Anachofanya Ibrahim Traore ni kizuri ila kinakosa misingi ya utawala yaani ni one man show

Anachofanya Ibrahim Traore ni kizuri ila kinakosa misingi ya utawala yaani ni one man show

Wewe unaamini ktk Demokrasia kumbuka Demokrasia ilikuja kulingana na utawala wa kifalme kuwa wa wachache

Sasa hivi Demokrasia imeanza kupitwa na wakati inatoa mianya ya wizi na rushwa plus ukoloni mamboleo mfano unakuwa na Tume, mahakama na serikali jina

Huo ni mfumo mpya unaouanzisha kama alivyo anzisha Demokrasia Abraham Lincoln

Kavunja Tume ya uchaguzi juzi tu
Hiyo nchi inaendeshwa tofauti na nchi zingine

Zamani walikuwa na hiyo mifumo wakawa watumwa kwa mfaransa ndicho kilichofanya Traore awe Traore unayemsema wewe kwenye huu uzi
Abraham Lincoln hakuanzisha demokrasia.
 
Abraham Lincoln hakuanzisha demokrasia.
Concept za demokrasia zilianzishwa na kina aristoste kabla hata Yesu hajazaliwa ni jambo ambalo watu wengi hawaelewi wanadhani demokrasia imeanza juzi

Utawala wa dola ya kirumi ulikuwa na bunge la waliochaguliwa na wananchi
 
Abraham Lincoln hakuanzisha demokrasia.
Ukielewa dhana ya Demokrasia kwa muujibu wa Abraham Lincolin utanielewa

Hoja yako ni kama ya Abraham Lincoln miaka ya 1800s

Ila sio nchi zote wanatumia huo mfumo


Hapa Africa tulicopy na kupaste

Huo mfumo hauendani na uhalisia
Ndio maana matatizo ya nchi nyingi za Afrika kiuongozi yanafanana sababu mfumo ni ule ule

Traore yupo kivyake anaamini ktk mfumo wake binafsi ambao wengi bado hawajauelewa

Hiyo ni evolution
 
Kila mtu akiongea hakuna la maana litafanyika hata hao mabeberu walianza na one man show walivojipata ndo wakaja na demokrasia
 
Ndo yalikua mawazo ya Magufuri.
Ona sasa kila kitu kimerudi Kama alivo acha kikwete
 
Mkuu Acha skanka hainipendi nyuzi zako nyingi ni nzuri,ila huo Urais unaoutamani sidhani
 
Exactly hio ndo point ýangu
Magufuli alikuwa na uwezo wa kuifanya katiba ya Tanzania ikawa bora sana na hata asingekuwepo matunda yake yangeonekana
Polepole kasema alikua ana mpango huo 2024 wakat anamaliza mda wake maan katiba huletwa kipindi cha kumaliza mda kama kikwete
 
Polepole kasema alikua ana mpango huo 2024 wakat anamaliza mda wake maan katiba huletwa kipindi cha kumaliza mda kama kikwete
Yaani mabadiliko ya katiba unayeleta mwaka 2024 si tunarudia makosa yale yale yaliyofanyika kwenye katiba ya warioba sababu ni wazi mchakato wa katiba unahitaji mda mrefu sana
 
Ni ukweli kwamba anachofanya Ibrahim traore ni jambo zuri in term of mabadiliko ni jambo ambalo waburkinafaso wanafurahia ma waafrika wote wanafurahia

Hawa viongozi wengi wa afrika ambao ni charismatic wanachangamoto moja inayofanana wana-upeo na hesabu ndogo sana naweza sema hivyo wako ambao watakuwa supprise sana na hii statement bali ndo ukweli

Hawatengenezi taasisi imara mfano
  • Mahakama huru
  • Bunge huru
  • Mamlaka ya kupambana na rushwa huru
  • Ofisi ya mwendesha mashtaka (DPP) iliyokuwa huru jambo la kufahamu ni kwamba sisi kama binadamu tunapita ila ukitengeneza misingi imara inaweza dumu
  • Tume huru ya uchaguzi ambayo traore hataki hata kukiongelea

Hata sankara aliongoza nchi as if ataishi milele akasahau sisi ni wapitaji hapa duniani

Kilichotokea Libya kinaweza kuwa somo kwetu waafrika lakini sisi ni ngumu sana kujifunza gaddafi aliitengeneza Libya sana ila ilikuwa ni one man show yaani hakutengeneza taasisi imara, kama Libya ingekuwa na taasisi imara basi hata bila uwepo wa gaddafi nchi ingeendelea vizuri tu

Mimi kiongozi ambaye haamini kwenye strong system basi nakua nimeshamshusha sana kwa sababu hicho anachokifanya ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga bila msingi siku ikija mvua kubwa na upepo basi myumba inabomoka sababu mfumo wowote lazima uje uwe tested kama ni imara au la

Ibrahim traore anayoyafanya yaendane na mifumo imara ya kuitawala nchi na sio one man show

MIMI NIKIWA RAIS WA TANZANIA NTATENGENEZA MISINGI IMARA YA UTAWALA HATA KAMA SITAKUWEPO BASI MAMBO YANAENDELEA KAMA KAWAIDA NA VIZURI ZAIDI

Mnacho maanisha ni democracy, najua mm democracy ni failure katika kuleta maendeleo but uongozi kama wa china mnaona kabisa wapo katika future na hiyo marekani wanaoiongoza ni elite wala sio trump, gadafi alifanya maisha ya walibia kua mazuri now democracy inawangamiza
 
Back
Top Bottom