"Mama aliupiga mwingi" toka mwanzo na sasa tunaona unavyoendelea kuwa "mwingi"
Nami ningependa kujua yule binti DC aliishia wapi?
Huenda tukijua alipo sasa tunaweza kuanza kujenga hoja juu ya hii mada.
Mkuu 'Escrowseall', nikushukuru kwa kumbukumbu zako hizi. Mimi nilianza kulishangaa hili jambo lilivyochukuliwa toka mwanzo, na kama kawaida ya waTanzania, hakuna alieshtuka, na sasa wala hakuna anayekumbuka kama swala hilo liliwahi kutokea na kunyamaziwa kabisa.
Na pengine hadi leo mradi huo unafanya kazi kama kawaida, maanake hatukuona mabomba yaking'olewa!
Pengine huu ulikuwa ni mradi wa mama mwenyewe, maana alivyolichukua inashangaza sana.
Na haya mahela tunayowapigia kelele akina Mwigulu, si nawe ulisikia "STUPID"?
Hizi ndiyo njia mpya za kushughulikia haya maswala ya uhujumu. Sema neno moja ukionyesha hasira, halafu nyamaza, acha waTanzania wasahau. Ikifika 2025, hakuna atakayekumbuka chochote, hadithi ni za kupamba tu, kama tunavyoona sasa mabango kila sehemu za miji.
Nchi ya ajabu sana hii.