Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Busara ni kuwa kiongozi yeyote ambaye angechaguliwa katika uchaguzi uliopita kama wa CCM au upinzani ambaye anataka kufanya kazi ipasavyo lazima mtindo wake wa utawala automatically unageonekana unaudhalilisha utawala uliopita.
Haihitaji uwe injinia wa Roketi kulitambua hilo

Soma uzi huu

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/281497-mbowe-aungana-na-mnyika-kusema-serikali-ya-kikwete-dhaifu-new-post.html
 
Mparaganyiko mkubwa
kaenda kwanza kagundua makontena 300
karudi tena kagundua mengine zaidi ya 2000

so inawezekana yakafika hata elfu 10 hajagundua bado
na hakuna namna ya kugundua hadi waziri mkuu aende mwenyewe..
ni kama system ime fail kabisa....waziri mkuu anafanya ukaguzi wa kontena
sio kujenga system mpya yasitokee haya tena

Come on man not from you. Sio kwamba yeye PM ndio anafanya "ugunduzi" huo, hap ana, wako wapelelezi ndio humletea data hizo. Sasa kwa sababu wakurugenzi nao ni wahusika hawawezi pelekewa hizi taarifa. Mkiwa mnaponda tumieni akili hizo hizo mnazotumia kwenye discussion zingine.
 
Huyo Mpuuzi yuko USA kila siku anatusema tunakula vumbi huku alafu bado eti hii nchi anayoitukana inamkosesha usingizi..

Mpuuzi wa Karne... USA Baby :usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2:

Namwitaga uncle ruckus. Pangekua na vidonge vya kujigeuza mzungu mjomba angemeza zamani sana.
 
Pasco

Kwa stage Tanzania tulipofikia hakuna haja ya kuitana pembeni, watu wanapoteza makontena karibu 3,000 ya billions of billions halafu unataka waitane chemba NO.

Hawa ni wahujumu uchumi nchi zingine adhabu yao ni kupigwa risasi.

Mhujumu uchumi ni sawa na jambazi huwezi kuliita jambazi pembeni eti mjadiliane.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Usitake haki bila wajibu hao unao taka wafanyiwe good governance wao wanazo hzo qualities za good governance???
Usiseme tu good governance toa na qualities za good governance ndo tukuone msomi ...
Usitetee upuuz na uvivu
 
Katika swala hili hakuna good governance

Tena ilitakiwa wapigwe makofi hadharani maana wapo kama hawapo

Uongozi Wa mzaramo ni kima nchi ilikiwa inajitawala yenyewe

Tena Mimi ninavyoona Tanzania ilitakiwa iwe recolonized tena na watu kama kina Trump, Bush na makaburu iyo mixer ingeleta manufaa sana maana ilifika hatua mpaka kina wema sepetunga wanatoa matamko ya serikali
 
Leo wezi na mafisadi wanajificha kwenye blanketi ya "good governance". Doctrine hiyo ni ya maana kama watu wanafanyakazi kwa uadilifu. Vinginevyo is useless. Magugili na Majaliwa endeleeni kuwakaba hawa watumishi wa dola mpaka wanyoke. Fukuza tuu!
 
Mkuu bado hujatuhumiwa tu kuwa unatembea na hse girl wako?
 
maumivu ya kichwa huanza poole popole...tuwekage akiba ya maneo naamini tutakuja geukana humu
 
Kinachofanyika sawa. Watu wamejisahau sana Tanzania.

Huu ni mwanzo mpaka wote wakijirekebisha ndio wataacha .

Msiopenda kazi ya magufuli na waziri mkuu mnaweza kuhamia Msoga muanzishe nchi yenu.
 
Muafrika haendi bila fimbo. Fimbo yenyewe ndio hiyo anayutimia Majaliwa

Ni kufuata sheria, taratibu, kanuni, kuoneana aibu, kuunda tume, kuogopana kumetufikisha hapa tulipo

Mlilalamika JMK anachekacheka sasa mmeletewa watu wakali mnalalamika tena. Hakuna jema machoni mwenu

Ukipewa dhamana ya kuendesha shirika Lazima uwe na full data at your fingertips ndivyo CEO wa mashirika wakubwa wanavyoendesha na kufanikiwa, ndivyo Magufuli alivyoendesha na ndivyo nchi inapaswa kuendeshwa kama hao wakurugenzi hawawezi kujibu kwanini makontena yanapotea kama pini basi hawapaswi kuwa hapo

Muafrika haendi bila fimbo
 
Acheni upuuzi wenu, muacheni rais na waziri mkuu wetu wafanye kazi. Wananchi wa chini tumedhalilishwa sana na hawa mafisadi wanaotumia ofisi zao kuangamiza uchumi. Sasa ni payback time, watalipa jasho letu. Tena ningekuwa mimi majaliwa ningepiga na vibao
 
Ngabu iko very clear hawana 'blue print' ya nini wafanye
kubadili hii nchi iondokane na kero
so wanashiriki ku expose kero na kukaripia on tv
lakini 'what to do to change things permanently' ndio hawajui...
'the blue print' ya ku replace hii failed system hawana
Nionavyo, wewe na uliyem-quote na mleta sredi mirija imekatwa! SIMPLE!
 
unachotaka kifanyike wewe ni mfano mtu akuibie halafu badala ya kupiga kelele ya mwizi ili usaidiwe kukamatwa kwake na mali yako irudi wewe unaamua kumkimbiza kimya kimya ili kumtunzia heshima yake mwizi. haha we jamaa umechemsha ujue. huna hata aibu chembe.
 
I shall.

Right now it's too early to give a thorough assessment on their governing style.

But at the same time I refuse to be caught up in the hoopla surrounding their style.
Subconsciously, you are caught up arleady! No wonder you spend a lot of energy being their critique.
 
Back
Top Bottom