Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Pasco. Good governancy ni kuwa mnafki kama una taarifa ya ulicho kifanya kwanini una shindwa kuelezea. Au mlizoea mfumo wa kuundiwa tume kila kajambo kadogo kanako tokea. Na ripoti zina somwa kimya kimya ishu inaishia jukwa juu.
 

Huyu pasco huwa ananishangaza sana kwa kweli...sijui definition yake ya good governance ni nini hasa! Yani CEO au Manager anaulizwa swali na waziri, ANADANGANYA mbele ya kamdamnasi, eti mfumo uko perfect kabisa, alafu eti pasco anasema waziri amlinde huyo mtu mbele ya kadamnasi, eti aende akamuulize hayo maswali kwenye kakichumba! khaa!!
Mie nilimsikia yule manager sijui ni wa bandari, alivyoonyeshwa zile data, akaanza kuweweseka eti ohooo muheshimiwa ningekuja kukupa hizo information baadaye lakini sio hapa! Loh!
Yani ni kwamba hawa watu wamezoea kudiscuss haya MAUONGO yao na UBABAISHAJI wao huko ndani ya vijumba na yanaishia humo humo ambako hakuna mtu anajua nini kinaendelea au nini kimeamuliwa...
Mie naaminni kuwa kama hao ma-CEO wasingedanganya mbele ya kadamnasi, wakatoa majibu ya ukweli kama ilivyo, then wasingedhalilika.
 
S niliweka uzi kuuliza bandari imesafishwa nini na kina Mwakyembe na Sitta?
mkanijibu bandari iko safi tatizo liko TRA?
Tatizo lao huwa wamepotshwa na ushabiki hadi mantiki huwa hawazioni. kwenye lilee bandiko walidai Bandari ni safi tatizo ni TRA. Ilipokuja hoja kwamba kama tatizo ni TRA geti namba 5 lipo TRA? Wao wakang'ang'ania kuwa tatizo ni TRA, leo tena wanasema tatizo ni Bandari, wala hawajielewi!!
 
Kwa hiyo mnataka kusema kwa kuwa kuna mtu mtaani kweni kakutwa anabaka katoto kadogo, na nyie suluhisho ni kupiga mpaka afe?
 
Wabongo bwana ! Magufuli hakuna kupunguza spidi ! Majitu mALAFI ETI NINI WACHEKEWE ????
 
Mkuu mie nakushauri tazama maswali wanayo ulizwa viongozi wa kiserikali na kamati za mabunge ya marekani ( congress and senate) katika uteuzi kuwa waandamizi wa serikali au inapotokea scandal naserikali inatakiwa itoe maelezo.

nikupe mfano Hillary Clinton juzijuzi tu hapa aliitwa kujieleza kama waziri wa mambo ya nje aeleze uwajibikaji wake wa kifo cha wamarekani kadhaa Bengazi akiwemo balozi wa marekani nchini libya, hebu tazama yale maswali kwa masaa 12 kawekwa kiti moto, namengine mengi tu. alafu linganisha na hiyo nusu saa wanazopewa maofisa wa serikali Tanzania utupe mrejesho

[video]http://nyti.ms/1GXXSfv[/video]
 
What i do believe good governance inaendana na transparence.kwa hio anachokifanya waziri mkuu ni sawa kabisa.
 
Umwite aliyesababisha makontena yapotee mkajadili, kisa utawala bora, let them go to hell, we will employ others. nchi inanuka rushwa, ufisadi wa kutupa. matajiri wanatamba kwa pesa za wizi.....
 
Sijashawishika kabisa na hoja mfu za Pasco,
Kwa hapa tulipofika kama nchi, tunataka mtu wa jamii ya Magufuli na Majaliwa. Kufanya kazi kwa mazoea kuishe na kuondoke kabisa na awamu ya nne. Sisi tulio kwenye sekta binafsi tunajua maana ya kuwajibika, kila wakati tuko alert, kwa sababu hatujui saa wala dakika ambapo kinaweza kunuka. Serikalini mmezoa mdebwedo.
Pole sana brother.
 
Last edited by a moderator:
Pasco kwa mfano hao wanaoshtukizwa wangesema ukweli hio karatasi aliokuja nayo ingewadhalilisha?? Wamesema uongo ndio maana anatoa data ili kuthibitisha uongo wao.
Like siioni ila ujumbe wako mujarabu kwa huyu Pasco.Watu wanafanya kazi kwa mazoea tu wizi wizi tu,uongo uongo,Pasco unaangalia upande mmoja wa shilingi huoni mara ya kwanza huyo menaja wa bandari aliongopa na alipoonyeshwa ile nondo akaanza kujikanyaga wewe unaona hiyo ni sawa??acha wanyooshwe tu maana hakuna namna nyingine.Mimi naona hiyo ni cha mtoto ila tulipofikia ilibidi tumpate dicteta kwa miaka mitano watu wangekaa sawa.
 
Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?

Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.

Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?


Chochote kile ukitaka kwenda mbele Zaidi kutaka kudadavua, lazima uje na tafsiri au maswali mengi!

Mmoja anaweza akahoji, kulikuwa kuna haja gani ya Mungu kuuweka mti wa katkati katika ile busatani?

------------------------
As long kuwa wamehusika na upotevu, wanatakiwa kujibu shauri lao, ila ukienda mbele Zaidi ndio unaweza ukaja na swala kuwa serikali iliopita inavuliwa nguo, au serikali iliopita imefeli! Inategemea anayehoji anataka kuliangalia hilo swala kwa mtazamo upi.

Cha msingi Zaidi ni kuwa, kama yanayo fanyika yana tija kwa jamii!
 
Hizi hela wangekuwa wakiiba wanazitumia kwa kuvizia hapo ningeungana na mtoa hoja, mijitu inatuibia halafu inatumia kwa mashauzi kuonekana kama wao wanaishi juu ya dunia lazima waumbuliwe hakuna namna malipo ni hapahapa
 
Mbona hueleweki wakinyamaza ooh wanakumbatia mafisadi wameona wanakemea oooh udhalilishaji umeshazoea kuisoma namba wewe
 
Mkuu Pasco Labda tungeanzia hapa "What is Good Governance?"
 
Last edited by a moderator:
Vyombo vya usalama kamata huyu mtu hana maana . Mwizi haitaji heshim yoyote .
 

waacha waumbuliwa nchi hii ilishaoza kila mkurutez hufqnya mambo yake...me cna cha jushaur hapo
 

Unaongeleaje kwa serikali kama ya China ambayo ingeenda mbele Zaidi ya hapo kwa kuwauwa?

Ni wakinamama wangapi wamedhalilishwa utu wao kwa kujifungilia chini, au kufariki dunia kwakuosa huduma stahiki kwa kukosekana kwa fedha ya vifaa tiba nk?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…