Anachofanya Ibrahim Traore ni kizuri ila kinakosa misingi ya utawala yaani ni one man show

Anachofanya Ibrahim Traore ni kizuri ila kinakosa misingi ya utawala yaani ni one man show

Afrika inahitaji kiongozi mzalendo, mchapa kazi,anayechukia na kukomesha rushwa na mwenye maono.. na hayo ndio msingi mkuu wa utawala bora.

Afrika haiitaji utawala bora wa aina unaoutaka wewe mleta mada na watu wanaokusapoti kwenye hii thread, uongozi wa kupokezana pokezana na kubishana bishana kwa afrika hii ni kupoteza muda na rasilimali.
 
Wee kwani kila mtu anaishi mjini
Kama unajua Hilo Kwa eunaropoka vitu vya uongo , uzushi na usivyovijua?

Ni lini Kijijini wanaunganjsha umeme Kwa 300k?

Ni Lini kwenye Vitongoji vya pembezoni mwa Miji watu wanaunga umeme Kwa 300k?

Ndio maana nimekwambia wewe na huyonaepoteza energy kumsikiliza ni wajinga pro max na hamjui kwamba mnazungushwa kama bendera.

Nilimsikia anazungukzia Hadi Mbolea na wakulima nikacheka sana
 
Ni ukweli kwamba anachofanya Ibrahim traore ni jambo zuri in term of mabadiliko ni jambo ambalo waburkinafaso wanafurahia ma waafrika wote wanafurahia

Hawa viongozi wengi wa afrika ambao ni charismatic wanachangamoto moja inayofanana wana-upeo na hesabu ndogo sana naweza sema hivyo wako ambao watakuwa supprise sana na hii statement bali ndo ukweli

Hawatengenezi taasisi imara mfano
  • Mahakama huru
  • Bunge huru
  • Mamlaka ya kupambana na rushwa huru
  • Ofisi ya mwendesha mashtaka (DPP) iliyokuwa huru jambo la kufahamu ni kwamba sisi kama binadamu tunapita ila ukitengeneza misingi imara inaweza dumu
  • Tume huru ya uchaguzi ambayo traore hataki hata kukiongelea

Hata sankara aliongoza nchi as if ataishi milele akasahau sisi ni wapitaji hapa duniani

Kilichotokea Libya kinaweza kuwa somo kwetu waafrika lakini sisi ni ngumu sana kujifunza gaddafi aliitengeneza Libya sana ila ilikuwa ni one man show yaani hakutengeneza taasisi imara, kama Libya ingekuwa na taasisi imara basi hata bila uwepo wa gaddafi nchi ingeendelea vizuri tu

Mimi kiongozi ambaye haamini kwenye strong system basi nakua nimeshamshusha sana kwa sababu hicho anachokifanya ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga bila msingi siku ikija mvua kubwa na upepo basi myumba inabomoka sababu mfumo wowote lazima uje uwe tested kama ni imara au la

Ibrahim traore anayoyafanya yaendane na mifumo imara ya kuitawala nchi na sio one man show

MIMI NIKIWA RAIS WA TANZANIA NTATENGENEZA MISINGI IMARA YA UTAWALA HATA KAMA SITAKUWEPO BASI MAMBO YANAENDELEA KAMA KAWAIDA NA VIZURI ZAIDI

One man show ndiyo njia ya kufikia hayo unayo yataka uwezi kufikia huko bila ya one man show kwa taifa lililo kwisha kuoza kwa ufisadi na rushwa na uzembe ...kumbuka kinacho zuia katiba mpya na nzuri na ya haki ni watu waovu wanao nufaika na katiba mbovu ili kubomoa hiyo code ni lazima upate Rais mzalendo mwenye mbinu za one man show kwanza ili kubomoa hiyo code ...hapa tz tulimpata JPM alisema tusubiri kwanza anyoshe nchi ...hayo mambo mengine yangekuja ...swali kwa nini nyinyi mnawalaumu viongozi wanao jenga nchi zao kwa kutumia kanuni ya one man show wakati atuwaoni mkiwa laumu wasio tumia kanuni ya one man show na awaleti hayo mnayo ya dai ...
KWA NINI LAWAMA ZA KUKOSA MIFUMO THABITI IWAANGUKIE HAO VIONGOZI WA ONE MAN SHOW WAKATI HIYO MIFUMO MIBOVU ILIKUWEPO HATA KABLA YA HIYO ONE MAN SHOW MNAYO IPONDA ....NATAKA MAJIBU KAMA NYINYI SIYO WANAFIKI.
 
Afrika inahitaji kiongozi mzalendo, mchapa kazi,anayechukia na kukomesha rushwa na mwenye maono.. na hayo ndio msingi mkuu wa utawala bora.

Afrika haiitaji utawala bora wa aina unaoutaka wewe mleta mada na watu wanaokusapoti kwenye hii thread, uongozi wa kupokezana pokezana na kubishana bishana kwa afrika hii ni kupoteza muda na rasilimali.
Uzalendo,uchapakazi ndio vitu gani hasa? Wapi Afrika hii hawachapi.kazi na sio Wazalendo? Huko Burkinafaso Kuna kipi Cha ziada ambacho hakifanyiki kwingineko?

Mna ujinga mwingi sana.
 
Uliwahi unganisha umeme Mjini Kwa 27k? Vitu vya Bure vinaendekeza uvivu na ujinga.
Wewe jamaa ni mpumbavv sana, kwa hiyo kwa hii nchi ilivyobarikiwa vyanzo kibao vya kuzalisha nishati ya umeme wewe unaona suala la kuunganisha umeme kwa 27,000/= linashindikana???

Tatizo ulishambishwa makombo na genge la samia kwa hiyo sasa hivi chochote anachokifanya kwako ni jambo jema.
 
Unakua na Mahakama then mahakamani zinapokea maelekezo kutoka juu katika maamuzi au DPP mpaka apokee maagizo hapo kuna Uhuru gani Traore hamegoma kua mnafiki kujificha kwenye mihimili ambayo anajua atanipa maagizo kama zilivyo serikali nyingi za Afrika
 
Unachoongea sio sahii
Sasa siuonyeshe huo usahihi mkuu
.kuipinga tu hoja Kwa kusema unacho ongea sio sahihi without fact inakua hauna tofauti na mtu aliyepo vijiweni

Inatakiwa uje na fact ili sisi tunao fuatilia mjadala tupate kuelimika umekuja na hoja ya weza kuwa ni hoja nzuri

Ila kitendo Cha kushindwa kuitetea hoja yako mwisho wa siku itaonekana kuwa Haina Mashiko
 
Kama unajua Hilo Kwa eunaropoka vitu vya uongo , uzushi na usivyovijua?

Ni lini Kijijini wanaunganjsha umeme Kwa 300k?

Ni Lini kwenye Vitongoji vya pembezoni mwa Miji watu wanaunga umeme Kwa 300k?

Ndio maana nimekwambia wewe na huyonaepoteza energy kumsikiliza ni wajinga pro max na hamjui kwamba mnazungushwa kama bendera.

Nilimsikia anazungukzia Hadi Mbolea na wakulima nikacheka sana
Wee tuache nanujinga wetu.....tunaupenda ujinga wetu. Nyie wente akili mbona hatuoni mnalofanya
 
Nyerere alifanya au niseme ameyafanya hayo. Kaomba uhuru kwa mzungu/malkia,akaunda taifa lenye taasisi huru na kuweka sheria ambazo kwa nyakati zile zilikuwa sahihi kabisa na muda wa kutoa kijiti ulipofika akawaachia wenzake bila kuleta ligi,ila nini kimefuata?

Waafrika sisi tuna kauzembe fulani kuanzia ngazi ya familia. Tutawalaumu sana hawa viongozi tunaowapa uongozi na mamlaka ila tukubali kuwa sisi ni wazembe katika kujisimamia tunataka atokee mtu aifanye kazi ya usimamizi na ndio maana watu kama akina Gaddafi wakiingia hawataki kutoka maana wanajiuliza atamuachia nani.

Hapa saa hii tuna tatizo la viongozi kuchezea sheria na mamlaka,tunabakia na kazi ya kuwalaani kwa maneno huku vitendo vyetu vikikinzana na maneno.

Hatusomi katiba na kuielewa vema ili tuweze jua nini cha kuongeza na nini cha kutoa tunabakia kulalamika.

Hivi unadhani ni kazi rahisi kwa mtu m'moja kusimamia taasisi zote?

Wewe kama mzalendo wa taifa hili kwa nafasi yako huwa unatumia mamlaka yako ya kizalendo kuwajibisha wale wanaochezea taasisi?

Tukitaka huo ubora wa kiutendaji inaanza na sisi raia kuwa wakali na kusimama pamoja. Mfano mnasimamishwa kwenye foleni ili hawa wavaa makoti na wachezea kodi wawaishwe nyumbani kukata gogo ninyi kama raia how do you stand up na kusema hii si sawa?

Mbunge analipwa million 12 kwa mwezi mwalimu wako aliyekufundisha wewe kaka yako,baba yako na pengine anamfundisha mwanao kwasasa,umeshawai kumtetea alipwe walau milioni mbili kwa mwezi au awe na stahiki nzuri ili maisha yake yawe mepesi?

Je,hapa saa hii kunatabia ya viongozi kuzima internet pale kunapokuwa na mijadala muhimu ya changamoto za kitaifa,je tumewawajibisha TCRA watuambie nani anatoa maagizo ya kuzima internet?

Je,ikatokea umeenda bank kuna Teller anafanya mapozi na ninyi raia mpo tu hapo mnajisonya na hamuwashi moto ili afukuzwe kazi tuwekewe teller makini,unategemea tutafuta viburi vya wafanyakazi wasiojua wajibu wao?

Mimi nadhani inaanza na sisi kwanza kuwa wawajibishaji na ndipo watu kama akina Traole hawatoona haja ya kufosi kuendesha inchi kwa maono yao binafsi na watu wanaosikilizana nao wao.

Hapa saa hiu tunachangamoto ya serikali ya sasa kushikwa na kuhodhiwa na watu wachache na tunawajua why hatuwahoji kama raia na kuwawajibisha kisheria na kufuta stahiki zao?

Mfano labda tunaona kikwete anazingua,then kama raia tunaweza sema afutiwe stahiki zote za kiongozi mstaafu mwenye heshima na tukomalie awajibishwe kisheria kwa mambo ya hovyo?

Ila tukiamini kuwa sisi ni wa kusaidiwa,kufanyiwa kutetewa,kupiganiwa,na kusikilizwa tu bila kujipa wajibu wa kizalendo kwa mujibu wa sheria then tunatengeneza tatizo kubwa sana sasa na hapo baadae.

Tubadilike sasa
Top comment
 
Uzalendo,uchapakazi ndio vitu gani hasa? Wapi Afrika hii hawachapi.kazi na sio Wazalendo? Huko Burkinafaso Kuna kipi Cha ziada ambacho hakifanyiki kwingineko?

Mna ujinga mwingi sana.
Huwa napata shida sana kuwaelewesha wapumbavv wa aina yako ambao mmejazana humu.

Unauliza ni wapi Afrika hawachapi kazi na sio wazalendo?

Anyway nchi yako hii ya tanzagiza ni jibu tosha kabisa kwa hili swali lako la kipuuzi.. kama uko Dar njoo maeneo ya kwa Mkuwa hapa wilaya ubungo nikuonesha mwalimu wa Secondary shule ya serikali jirani yangu ambaye mpaka muda huu saa tatu hii bado hajaingia kazini yuko bize na biashara yake, na wala hana wasi wasi wowote.

Na pia nenda Mwanza kwenye ofisi za almashauri ya wilaya ya Ilemela ukajione majitu mavivu ambayo hayaskilizi hata shida za watu, kazi yao ni kudhulumu viwanja vya wenyeji na kisha kuviuza kwa mafisadi na wezi wenzao.

Nenda TRA huko kwenye ofisi yoyote uone wakwepa kodi wanavyolipa faini ndogo na yenyewe haiingii serikalini ukilinganisha na kiwango sahihi wanachodaiwa.

"Huko Burkinafso kuna kipi cha ziada ambacho hakifanyiki kwingineko?"

Huwezi kulinganisha utawala thabiti chini ya Captain Traore na huu utawala wa kipumbavv uliojaa maudhi kibao wa chura kiziwi.

Nyie wala makombo ya mafisadi ya ccm huwa mnamchukia sana Traore, mnatamani mama yenu chura kiziwi ndio angekuwa anapewa hizi sifa anazopewa Traore.
 
Sasa siuonyeshe huo usahihi mkuu
.kuipinga tu hoja Kwa kusema unacho ongea sio sahihi without fact inakua hauna tofauti na mtu aliyepo vijiweni

Inatakiwa uje na fact ili sisi tunao fuatilia mjadala tupate kuelimika umekuja na hoja ya weza kuwa ni hoja nzuri

Ila kitendo Cha kushindwa kuitetea hoja yako mwisho wa siku itaonekana kuwa Haina Mashiko
Fuatilia conversation ya nyuma nimeshamjibu yeye ndo anakaza fuvu
Kwa kukusaidia Afrika hatuitaki demokrasia yenyewe sababu tunapenda vya kunyonga
 
Huwa napata shida sana kuwaelewesha wapumbavv wa aina yako ambao mmejazana humu.

Unauliza ni wapi Afrika hawachapi kazi na sio wazalendo?

Anyway nchi yako hii ya tanzagiza ni jibu tosha kabisa kwa hili swali lako la kipuuzi.. kama uko Dar njoo maeneo ya kwa Mkuwa hapa wilaya ubungo nikuonesha mwalimu wa Secondary shule ya serikali jirani yangu ambaye mpaka muda huu saa tatu hii bado hajaingia kazini yuko bize na biashara yake, na wala hana wasi wasi wowote.

Na pia nenda Mwanza kwenye ofisi za almashauri ya wilaya ya Ilemela ukajione majitu mavivu ambayo hayaskilizi hata shida za watu, kazi yao ni kudhulumu viwanja vya wenyeji na kisha kuviuza kwa mafisadi na wezi wenzao.

Nenda TRA huko kwenye ofisi yoyote uone wakwepa kodi wanavyolipa faini ndogo na yenyewe haiingii serikalini ukilinganisha na kiwango sahihi wanachodaiwa.

"Huko Burkinafso kuna kipi cha ziada ambacho hakifanyiki kwingineko?"

Huwezi kulinganisha utawala thabiti chini ya Captain Traore na huu utawala wa kipumbavv uliojaa maudhi kibao wa chura kiziwi.

Nyie wala makombo ya mafisadi ya ccm huwa mnamchukia sana Traore, mnatamani mama yenu chura kiziwi ndio angekuwa anapewa hizi sifa anazopewa Traore.
Mwalimu mmja ndio kielelezo Cha Taaluma nzima ya walimu?

Utawala thabiti ni matokeo Sasa kina kipi Cha maana ambacho kinafanyika Burkinafaso na Tzn hakifanyiki?

Saba sana hao kina Traore ndio wanakuja kujifunza au unabisha nikupe.ushahidi?

Wewe ni mpumbavu unaropoka tuu
 
Huwezi kutengeneza misingi ya kiuongozi kwenye mataifa yenye njaa na yaliyojaa wezi na wabinafsi na uchumi tegemezi kama ya Afrika...
Wengi mnaongelea theory fikirika ambazo hamna popote zinapofanya kazi kwa nchi kama zetu..
Ndo maana hakuna nchi yoyote ya Afrika yenye utawala na uongozi ulio kwenye mstari...
 
Wee tuache nanujinga wetu.....tunaupenda ujinga wetu. Nyie wente akili mbona hatuoni mnalofanya
Wewe ni mjinga na utakua na kulishwa ujinga Kwa maslahi ya Slowslow.

Slow Slow hana tofauti na Kigogo,Mange na wajinga wengine ambao wanatumia Lindi kubwa la nyie mbumbumbu kupata hela Kwa njia ya views, comments etc huki nyie mkiambulia matangopori Kwa sababu za kukosa na kushikiwa akili.
 
Back
Top Bottom