbowe pesa za kutoa Rushwa?

Dr Slaa aliwahi kuwatuhumu wakubwa wote mwembeyanga kwamba ni mafisafi papa Mkapa,Kikwete, Chenge, Lowassa. Rostam, Mkono nk na akasema amepewa taarifa na usalama hakufungwa.

Lyatonga Mrema aliwahi kutoa tuhuma kama hizi za ufisadi, taarifa zake alisema amepewa kutoka jikoni kuhusu Rais Mwinyi.

Msigwa aliwahi kusema hivyo siku za nyuma kwenye uchaguzi wa Nyasa, Lissu amesema hivyo mara nyingi na wengine wengi. Kwanini wanamkamata huyu tu na kumnyima dhamana?

Wanaogopa influence yake kuelekea uchaguzi? Wanataka wamdhoofishe afya yake, labda afariki?
 
Kufariki Hapana. Tumuombee Heri
 
Back
Top Bottom