Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Negative!

I don't spend a lot of energy criticizing anybody.

And trust me, I am a very high energy guy.

Mkuu ,I am a very high energy guy ndo nn?next time sema hivi:I am very energetic guy,
 
Hayo ni maoni ni kwanini unataka uyalazimishe kqwa WatanZania wote? Hayo ya utawala bora ni kulingana na tafsiri yako wewe na jinsi unavyoongoza familia nyumbani kwako usitake kutuletea kwenye nchi yetu, tumeshatoka huko, tumeshayafanya yote hayo ya kuitana faragha, kuundiana tume, kuonyana kwamba ninawajua wala rushwa msipojirekebisha mtakona cha mtema kuni kote huko tumepita lkn matokeo yake nikwamba makontena zaidi ya 2500 hayajalipiwa kodi, yaani yamekombolewa Bandarini bila kulipiwa sasa huu ni uhujumu Uchumi na kwa nchi nyingine adhabu yake ni sawa na Uhaini kwani unalinganishwa na uuwaji watu wote waliofia mapokezi kwa kukosa dawa hospitalini wameuliwa na hawa wezi!

Hivyo tuache na Magufuli wetu tumeshamkubali jinsi alivyo na vyovyote anavyofanya ana baraka zetu, na ndio maana ya kushinda Uchaguzi na kuwa Raisi vinginevyo basi kila mtu angejiongoza?

majina ya wala rushwa ninayo

majina ya wauza madawa ninayo

tunawajua walioficha hela nje

tunajua........il

kabisa mkuu tushatoka huko!!
 
Ee Mungu naomba waendelee kudhalilika,kunyanyasika,kuaibika,kuumbuka nk,maana watanzania wengi tushapitia hayo kwa sababu ya mijitu kama hiyo! tazama wajawazito wanaojifungulia chini,watoto wanaokaa chini kwa kukosa madawati,wagonjwa wanaokaa mahospitalini zaidi ya mwenzi kwa kukosa vipimo na mengine mengi,je haku sio kudhalilishwa!?
 
Mleta uzi wewe ni mjinga wa mwisho chini ya jua, ninyi ndio wale mlokua mmegeuza ofisi za umma kama za wazazi wenu , kosa la waziri hapo ni nini? anamdhalilisha nn elihal kawauliza kitu kilcho ndan ya kaz zao? mda wa kubembelezana umekwisha sasa na hapa kila mmoja atawajibika, for your information, many more are coming..

Mkurugenz anaulizwa pesa mlizokopa TIB mtazilipaje elhal mmejilipia mishahara badala ya kupeleka kwenye uzalishaji ambao ndio base point ya mkopo, lizee latoa mimacho tu, nashangaa kwann yule mze hakufukuzwa pale pale..

Less n weak minded people are no longer needed in this country!!!!!
 
Napenda pale rais anaposema "hii ni serikali ya John Pombe Magufuli.."
Mambo ya ekotite..,kuunda tume,kulindana nk. Yameligharimu taifa...
TPA,TRA nk yafaa PM aweke ofisi ya muda.
hata mimi naipenda sana hiyo kauli maana angesema hii ni serikali ya sisiemu angeboa
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Maisha ya kimazoea ndio yanayofanya uandike hv bwana Pasco.Ss ni wapinzani lkn mtu akideal na uozo fulani ambao uko dhahiri tunasifu au tunabeza?Kwa hiyo ww ulitaka waachiwe tu waendelee na wizi,Sijui labla ndio athari za kuzoea dhambi na kufa kwa dhamiri.
 
Ha ha ha,watu mnafurahisha ..........

Wao waendelee kuisoma tu,maana hakuna namna nyingine.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco
Tulipofika kwasasa tunahitaji uongozi wa aina ya pm anavyofanya kwakuwa hiyo good governance tulishindwa tukabaki na michakato na naona tunahitaji wawe madictator kwa muda hadi tutakaponyooka ndipo turudi kwenye hiyo good governance uisemayo.
 
Ni mapema sana kusema sana. Uongozi wa kuteuliwa ni kazi nzito sana, ipo siku tunaweza tena kuja hapa hapa na kusema bora Pinda au bora Kikwete, kipya kinyemi ingawa kidonda, Changamoto za serikali mpya zinakuja, na hapo Majariwa atapimwa vizuri zaidi. This is worldwide, hata Obama at First alionekana like African Messiah ila baada ya muda kiasi akapwaya sana.
Let wait and give time.
 
Kwanini unaamini asingeweza?
Boss wake ndio alikua tatizo.
 
Mtoto wa mkulima kamati ya maadili ya ccm ilishasema hana maadili sasa angewezaje kukemea haya!
 
Kwani mkuu si majuzi alienda na akawaambia wajirekebishe wenyewe kabla hajarudi tena hapo?? Na aliwaambia kabisa kwamba atarudi.. Kwanini wao hawakuanza take measures??

Cha kushangaza leo ameenda amekuta hakuna kilichofanyika, sasa ulitaka afanyaje?? Tena amekuta ule ujinga ambao ICT wanaofanya bado walikuwa wanaendelea.. Hakuna namna wacha wahaibishwe tu..

Uwezo wa wafanyakazi wa serikali in ICT ni mdogo sana. Lazima tunaibiwa sana kwa jina la ICT. Lazima tunauziwa programs ambazo ni substandard, mara nyingi kwa kutokujua ni program gani tunataka. Na kwa jinsi tulivyozoea ujanja ujanja na udanganyifu, lazima ICT inatumika sana kuwezesha ukwepaji wa kodi. Kabla ya kuendelea kushangilia ICT kwenye mifumo ya ukusanyaji mapato ya serikali, forensic auditing inahitajika kwa mifumo ambayo inatumika tayari.

Cha kushangaza, eneo ambalo hajafika au sijasikia kama amefika pale bandarini ni la kupokea mafuta. Kuna ujinga mkubwa sana uliofanyika kwa miaka mingi wa ku-temper na vifaa vya kupimia shehena ya mafuta inayoingia nchini "flow meters". Bila "flow meters" inayofanya kazi na ambayo haijachakachuliwa, serikali haiwezi kujua kiwango sahihi cha kodi inachostahili.
 
Pinda alikuwa anamsikilaza bosi wake gu..wizi wote umecanyika chini yao...ahhhh
 
Pasco kama hutaki hama nchi na kama una ndugu yako mwambie kama ana hofu aache kazi kabisa..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom