Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Notice kwanza hujui sharia ya madai nn zen shida itafata

mimi sio mwelewa hilo nakubali 100% ila ambacho sikubalini eti KUKWEPA KODI ni kesi ambayo hukumu yake unatakiwa ulipe tu. kama wameshahukumu hivyo nini sina tatizo nao ila watuambie sheria inasemaje mtu kutorosha kontena ili asilipe kodi. Na ni kinanani waliotorosha, ni kiasigani cha kodi kila mmoja na wakilipa tuambiwe ni kina nani tusije tukabaki na hisia labda fulani kakwepa kodi
 
Inanishangaza sana wa2 wanatuibia kiasi kikubwa cha hela ambacho hatujatangaziwa ni kiasi gani tunaambiwa kirahisirahisi eti wakirudisha ndani ya siku saba watasamehewa. Hii ni only in Tanzania sijawahi sikia nchi nyingine. Watuambie kupitia gazeti la serikali ni kina nani wamekwepa kodi kiasi walichokwepa na kuanzia lini. Pia sheria inasemaje na wakitimiza matakwa ya hiyo sheria tuambiwe. Isije ikawa changa la macho kama ile EPA. Hizi za sasa ni nyingi mno jamani viongozi wetu waache kubembeleza majizi

tofautisha kukwepa kodi na wizi hayo ni maneno mawili tofauti yenye maana tofauti.
 
Endeleeni kutumbua majipu viongozi wangu,
Hawa wanafki wachache hawawezi kuwarudisha nyuma,

Go Magufuli,
Go Majaliwa.
 
Na hao mawaziri sasa wakianza kazi
itakuwa full bongo movie kila wizara

Hao mawaziri sijui watawapata wapi waandishi wa habari..maana kila waziri atataka akavamie mahala flani akiwa na waandishi kibao ili magu amuone anavyo chapa kazi..hapo bado waku wa wilaya..kweli itakuwa bongo muvi
 
Ili uendelee kuwavua chupi na kuzini na watoto wa wenzako.Zaa wako nae umfanye kama unavyowafanyia wa wenzako, usipomvua wewe atavuliwa na wengine kama first law of KARMA inavyosema mpumbavu mkubwa wee.Jinga kabisa.

ndugu yangu mi sio mwalimu mi ni mtaalamu wa kudukua mitandao ya internet kama snowden.nilikuwa nafikisha ujumbe kwa wazazi so mpumbavu mwenyewe kama hukusoma literature mlaumu babako jinga wewe
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Sasa anamuumbua nani? Kwani kuna wenye heshima hapo? Mbona Lema alishasema kuwa watanzania wanahaki ya kumzomea mwizi. Huwezi kudai heshima wakati hujiheshimu. Mwizi hastahili heshima hapa duniani hata kule mbinguni. Endelea PM wetu tuko nyuma yako.
 
Mimi naamini.mifumo ipo ila aifanyi kazi kwa sababu ya uzembe na mazoea yetu ya kufanya kazi.Namsaport waziri mkuu kwa sasa kufanya hivyo kwani itasaidiq kua assess na kuja na maboresh😵therwise ndio maana mkoloni aliweza kututawala kwani miafrica haiendi bila fimbo.
 
Hayo ni maoni yako ni kwanini unataka uyalazimishe kwa WatanZania wote? Hayo ya utawala bora ni kulingana na tafsiri yako wewe na jinsi unavyoongoza familia nyumbani kwako usitake kutuletea kwenye nchi yetu, tumeshatoka huko, tumeshayafanya yote hayo ya kuitana faragha, kuundiana tume, kuonyana kwamba ninawajua wala rushwa msipojirekebisha mtakiona cha mtema kuni kote huko tumepita lkn matokeo yake ni kwamba makontena zaidi ya 2500 hayajalipiwa kodi, yaani yamekombolewa Bandarini bila kulipiwa sasa huu ni uhujumu Uchumi na kwa nchi nyingine adhabu yake ni sawa na Uhaini kwani unalinganishwa na uuwaji watu wote waliofia mapokezi kwa kukosa dawa hospitalini wameuliwa na hawa wezi!

Hivyo tuache na Magufuli wetu tumeshamkubali jinsi alivyo na vyovyote anavyofanya ana baraka zetu, na ndio maana ya kushinda Uchaguzi na kuwa Raisi vinginevyo basi kila mtu angejiongoza?

Yaani ulichoandika hapa kinaonyesha una akili nyingi mpaka kero. Kula like 10,000. Very-very well said.
 
Tutegemee kusikia vilio vingi kama hivi wakati majipu yakitumbuliwa!! Nasema Majaliwa, Kasim Majaliwa yuko sawa 100%, Good governance ni pamoja na kwenda na facts ili usimuonee mtu, Hao wanaoongea uongo mpaka wawekewe facts mezani ndio wasio na good governance!! Enough is Enough haiwezekani watu wakatumia migongo ya watanzania kujilimbikizia fahari za dunia huku maskini wakiteseka... Pasco tuachie Musketeers wetu wafanye kazi, ikiwezekana waende na viboko kabisa watu wacharazwe hadharani hata kama ni mimi nimekutwa na huu utumbo nicharazwe tu manake hamna namna ingine ya kuponya taifa hili. Tuwaonye tu wale mnaotaka kupotosha, tutasimama na Mh Rais kwa kila jambo
 
Last edited by a moderator:
Mtoa hoja uwe na hata chembe ya aibu kutoa hoja kama hii, anachofanya Rais wengi wamekikubali. Ungekuwa umesomea uongozi wa umma kwa level ya juu ungemwelewa Rais ana maana gani kutumia technical hiyo.

Tatizo naloliona kwako si uelewa tu wa taaluma ya uongozi bali hata kuchanganua mambo kidogo kwako ni ngumu.

Si kweli kama unavyotaka kuudanganya Umma,usifikiri walioshiriki vitendo hivyo vya kihalifu ni watu wepesi,vitendo hivyo vimefanywa na vigogo wa Serikali kupitia Kampuni zao.Kama sheria ingefuata mkondo wake,sakata hili lingeiacha uchi serikali yenyewe.

Kitendo cha kuwapa muda wakalipe kodi ni kusalimu amri baada ya kugundua wahusika wa sakata hilo ni watu wazito wasiogusika.Mh Pinda alishawahi kukiri hadharani kuwa wanaofanya vitendo vya ufisadi ni watu wazito ambao ukiwagusa nchi itayumba.

Zilikuwa ni kelele tu,wenye nchi wamempa onyo la kuacha kufukua "makaburi ya ufisadi" kuendelea kufukua makaburi hayo kungeweza kusababisha uchafu wa watangulizi wake ujulikane na kushusha kuaminika kwao.

Zipo wapi bilioni za EPA tulizoambiwa zilirudishwa na wezi?Tuliishia kuambiwa tu kuwa zilirejeshwa bila kuambiwa zilirejeshwa ngapi.
 
Kumuuliza mkurugenzi wa TRL kuwa mlipata wapi idhini ya kukopa hela TIB it wasn't professional, halafu kuna maswali na vitu vya kuzungumza mbele ya waandish wa Habari,
 
Civility, good governance, courtsey and what have you! Vimetusaidia nini kama sio kuacha mchwa wa JK kuitafuna nchi hivi? Kwa nini hao unaowalilia hawakutumia professionalism kusimamia Sheria taratibu na kanuni za kazi zao kama ilivyostahili!? Its pay back time Pasco, nchi hii alipoifikisha JK inahitaji shock therapy kuinasua hapa! Jerry Rawlings wa Ghana alikwenda mbali Saudi, hawa mchwa aliwatandika risasi hadharani na sasa Ghana mambo tambarare kabisa!

Habari ya business as usual haitusaidii, hakuna haja ya kuwa mstaarabu mahali ambapo hakuna ustaarabu, mtu mzembe na mwizi shurti aitwe hivyoo, hakuna kurembaremba!! Go go Majaliwa

Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco
 
Khaa!! Dawa ya jipu ni kulitimbua tu. Japo kuna maumivu lakini hakuna namna nyingine
 
anataka amfunike pinda ili yeye apate sifa na umaarufu zaidi

Bilions and bilions zimepotea then aende kuwachekea??? kweli??? Tumechoka na ufisadi, ubadhilifu, wizi wa mchana kweupe, uzembe kazini, usanii na umangi meza. PM na JPM tupo nanyi daima na tunaendelea kuwaombea
 
Yani kamizani kangu cha sh 100000,nimelipia kodi alafu unasema watu wanaoacha makontena yapite free unawatetea hapa.Hapana na sisi tunataka haki itendeke.Majaliwa fukuza kazi kabisa hao wapiga dili.
 
Waziri mkuu yuko sahihi kabisa na hiyo ndiyo njia pekee ya kuwaondoa watu wasio na sifa waliojaa kwenye utumishi wa umma hawajui mambo yanayotendeka ndani kazi kwao ni kusafiri tu, kuweka saini kwenye makaratasi yaliyoandaliwa na watu wa chini bila kuyasoma bali kuchagua watu wao na wanachowaambia wao wanaamini na kusaini tu na kuweka percent kwenye manunuzi.

mkurugenzi natakiwa kuwa na majib ya kila jambo linalokea kwenye taasisi yake kichwani kuhsu mambo ya kiutawala. mambo ya kiufundi mpaka watu wa chini wampe ajibu na kama waziri mkuu anakuja na tuhumakama ni mtendaji makini bado atatoa majibu ya kuridhisha hapohapo.

kosa ni kumpa mda akajandae basi wanatengeneza majibu ya kuridhiha hatakama yako tofauti na ukweli.

kwa watanzania anachokifanya waziri mkuu ndio utawala bora wewe unayetaka staili kama ya waliopita tunasema wewe hufai kuwa kongozi na hivyo huwezi kumshauri kiongozi
 
Magufuli anatumbua majipu usaha unawarukia akina Pasco pembeni!

Mzee Mwanakijiji alisema haya maumivu ya majipu yatatukuta wote hata tulioko huku Nakapanya!
 
wao walipikuwa wanapora mali ya umma hawakudhalilisha taifa na kusababisha mateso kwa watanzania?wacha waisome namba.jino kwa jino.
 
Ukicheka na nyani utavuna mabua! Yaani umchekee CEO aliyepitisha mabehewa 2,400 bila kulipia kodi eti umwite ofisini ukaongee naye kwa ajili tu ya utawala bora? Huo utawala bora ukoje!
 
Back
Top Bottom