Anachokifanya polepole ni kuvivua nguo vyombo vya ulinzi na usalama TZ siyo CÇM hata Raisi hayupo salama chini ya wanamtandao.

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
9,205
Reaction score
22,219
GT
Ukifuatilia kwa umakini madai ya polepole tatizo utagundua ni wanausalama wetu siyo CCM. Vyombo vyetu vipo corrupted na wanasiasa kiasi kwamba hawaoni mambo yenye kuhatarisha usalama na maendeleo ya nchi.

Tujiulize.
1. Mpaka mkataba wa Bandari unasainiwa kinyemela walikuwa wapi.

2. Mtu anasema raisi atauwawa na akafa kweli it is shocking.

3. Wanamtandao kuamua nani awe rais wa nchi rejea mwinyi kule Zanzibar etc, taifa limetekwa hili

4. Rostam kuwa na hatimiliki ya TZ it is crazy.

5.Deni mpaka linafika 107TR kiholela where are they?

6.Kesi ya Lissu upuuzi mtupu

7. Hili la NIDA, NEC na CCM ndiyo kiboko.

9. Katiba ya warioba licha ya kutumia pesa nyingi za serikali iko wapi mpaka sasa?

10. Mgawanyiko na Raia kukosa uzalendo kwa nchi wamelala tu wanakunywa mvinyo.

11. Hao waarabu wanaouziwa.mbuga zetu kiholela what for?

12. Samia kuendelea kuwa raisi hadi 2030 pathetic.

13. Utoroshwaji wa madini na rasilimali zingine kama wanyama, it is painful.

In short wanausalama wetu wamegeuka.kuwa politicians wanakula hela na kulala hawalisaidii Taifa kabisa wanakazi moja tu kukimbizana na chadema ndo uwezo wao unapoishia.
 
Anayoyasema Polepole yanatia hasira sana, na kwakuwa hakuna aliyejitokeza kufafanua au kupinga kwa hoja, kwa asilimia kubwa inathibitisha ni ukweli mtupu.

Nawashangaa sana wanaotaka tumpuuze Polepole, yani leo hii Nape au Kinana wajitokeze waombe msamaha na waseme vile walivyoshinda chaguzi kwa mbinu chafu halafu tuwapuuze na tuwaamini akina Lucas mwashamba kweli? Tutakuwa mapunguani.
​
 
Tunaendekeza sana umasikini au njaa zetu, kiasi kwamba hata taifa letu, hatulithamini. Angalau kungekuwa na idara Fulani inayosimamia Katiba na sheria au taratibu tulizojiwekea, ila zote zinajilinda, kibarua kisiote nyasi, ilhali nchi inaachwa mkiwa, bila anayeilinda.
 
Mie nachoelewa nchi hii kama kuna kitu kinaitwa Usalama wa Taifa ni pale mtu anapoonekana kuitetea nchi yake dhidi ya hawa makaburu weusi ndo anakuwa tishio. Usalama uliopo Tanzania ni Usalama wa kulinda masrahi ya wezi wakubwa wakubwa badala ya kulinda Taifa na rasilimali zake, Taifa linaangamia na wao wakiwa wanachekelea
 
agree
 
Wanausalama ni chawa, vetting na recruiting kuanzia huko wanakowaokota these days(UVCCM) wanachokaririshwa ni kuwa akiwa bootleeaker wa kiongozi, mke wa kiongozi, mtoto wa kiongozi au mabepari kama Rostam Aziz wanaowamiliki viongozi ndiyo kuaminika na kupanda kwao vyeo. This whole ordeal is pathetically bad and it’s crushing the country into pieces.
 
Watu kama Warioba, Butiku, Polepole.. ni kati ya wazalendo wakweli wachache sana waliosalia. Inasikitisha kuwa Polepole analazimika kuzungumzia mafichoni ili wahuni walioteka nchi wasi-Mdude.

Gwajima anafungiwa makanisa zaidi ya 2000 kwa "kosa" la kakemea na kupinga utekaji wa watu. Yaani wahuni na watetezi wao wanaona utekaji na mauaji ni jambo zuri
 
Umemwaga madini lakini kichwa cha habari hakipigi kwenye mshono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…