Anachofanya Ibrahim Traore ni kizuri ila kinakosa misingi ya utawala yaani ni one man show

Hofu yangu ni kubwa sana ngoja tuchunguze kabla ya kuungana kusifu.Mambo ya Magu siwezi kusahau kirahisi.Upande mmoja ulikuwa unashangilia,upande mwingine vilio vilikuwa vya hatatari
 
Mama anaupiga mwingi , ng'ombe wa mama kila kitu cha mama , hizi kumbe ni sifa jumuishiπŸ˜…
Sifa zinaenda kwake lakini mfumo wa utendaji ni shirikisho na unaozinhatia sheria badala ya matamko kama ya kina Traore.
 
Hakuna nchi yeyote afrika inayofuata demokrasia hili ni vizuri ukalifahamu nyingi zinaigiza demokrasia
 
Wee wacha tushikwe akili ata wakitaka watushike hadi mbupuz
 
Huyo jamaa yako ni suala la muda tu,lazima wahuni watamchomoa
 
Kwa Afrika mtu kama Traore ndiye afaa kuongoza kwa kipindi fulani huku akiimarisha hizo taasisi unozidai.

Hadi sasa kuna machache ambayo Traore ameyafanya tangu ashike nchi:

1. Watoto wanasoma bure na kila shule yahakikisha mwalimu yupo na afanya kazi yake.

2. Kila shule watoto wavalia sare za shule ambazo zauzwa kutoka humohumo nchini hivyo kuwasiadia watengenezaji nguo wa ndani.

3. Sasa hivi Burkina Faso yajenga barabara zote ziwe za lami hadi kufikia 5000 kwa mwaka kutoka kwenye kusuasua kwa barabara 3000 kwa mwaka.

4. Chini ya uongozi wa Traore vipo viwanda karibia vinne vimejengwa vya kusindika nyanya na matunda na viwanda hivyo vimejengwa kwenye maeneo ya wakulima ili ilwe rahisi kutoa ajira na kuwasaidi wakulima.

5. Hadi sasa kuna magari ya aina tano (Models) yanoundwa nchini Burkina faso yenye kutumia umeme na yenye majina mbalimbali kama Sahel, Tqqaua na mengine.

6. Ili pia kwenda sambamba na wananchi wake wanomlinda usiku kwa zamu isi asidhuriwe, Traore amebadilisha majina ya barabara khasa ile kuu ya Charles Gore ambayo imekuwa ikikumbisha fikra za kikoloni na kuipa jina la Thomas Sankara.

Na traore amefanya hayo huku akikwepa majaribio yapatayo 19 ya kumuua yanoratibiwa kutoka nje ya nchi hiyo kwa wale ambao walidhani wangeweza kuitawala nchi hiyo kifikra milele.

Wananchi wengi wa Burkina faso wamejitambua na wajisikia furaha kuwa na kiongozi kama huyo ambae hujali nchi yake na wananchi wake kwanza kabla ya mengine.

Kwahiyo ukiangalia sana hii kitu demokrasia yaweza kuwa na matokeo mazuri endapo tu nchi imejengwa uzuri katika muktadha unousema wa taasisi imara ambazo pia kwa sasa nchin humo taasisi hizo zafanya kazi zake bila shida zilikuwepo kabla.

Hivyo, kutokana na yanoendelea Duniani kote kwa kila nchi kujitafakari na kuamua kuchukua maamuzi magumu ni jambo la uzuri pia kwa nchi za Afrika kujitafakari na kuamua ni njia ipi sahihi ya kuchukua ama ya kufuata uhuni wa CCM na mifumo yake kandamizi au kufuata akili ya kujitambua.
 
Traore kwa Dunia ya leo hana faida na mfumo anaoutumia ni ule wa 1300 wa Uingereza "Monarchism" ambao watu wengi hawatoi maoni yao na Maendeleo yanafanyika as a favour.

Kama ulivyoandika ni Muhimu kiongozi bora kutengeneza Taasisi hata kama hautakuwepo mambo mazuri yatafanyika pia kiongozi anajipunguzia maadui maana mambo mengi yanafanywa na Taasisi sio Rais.
 
Unafananisha demokrasia ya nchi za Western na za Afrika serious
demokrasia ni kitu cha kufikirika, kimeanzishwa na wanasiasa kwa ajili yao hao hao wanasiasa.. hivi we kama mwananchi demokrasia una nguvu nayo vipi bila nguvu ya hao wanasiasa?

hata huko magharibi hao wanasiasa wako chini ya influence ya same big corporations, lobbyists, na elites.... hata vyombo vya habari vinatumika kimkakati .
 
Taasisi ni Muhimu sana maana ikitokea akaondoka hayo mazuri yote yatatoeka.
 
Kwa hiyo ulitaka nizunguke Tanzania nzima nichunguze tabia za walimu wote kisha ndio nije na coclusion? Hivi una elewa hata statistical sampling inavyofanyika mbwa wewe?

Ulitaka nipite kwenye kila ofisi ya uma hili nibaina wazembe ni wapi na wachapa kazi ni wapi na wako wangapi? Kwani hata huyo kafulila wenu hizo data anazotoaga huwa anazunguka tanzania nzima kama sio kufanya sampling?

Kwa hiyo unakataa hapa Tanzani watumishi wa uma ni wachapa kazi na sio wazembe?

Wewe jamaa ni kumer sana tena mpumbav wa kuzaliwa haya kama nyie watanzania sio wazembe na ni wazalendi mko makini na kazi yale mabilioni ambayo kila mara yanasomwa na CAG yanapoteleaga wapi?

Eti nini hao kina Traore wanakuja kujifunza hapa kwenu?

Aisee una mzaa sana fala wewe, Traore aje ajifunze nini kwa huyu mama ako wa kizmkazi dalali wa rasilimali za taifa?

Yaan Traore kabisa aje ajifunze kwa Samia? Ajifunze nini sasa? kufuga mafisadi na wazembe serikalini au?

Traore kwanza akisikia yaliyofanyika kwenye mkataba wa DP world hawezi hata kukaa meza moja na huyo bibi yako wa kizanzibari maana atamdharau sana.

Utawala thabiti unaonekana kwa matokeo ndio, na kwa mambo aliyofanya Traore kule Burikinafaso(zaman Upper Volta) ni makubwa sana kulinganisha na muda aliokaa madarakani.

Ndio maana ni dhambi kubwa sana kumlinganisha Traore na taka taka zingine hapa afrika ikiwemo ya taka taka ya kizimkazi.
 
Ndio maana nikakwambia wewe ni mpumbavu huwezi hitimisha hoja Kwa poor samplings,shule ulienda kukuza nywele.

Yapi hayo makubwa ambayo hayafanyiki kwingineko?
 
Taasisi ni Muhimu sana maana ikitokea akaondoka hayo mazuri yote yatatoeka.
Atafuata mtu mwingine mwenye hulka,akilo na mzalendo wa aina yake...

Forums
https://www.jamiiforums.com/forums/Kuna watu wanaamini etii siku Kagame akiondoka basi Rwanda itapitia wakati mgumu sana, ila mimi nawaambieni Rwanda itaendelea kuwa imara tena maradufu zaidi, Kagame sio mjinga lazima ataacha successor wa aina yake.
 
Acheni ujuaji,
Mtu akifanya vizuri shida,akifanya vibaya shida
Ingekua wewe ungeweza?
 
Waafrika gani hao wanaojitambua sasa bora hata hao one man show uacha legacy ya vitu vinavyoonekana
 
NYIE MSIFIENI TU BAADAE AKINGANGANIA KAMA WAKINA MUSEVENI NDO MTAJUA MLIKUWA MNAKURUPUKA KUSIFIA NGOZI NYEUSI SISI SIO WAKUAMINIANA SANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…