Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Huyu Pinda alipokuwa PM huyu ndio sana alikuwa anaizuia speed ya magufuli kwa nafasi yake,
 
Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?

Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.

Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?

nyie chadema mna matatizo, eti wanaivua nguo serikali!? kwa ujinga wenu huu sasa naelewa kwa nini mko kimya hata chadema pale inapo haribu
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

So kama majaliwa anachofanya sio good governance vipi hao maofisa wa bandarini na TRL wanachofanya ni sawa?...
Na usitegemee hata siku moja kwa nchi yetu ilipofika tutakombolewa kwa good governance ...
 
nyie chadema mna matatizo, eti wanaivua nguo serikali!? kwa ujinga wenu huu sasa naelewa kwa nini mko kimya hata chadema pale inapo haribu

Mimi siwezi kuwa mwanachama wa chama cha akina Nkya:biggrin1: na wenzake.
 
Akili zingine za kuazimwa,katumwa aseme na kule anakounga mkono au ana ndugu kaguswa jana kule?
 
Watanzania wengi ni wanafki!Ukiwa mkali shida,ukicheka cheka kama jamaa yetu yule wa Chalinze shida.
 
Go to hell! Ulitaka waitane wapi wakati pesa zinazoliwa ni zetu.wacha awashtukize, awaaibishe na awadhalilishe Mbele yetu, afterall wao ndio wanufaika wa madudu wanayofanya. Hapa kazi tu!
 
Wanacho kifanya watumisha wa TPA ndio haki,good governance na wala hawamdhalilishi mtu??pathetic mitanzania ndivyotulivyo.
 
Good governance? Not now Pasco! Njia pekee ya kuvunja mazoea yaliyoifikisha nchi hapa ndo hii ya Tit for Tat. Na nzuri zaidi, kila kinachofanywa na PM kinakuwa na ushahidi wote. Hivi sisi watanzania tumerogwa?

Haya maamuzi lazima yawe public ili na wengine wasikie na wajifunze. Kwa hiyo ushiriki wa media ni muhimu sana. Pasco najua wewe ni mwanahabari, hivi hautambui kuwa media ni muhimili unaosaidia mihimili ya serikali? Kwa post yako hii inaonyesha umeguswa sehemu mbaya, lazima povu likutoke!

You cant fight, just join.......
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco
Mimi nakubaliana na wewe alimia 100 Kwa macho ya haraka wananchi wanapenda na kushangilia sana hivyo. Na kwakuwa ndio wameanza kazi wanatafuta kuteka saikolojia ya wananchi kuwa wao ni wakali sana na aliyekuwepo alikuwa zoba. Katika hali ya kawaida yale yote yalikuwa ni kuyazungumza ofisini halafu taarifa inatolewa kwa waandishi wa habari kupitia wasemaji husika. Tabia hizi ndio zimeanza kuigwa hata na viongozi wa chini kama kina Makonda kuwaweka watu ndani kinyume cha taratibu za kazi eti kisa wamechelewa. Wakiambiwa sheria haisemi hivyo wanasema wanakwenda na kasi ya Magufuli. Katika hali ya kawaida huwezi kujibu mambo ya kitaalamu hasa yanayohusu takwimu abraptili. Hata Magufuli ukiona anataja takwimu mbali mbali ujue amekariri kabla na jambo ambalo hajakariri au hana uelewa utamuona anavyobabaika kama alivyosema wananchi wa Libya walimuua Sadam na baadaye akasema sio huyo ila huyo ni wa Kuwait. Hivi ikitokea wameenda na matakwimu yao hadharani halafu ikagundulika ni ya uongo ha watendaji wakawajibu hadhaarani kuwa sio kweli hizo ni feki watajisikiaje. Ivumayo haidumu! Soon tutaanza kushuhudia kama yale ya JK kwani naye alianza hivi hivi, mara sokoni Tandale, mara Muhimbili, mara semina elekezi Ngurdoto... baadaye ikawa kimya!!! Ukweli ni kuwa kiofisi hutakiwi kumuonesha mtu aliyechini yako kuwa amekosa hadharani. Kwamfano yule wa TRL baadaye akipata jibu kuwa walikopa kwa maelekezo na idhini ya serkali chini ya waziri fulani alikuwa mpiga debe mkuu wa Magufuli au rais aliyepita watafanyaje? Tabia hii hata rais anayo sana lakini kuna siku watachomekewa takwimu feki halafu wakakutana na kipanga atawachana hadharani wabaki na aibu! Tena yule jamaa wa bandari alikuwa mmngwana sana akamwambia hayo watayazungumza kiofisi si ajabu alishagundua tatizo. Sasa waende wakashitukize hata nyumba za serikali kuona kama waliouziwa ndio waliostahili na nani alishiriki uovu huo halafu yaoneshwe hadharani tumjue hata aliyeuza kwa ndugu na hawara!
 
Kuwakamata wezi wa EPA tu alisema wanaweza kuangusha Serikali maana wana nguvu sana, sasa huu mziki atauweza kivipi?
 
kwan angeulizwa na akawa na majibu sahh na ya mh majaliwa kungekua na shida tatzo ni kwamba mnataka akatafute uongo wake kwa muda wake.... ni sawa urud nyumbna umuulize dada mtoto anaendleaje anakujibu vzur kumbe una taarifa fika kuwa mtoto aligongwa na baskel mchana
 
Mparaganyiko mkubwa
kaenda kwanza kagundua makontena 300
karudi tena kagundua mengine zaidi ya 2000

so inawezekana yakafika hata elfu 10 hajagundua bado
na hakuna namna ya kugundua hadi waziri mkuu aende mwenyewe..
ni kama system ime fail kabisa....waziri mkuu anafanya ukaguzi wa kontena
sio kujenga system mpya yasitokee haya tena

Ndugu naona unatupa lawama pekee kwa hii serikali bila kusema badala yake ilitakiwa kufanya nini kwa ilichokikuta kinaendelea kwenye bandari. Ok let's say wamesuka mfumo mpya wa kuiendesha bandari na kuisimamia kwenye mapato ila bado wanasubiri sheria maybe ipitishwe na bunge au vipi labda. Je wakati wanashughulikia uundwaji wa huo mfumo, ilitakiwa waache hizo pesa zinazopotea ziendelee kupotea mpaka huo mfumo uwe tayari ? Ilitakiwa waache kilichokuwa kinafanyika kiendelee au mimi ndio siwaelewi nyie mnaokosoa kila atachofanya?
 
Wale ni wezi wa mali za uma..
Unataka utawala bora vipi sasa..
Mwizi ni mwizi tu..

Wale sio wazembe ni wezi wanashirikiana na wafanya biashara..
 
Napenda pale rais anaposema "hii ni serikali ya John Pombe Magufuli.."
Mambo ya ekotite..,kuunda tume,kulindana nk. Yameligharimu taifa...
TPA,TRA nk yafaa PM aweke ofisi ya muda.
 
UTAWALA BORA peleka kwa MKEO, wameshatunyonya vya kutosha HAPA KAZI TU!
 
Sometimes good dictatorship is better than bad democracy.hiyo mambo ya kuitana sijui chamber sijui nini hayapo tena....sometimes huwa nashindwa kuelewa wanachokitaka chadema maaana wako kila kitu ni kupinga tu.
 
Back
Top Bottom