Anafanya kazi kiwandani ameshajiwekea msingi wa umasikini milele

Anafanya kazi kiwandani ameshajiwekea msingi wa umasikini milele

Unalimaje bila mtaji na mtaji utaupata vipi bila kufanya vibarua.

Hivi wazee haya maoni mnayotoa ni kwa ajili ya Tanzania ama wenzetu mpo mambele
Wewe Kuna watu wapo miaka 5 kiwandani na hawana maendeleo yeyote zaidi ya nguo na kula na godoro lake la kulalia yaani kama akipata hata shida kidogo tu hata ya laki 1 mfukoni hana yaani kiufupi kashalizika kudhalilishwa
 
Kuna viwanda vipo huko kibaha watu wanalambwa viboko wakizingua yaani jitu jeusi tena dume zima lipo kwenye ardhi yake ya taifa lake linalala kabisa halafu mjinga mmoja kutoka china analipiga bakora aisee vitu hivi vinahudhunisha na kuchekesha Kwa wakati mmoja hii sio kazi Bali ni msingi wa umasikini
Duh,
Hapo ndipo ccm wamelifikisha taifa.
Inasikitisha sana
Tlaatlaah
 
Usimcheke muhurumie,unajua umasikini ni circumstances,na si kitu kinachoondoka mara moja kwa kutumia pesa tu,hapana
Thus why Kuna watu hata uwape bilioni ,wataishia kununua madela tu.
Kipindi wewe unaagiza Prado la mwaka 2008 na kuonekana kibosile,hio Gari huwezi ingiza Algeria tu hapo acha Europe,.........ila huku wewe ni tajiri mkubwa sana
Inahitaji malezi,exposure,elimu,tabia na makuzi kuundoa umasikini,...thus why kwenye hizo kazi hutawaona waarabu,wapemba Wala wazanzibar.....huko utakutana na wadau kutoka Simiyu,Katavi,Kyela😁😆 huko na wanaona kwao wameyapatia maisha
Aisee ni shida
 
Duh! Bro,sijui ni serikali haijali,au ni watu wenyewe hawajitambui. Kufanya kazi kwa wale watu,kunahitaji kujenga ujinga kiasi furani. Manyanyaso na mishahara yao,bora ukalime mboga mboga au uajiliwe sehemu nyingine. Sema tu utakuta watu wengine wanafata mkumbo,kwamba kuna chama cha wafanyakazi kitawatetea,na mambo mengine. Ile kazi huwezi kuendelea. Mshahara wenyewe utatoa,madeni yanazidi mshahara. Kulipwa, wengine atakupa nusu nusu mpaka iishe,kila baada ya wiki. Pesa isiyokuwa na msaada wowote. Sema tu ngozi nyeusi wenyewe hatupendani, kuna watu wengi wana fursa za maisha, lakini hawawastui wenzao.
Wakistuliwa wanawaibia ,watu hawako committed kufanya kazi Bali kuiba ,yaani imekuwa ni fasheni ukikaa mahala usipoiba unaonekana mjinga na usiyejitambua kabisa.
Watu wanapenda visivyotoa jasho Wala kuumiza kichwa acha waendelee kubeti mafuta ya upako wajipake
 
Hamna Cha kujaaliwa Wala nini wote tunajua life ni mapambano Sasa mtu anaruhusu kudhalilishwa na wajinga Fulani kutoka china kisa elfu 5 huyo mtu kwenye maisha yake haji kutoboa zaidi atakua anatafuta hela ya kula
Ndio anatafuta hela ya kula na possible anatafuta ili watu aliowaacha kwake wapate chakula....
 
Wewe Kuna watu wapo miaka 5 kiwandani na hawana maendeleo yeyote zaidi ya nguo na kula na godoro lake la kulalia yaani kama akipata hata shida kidogo tu hata ya laki 1 mfukoni hana yaani kiufupi kashalizika kudhalilishwa

Wewe Kuna watu wapo miaka 5 kiwandani na hawana maendeleo yeyote zaidi ya nguo na kula na godoro lake la kulalia yaani kama akipata hata shida kidogo tu hata ya laki 1 mfukoni hana yaani kiufupi kashalizika kudhalilishwa
Una umri gani?
 
Ndio anatafuta hela ya kula na possible anatafuta ili watu aliowaacha kwake wapate chakula....
Hiyo ni ya kula yeye ukiona mtu anatafuta elfu 5 Kwa maisha haya na anafamilia basi anatesa watoto wanapitia uchungu wa Hali ya juu kwasababu ya ujinga wake
 
Tatizo la kwanza ni wananchi wenyewe hawajitambui, cha pili ni Serikali kushindwa kuweka Sheria rafiki kwa wafanyakazi wa Nchi yake.

Marekani na baadhi ya nchi za ulaya wafanyakazi wa ndani(mabeki tatu) wana mikataba na kiwango cha kuwalipa kimewekwa kabisa ukikiuka jela inakuhusu pamoja na faini juu,

Ila nchi zetu hizi wafanyakazi sheria haziwalindi zinawalinda zaidi maboss na hata hizo chache nazo zinazowalinda waajiriwa bado zinapotoshwa kwasabab ya rushwa na uonevu,

Kiufupi Tanzania ni Nchi mfano wa jalala la Takataka ukifukua hukosi mavi.
mkuu utatekwa ww huruhusiwi kukosoa unatakiwa upongeze tu. futa hii kwa usalama wako
 
Wapo wengi mno, wanaaihidiwa ajira miaka na miaka na hawapewi, nafasi zikija wanapewa watu wengine hasa serikalini 🤣
Ndio wajinga wenyewe Sasa hao yaani unafanya kazi ya kujitolea kisa umeahidiwa kazi akili Gani hii je usipopewa hiyo kazi inamaana utakua umepoteza mda wako bure
 
Hawa vijana wetu wanaohitimu ngazi mbalimbali za elimu wasiwe wavivu wa kuanzisha shughuli zao binafsi kupata hela. Kama msetifiketi unaona haukupatii ajira staha weka sandukuni ingia mitaani fanya kitu halali cha kukupatia fedha au nenda shambani kalime na ufuge. Hii ya kukimbilia vibarua huko ni kwenda kurutubisha umasikini wa kujitakia
Huu ndio UKWEL mchungu.
 
Sasa vyeti tunavyo huo mtaji tunatia wapi
 
Back
Top Bottom