Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Hata mimi nilikuwa najiuliza...hivi ni kipi tulichokuwa hatukijui ambacho wao wamekifunua?

Sijapata jibu.
Kabisa unamaanisha unachokiongea? Anyway
1.Ulikuwa unajua kuna makontena 300 yamepotea,najua hujui hadi PM alipotimba bandari
2.Najua ulishakariri makontena yaliyopotea bandari ni 300,yet again PM akarudi akagundua mengine 2000 yamepotea,ulilijua hili
3.Swali la msingi kwa nini upotevu huu tuujue hadi pale anapotembelea PM?
OK kama ulivouliza nini Kifanye
Very simple hakikisha kila contena linalofika bandari ya Dar linalipiwa kodi na inaingia moja kwa moja serikalini.
Unajua bado siamini kama unasema hujui nini kifanyike.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.

Pasco

kwa nini wasiwe wakweli kama hawahusiki? muda mwingine kumvua nguo mtu ni onyo kwa wengne kuwa wakweli na waaminifu. anachotaka ni kuwa mkweli, maana taarifa hizo wanazo.

anashindwa nn kusema kontena kadhaa hazikulipa kodi tangu siku fulani, aliyesababisha ni fulani, na tumechukua hatua hizi?

pm majaliwa, shitukiza na kwa Pasco, maana huenda ana magumashi mengi
 
Bwana Pasco, ulishaambiwa kuna kazi ya kutumbua majipu na huwa yanauma sasa unashangaa nini?

miaka nenda rudi tunajadiri wizi mkubwa bandarini na TRA mpaka watu wananukuu maelezo ya Kagame juu ya ujinga wa wantanzania. sasa mbona viongozi wanajaribu kusaidia kubadilisha hali hiyo mnawakejeli?

kupambana na wizi siyo kazi ndogo na ukisema uishie kwenye mazungumzo tu ndiyo kwanza utazungukwa na kuendelea kuibiwa. Watanzania tumepoteza maadili, tunaibiana mchana kweupe, huu utaratibu wa kuviziana ndiyo muafaka kwa sasa
 
Watz wanapenda rongo rongo. Hiyo ya majaliwa nimsg tosha kwa wazembe. Bana juu chini watabanana wenyewe.
 
'Good governance' ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Mkurugenzi TRL hajui hata kama waliwahi kukopa
3Bn/-? Zilitumikaje? Anabaki kuwa na kigugumizi tu.
Lakini pia hawa jamaa huwezi kuwaondoa kwa 'good governance', inabidi uwavunjie heshima kwa wananchi kwanza ili upate uhalali wa kuwatoa.. 'if they bend the official procedures, you bend the morality too'..
Mwache PM afanye awezalo akizidi JPM atamshika shati tu..
 
Mkuu Pasco,

Watu bado wanaendelea na mfumo uleule wa kushabikia bila kujua kama tumefanikiwa kulenga tatizo au la.

Kwa mfano huyo meneja wa bandari hakupewa nafasi muafaka ya kuelezea yaliyotokea kiutendaji.

Kama kingekuwa kikao cha ndani angepata majibu muafaka zaidi. Lazima mtu apewe muda wa kuweza kuja na majibu yanayojibu swali.

Huyu ndugu wa bandari amechukua nafasi hiyo muda mfupi tu uliopita. Sawa yeye ndio mkuu, ili aweze kujibu kwa mambo yaliyofanywa na watangulizi wake anahitaji muda.

Tutaumiza watu wadogo wadogo, wakati mambo haya , haiingii akilini yangeweza kufanya bila utawala wa juu kabisa kujua .

Kila bandari na ICD kuna watu wa usalama wa Taifa , je hawa nao kuna hatuna gani imechukuliwa dhidi yao? Mojawapo ya majukumu yao ni kulinda maslahi ya Taifa.

Kweli makontena 2431 + 349 yanaweza kutoka bandarini bila vyombo vyote vya nchi kujua ?

Au ndio yaleyale ya kuchukua hela za escrow kuchukuliwa na sandarusi bila hata watajwa kusemwa?

Huo wizi ulikuwa ni mkubwa na mfumo wa kutoa makontena hayo unaonekana ulikuwapo na swali la kujiuliza ni kwanini mambo haya yamefanyika kipindi hiki tu?

Taarifa zimepatikana jana ?
 
Kwa nini waliondoa like.
Nimependa comment yako mkuu
acha muisome namba mlidhani UKAWA wataisoma kumbe ni ninyi wenyewe....mi naona yupo right sometimes dictatorship is a good government....nimemaliza sio kama mkwere anachekacheka tuuu
 
pumbavu mkubwa ww mtoa uzi-huo utawala bora alioufanya kikwete umetufikisha wapi? au utawala bora ni watu kukwepa kodi? kuiba dawa za serikali? kununua mabehewa mabovu? au na ww unahusika na huu ujinga? twende kazi MAJALIWA.
 
unataka kuleta ustaarabu kwenye wizi? ungekua na akili ungeleta thread ya kuuliza polis wanavowafanyaga wamachinga wakiwa kwenye maeneno yasioyowahusu kama ni good gorvernance, acha unafiki Pasco
 
Last edited by a moderator:
Pasco, ukweli ni kwamba upepo unapuliza na sasa 'yeti za kuku' zinaanza kuonekana. Tawkimu zinaanza kuonyesha kuwa taifa letu lilikuwa linaeleka sipo
 
Nimeshindwa kukujibu maana umeniti ahasira sana, wafanyakazi wa nyumbani wanajittuma kwa moto kutusaidia ndio maana huwez kuwagombeza mbele za watoto , lakini hii mijizi inayojenga nyumba 100 na kuficha hela nje, inayotumbua kodi zetu na kusababishha huduma mbovu za jamii ....hii mijipu MHESHIMIWA ATAKOSEA SANA KAMA ATAONGEA NA HIYO MIJIZI PEMBENI...MAADAMU ILIKUWA IMESHAJUA KWAMBA MAGUFULI ANAKUJA NA HAIKUJIPANGA KUFANYA KAZI IUIMBUIWE TUUUUU...MCHANA KWEUPEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Ukitaka kumuua nyani usimtizame usoni.
Mimi sioni tatizo kabisa hapo,wakiitana chemba watu hawakawii kuzua jambo,acha kila kitu kifanyike hadharani kila mtu ajionee madudu.

Kwanza sioni haja yakuwaheshimu maofisa walioisababishia nchi hasara kubwa namna hiyo,waheshimiwe kwa lipi haswa hadi waitwe chemba??!!
Nchi hii ilipofikia hii style ya kushitukizia,kuvizia na kuaibisha viongozi waliofikisha taifa hapa lilipo ndio nzuri na inayofaa.

Mkuu Pasco huo mfano wa mama kutofekea ma tx nyumbani kwenu na wa Pm kuhoji hadharani mambo yaliyotia taifa hasara hata haiendani.

Kwanza natamani Magufuli na MP wageuke wakoloni,ukikutwa na uzembe uliolisababishia taifa zaidi ya milioni kumi unalambwa viboko hadharani ndio taratibu nyengine za kukuachisha kazi na kukutaifishia mali zako na n.k ndio zifuate.
Go Mr PM Go, we like your style
 
we PASCO usituchanganye hapa nini maana ya uwajibikaji kulingana na majukukmu ya kiongozi husika au unataka na MAJALIW alie kama PINDA mwache PM apige kazi . kama umetumwa na hiyo mijizi tafadhali sana achana na MAJALIWA mwache awatumikie Watz.
 
Asipofanya hivyo atapigwa kisomo ili ionekane kila kitu kipo sawa, Huo ndio mfumo wa kwetu, ukitaka demokrasia na haki za binadam, hata hao wamagharibi linapokuja suala la kujineemesha huziweka pembeni na hufata maslahi yao. Hongerereni wakuu wa nchi. Tunakuombeeni Mungu akupeni nguvu zaidi, na hekima za kutumbua majipu.
 
wewe mtoa post akili huna. good governance iko pande zote. huyo msimamizi wa hivyo vitengo walitakiwa kumpa taarifa kamili bos wao majaliwa uone kama angewaumbua but walikuwa wandanganya kwa kudhani hani taarifa kamili. shame on u.
 
Pasco

Una akili za kutosha kuchambua mambo lakini katika hili unataka kutujaza upumbavu. Bade alipoulizwa kama kuna makontena yaliyotoka bandarini bila kulipiwa kodi alikubali na hata akawa anaeleza ukaguzi walioufanya kwenye bandari ya nchi kavu. Alipoulizwa kama anawafahamu wahusika alianza kujikanyaga kwamba mpaka apewe na walio chini yake.

Hiyo misingi ya "utawala bora" wa nchi inayopoteza mapato kwa namna na kiasi hicho halafu tunacheka na tunataka watu waitane ofisini wazungumze nini?tuna akili kweli? Hayo ya kuzungumza ofisini yalifanyika huko nyuma na ndiyo maana nchi imefika hapa tulipo.kwanini tusijaribu na njia nyingine?
 
Hakuna good governance ya kuficha ujinga. Huwez kua CEO ambaye hujui shirika lako.
 
Back
Top Bottom