Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii nchi tulipofika Pasco tusichekeane. Kucheka cheka na mkeo nyumbani.
Ukiwa CEO unatakiwa kuwa na data at your fingertips. Kama hauwezi kaa pembeni.
Wanyooshwe tu. Hakuna namna nyingine
Hivi unadhani Bade alikuwa hajui kuwa makontena yalikuwa yanatolewa bila kulipiwa kodi? Hata kama hakushiriki kwa mfano. Huyo wa TRL hakujua hela ya mkopo imelipia salary?
Good governance?
Tatizo lao huwa wamepotshwa na ushabiki hadi mantiki huwa hawazioni. kwenye lilee bandiko walidai Bandari ni safi tatizo ni TRA. Ilipokuja hoja kwamba kama tatizo ni TRA geti namba 5 lipo TRA? Wao wakang'ang'ania kuwa tatizo ni TRA, leo tena wanasema tatizo ni Bandari, wala hawajielewi!!S niliweka uzi kuuliza bandari imesafishwa nini na kina Mwakyembe na Sitta?
mkanijibu bandari iko safi tatizo liko TRA?
Kwa hiyo mnataka kusema kwa kuwa kuna mtu mtaani kweni kakutwa anabaka katoto kadogo, na nyie suluhisho ni kupiga mpaka afe?
Like siioni ila ujumbe wako mujarabu kwa huyu Pasco.Watu wanafanya kazi kwa mazoea tu wizi wizi tu,uongo uongo,Pasco unaangalia upande mmoja wa shilingi huoni mara ya kwanza huyo menaja wa bandari aliongopa na alipoonyeshwa ile nondo akaanza kujikanyaga wewe unaona hiyo ni sawa??acha wanyooshwe tu maana hakuna namna nyingine.Mimi naona hiyo ni cha mtoto ila tulipofikia ilibidi tumpate dicteta kwa miaka mitano watu wangekaa sawa.Pasco kwa mfano hao wanaoshtukizwa wangesema ukweli hio karatasi aliokuja nayo ingewadhalilisha?? Wamesema uongo ndio maana anatoa data ili kuthibitisha uongo wao.
Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?
Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.
Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?
kwani kwenye jamii yetu hakuna jinsi ya kushghulika na wabakaji?? Hii tabia ya majaaliwa mnayoipogeza ni dalili kwamba nchi inaendeshwa kiporini porini!!Wewe ulitaka mtu aliyebaka katoto kadogo afanyweje?
Apongezwe??!
Wanabodi,
Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.
Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.
Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.
Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.
Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.
Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.
Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.
Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco
Barbarosa Pasco hajalazimisha maoni yake ndiyo yawe ya watanzania wote, kama wewe unaona maoni yako hayafanani na ya kwake siyo mbaya ukayapinga kwani ndiyo demokrasia. Kwa bahati mbaya sana Afrika kuna fikra mufulisi kwamba mtu akiwa madarakani apingwi kwani busara za kuongoza huzitoa kwa mungu!!
Maoni ya Pasco yanaungwa mkono na watanzania wenzako ambao wanaona Majaaliwa kama waziri Mkuu wetu anadhalilisha utu wa wale anaowahoji kwa lengo la kuujua ukweli wa ukwepwaji kodi. Hakuna anayepinga wanaokwepa kodi kufuatiliwa, lakini kama njia zinazotumika zinadhalilisha utu wa wengine ni lazima zipingwe!