Anachofanya Ibrahim Traore ni kizuri ila kinakosa misingi ya utawala yaani ni one man show

Anachofanya Ibrahim Traore ni kizuri ila kinakosa misingi ya utawala yaani ni one man show

Mnacho maanisha ni democracy, najua mm democracy ni failure katika kuleta maendeleo but uongozi kama wa china mnaona kabisa wapo katika future na hiyo marekani wanaoiongoza ni elite wala sio trump, gadafi alifanya maisha ya walibia kua mazuri now democracy inawangamiza
Democracy inafanya nchi inakuwa ya wote na sio kikundi cha watu wachache

Alafu Tanzania na nchi nyingi za Afrika bado hatujafikia kwa asilima mia moja misingi ya demokrasia
 
Acha ngonjera mkuu hakuna hicho kitu nchi zote za magharibi ziliadopt demokrasia baada ya kujipata hakuna hata moja ilikua Maskini kabla ya demokrasia kama ipo taja hapa twende na data acha generalization
Nchi za ulaya zimeendelea baada ya vya pili vya dunia yaani zilianza upya sababu vita vya pili vya dunia viliwafanya waanze upya na hawakuwa na one man show
 
Kwenye mambo ya kiafrika usilete uzungu ,jamii ngapi hazijawahi kuwa na bunge ...Traore yuko sahihi ,akianza kutumia hao wahuni ni walewale wenye elimu ya Mzungu ,watamletea tabu.

Waulize wenzio kisa cha Nyerere na Justin Rweyamuma kugombana , Rweyamuma kasoma na kukariri elimu ya mzungu so alikataa ujamaa na alitaka ubepari wa wazungu...Traore kwa sasa lazima atulie ,hao akianza kuwaamini wanaenda kumuangusha ...Itakuwa anajiidanganya kwa kutumia mifumo ile ya kitapeli.
 
Kwenye mambo ya kiafrika usilete uzungu ,jamii ngapi hazijawahi kuwa na bunge ...Traore yuko sahihi ,akianza kutumia hao wahuni ni walewale wenye elimu ya Mzungu ,watamletea tabu.

Waulize wenzio kisa cha Nyerere na Justin Rweyamuma kugombana , Rweyamuma kasoma na kukariri elimu ya mzungu so alikataa ujamaa na alitaka ubepari wa wazungu...Traore kwa sasa lazima atulie ,hao akianza kuwaamini wanaenda kumuangusha ...Itakuwa anajiidanganya kwa kutumia mifumo ile ya kitapeli.
Bado uko mbali sana kifikra mfano akifariki leo traore nchi inarudi kue kule
 
Nyerere alifanya au niseme ameyafanya hayo. Kaomba uhuru kwa mzungu/malkia,akaunda taifa lenye taasisi huru na kuweka sheria ambazo kwa nyakati zile zilikuwa sahihi kabisa na muda wa kutoa kijiti ulipofika akawaachia wenzake bila kuleta ligi,ila nini kimefuata?

Waafrika sisi tuna kauzembe fulani kuanzia ngazi ya familia. Tutawalaumu sana hawa viongozi tunaowapa uongozi na mamlaka ila tukubali kuwa sisi ni wazembe katika kujisimamia tunataka atokee mtu aifanye kazi ya usimamizi na ndio maana watu kama akina Gaddafi wakiingia hawataki kutoka maana wanajiuliza atamuachia nani.

Hapa saa hii tuna tatizo la viongozi kuchezea sheria na mamlaka,tunabakia na kazi ya kuwalaani kwa maneno huku vitendo vyetu vikikinzana na maneno.

Hatusomi katiba na kuielewa vema ili tuweze jua nini cha kuongeza na nini cha kutoa tunabakia kulalamika.

Hivi unadhani ni kazi rahisi kwa mtu m'moja kusimamia taasisi zote?

Wewe kama mzalendo wa taifa hili kwa nafasi yako huwa unatumia mamlaka yako ya kizalendo kuwajibisha wale wanaochezea taasisi?

Tukitaka huo ubora wa kiutendaji inaanza na sisi raia kuwa wakali na kusimama pamoja. Mfano mnasimamishwa kwenye foleni ili hawa wavaa makoti na wachezea kodi wawaishwe nyumbani kukata gogo ninyi kama raia how do you stand up na kusema hii si sawa?

Mbunge analipwa million 12 kwa mwezi mwalimu wako aliyekufundisha wewe kaka yako,baba yako na pengine anamfundisha mwanao kwasasa,umeshawai kumtetea alipwe walau milioni mbili kwa mwezi au awe na stahiki nzuri ili maisha yake yawe mepesi?

Je,hapa saa hii kunatabia ya viongozi kuzima internet pale kunapokuwa na mijadala muhimu ya changamoto za kitaifa,je tumewawajibisha TCRA watuambie nani anatoa maagizo ya kuzima internet?

Je,ikatokea umeenda bank kuna Teller anafanya mapozi na ninyi raia mpo tu hapo mnajisonya na hamuwashi moto ili afukuzwe kazi tuwekewe teller makini,unategemea tutafuta viburi vya wafanyakazi wasiojua wajibu wao?

Mimi nadhani inaanza na sisi kwanza kuwa wawajibishaji na ndipo watu kama akina Traole hawatoona haja ya kufosi kuendesha inchi kwa maono yao binafsi na watu wanaosikilizana nao wao.

Hapa saa hiu tunachangamoto ya serikali ya sasa kushikwa na kuhodhiwa na watu wachache na tunawajua why hatuwahoji kama raia na kuwawajibisha kisheria na kufuta stahiki zao?

Mfano labda tunaona kikwete anazingua,then kama raia tunaweza sema afutiwe stahiki zote za kiongozi mstaafu mwenye heshima na tukomalie awajibishwe kisheria kwa mambo ya hovyo?

Ila tukiamini kuwa sisi ni wa kusaidiwa,kufanyiwa kutetewa,kupiganiwa,na kusikilizwa tu bila kujipa wajibu wa kizalendo kwa mujibu wa sheria then tunatengeneza tatizo kubwa sana sasa na hapo baadae.

Tubadilike sasa
 
Ni ukweli kwamba anachofanya Ibrahim traore ni jambo zuri in term of mabadiliko ni jambo ambalo waburkinafaso wanafurahia ma waafrika wote wanafurahia

Hawa viongozi wengi wa afrika ambao ni charismatic wanachangamoto moja inayofanana wana-upeo na hesabu ndogo sana naweza sema hivyo wako ambao watakuwa supprise sana na hii statement bali ndo ukweli

Hawatengenezi taasisi imara mfano
  • Mahakama huru
  • Bunge huru
  • Mamlaka ya kupambana na rushwa huru
  • Ofisi ya mwendesha mashtaka (DPP) iliyokuwa huru jambo la kufahamu ni kwamba sisi kama binadamu tunapita ila ukitengeneza misingi imara inaweza dumu
  • Tume huru ya uchaguzi ambayo traore hataki hata kukiongelea

Hata sankara aliongoza nchi as if ataishi milele akasahau sisi ni wapitaji hapa duniani

Kilichotokea Libya kinaweza kuwa somo kwetu waafrika lakini sisi ni ngumu sana kujifunza gaddafi aliitengeneza Libya sana ila ilikuwa ni one man show yaani hakutengeneza taasisi imara, kama Libya ingekuwa na taasisi imara basi hata bila uwepo wa gaddafi nchi ingeendelea vizuri tu

Mimi kiongozi ambaye haamini kwenye strong system basi nakua nimeshamshusha sana kwa sababu hicho anachokifanya ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga bila msingi siku ikija mvua kubwa na upepo basi myumba inabomoka sababu mfumo wowote lazima uje uwe tested kama ni imara au la

Ibrahim traore anayoyafanya yaendane na mifumo imara ya kuitawala nchi na sio one man show

MIMI NIKIWA RAIS WA TANZANIA NTATENGENEZA MISINGI IMARA YA UTAWALA HATA KAMA SITAKUWEPO BASI MAMBO YANAENDELEA KAMA KAWAIDA NA VIZURI ZAIDI

Amachofanya ni kuwakumbusha waafrika wasipojitambua na kujituma ni kuwa siku moja watarudi utumwani kwa mara ya pili,hivyo anawafundisha watu wake kila kitu kinawezekana kwa kuamua na kumaanisha.Na pia anajaribu kuikumbusha africa umuhimu wa siasa safi na utawala bora na washeria.Yupo babu mmoja wa miaka sabini hivi sasa karibu 80,ila anaichukia Afrika kutokana na tabia za tawala na serikali nyingi za Africa.Tujisahihishe,tujirekebishe.
 
Bado uko mbali sana kifikra mfano akifariki leo traore nchi inarudi kue kule
Traore ana mifumo yako ,ila hiyo ulivyotaja imejaa wezi mpaka achague wengine ...Jeshi liko kamili ,hayo mengine hayana maana kama una akili lakini...

Traore yuko pale kwa vile kuna watu wanamuunga mkono ,wanamsaidia katika utendaji wake .
 
Mkuu sisi tunazo taasisi zote ulizo orodhesha, lakini hakuna uwajibikaji. Unakusanya kodi lkn zinaishia mifukoni mwa kupe wa kijani.
 
Back
Top Bottom