Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Technolojia hii ni nzuri ila mimi binafsi sijaipenda sababu inaondoa ubinadamu kidogo, ila ya kupandikiza kwa mwanamke kuna ubinadamu kwa kiumbe atakae zaliwa.
Huo ni mtazamo wangu
Nafikiri kama ni upande wa Imani zaidi hata mimi naona wamefika mbali kwa kweli
Unakumbuka hata zamani walipotengeneza clone ya kondoo
Waingereza walikataa kabisa kufanya hayo wakiwa upande wa dini zaidi na uumbaji

Kweli inatisha ila ndio hivyo tena
Imagine wanafyatua watoto kama wanatengeneza toys
 
Nafikiri kama ni upande wa Imani zaidi hata mimi naona wamefika mbali kwa kweli
Unakumbuka hata zamani walipotengeneza clone ya kondoo
Waingereza walikataa kabisa kufanya hayo wakiwa upande wa dini zaidi na uumbaji

Kweli inatisha ila ndio hivyo tena
Imagine wanafyatua watoto kama wanatengeneza toys
Na tunakoelekea watakuwa na uwezo wa kuedit genes za watoto,
Kwahyo wanaweza kumpa mtoto traits za akili nyingi, Nguvu nyingi, athleticsm etc. Etc.

Inawezekana mbeleni watoto wa hivi wakawa dili kuliko wa kawaida.
Mzazi anaenda na xstics za mtoto anayetaka, aweje...Awe handsome kama Idris Elba au awe na kipaji kama Messi.

Tena unakuta genes za hao watu amarufu tayari zipo, mzazi unafika unachagua tu traits unazotaka
 
Ukiangalia trend ya utoaji Mimba jinsi ilivyo je ninani atakataa mil 57 kwa wadada wa Tz wanaoishi kwa kujiuza
 
IVF kirefu chake ni In Vitro Fertilization.
IVF ni jambo la kurutubisha kwa kuunganisha mbegu za uzazi za mwanamme na yai la uzazi la mwanamke maabara, baada ya hapo zoezi linalofatia ni kupandikiza ujauzito kwa mwanamke kwa njia ya sindano kisha ujauzito utaendelea kukua kama kawaida kwa mda wa miezi tisa kisha mwanamke atajifungua kawaida.

IVF haihusishi kukutana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume bali mwanaume anatoa mbegu kwa kujichua au punyeto na mwanamke anatolewa yai lililopevuka maabara na wataalamu baada ya hapo ndio ujauzito unapandikizwa kwa mwanamke,
Ni njia safi na salama na haihusishi operation kubwa na haina hatari yeyote kwa mwanamke.

Sasa anahitajika mwanamke au msichana katika zoezi hilo,

MALIPO
Moja malipo ni milioni 25 ambayo yatasainiwa kisheria mahakamani na ustawi wa jamii.
Pili kila mwezi atalipwa milioni moja kama malipo ya motisha kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito, malipo hayo ni nje ya ile milioni 25.
Tatu kila siku atalipwa elfu ishirini kama gharama ya chakula kulea mimba kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito.
Nne atalipwa shilingi elfu hamsini kila siku kama gharama ya chakula baada ya kujifungua kwa mda wa mwaka mmoja kipindi ananyonyesha.
Tano gharama zote za hospital kwa mama kipindi cha ujauzito, mama na mtoto baada ya kujifungua zitagharamiwa na baba wa mtoto/watoto

MASHARTI
Moja ujauzito utalelewa sehemu aliyopo baba wa watoto.
Mbili hauruhusiwi kisheria kutangaza kwa mtu yeyote kama una ujauzito labda wazazi wako tu, na wazazi wakiambiwa nao wataelimisha kuhusu hili sharti.
Tatu baada ya kujifungua, mtoto/watoto wakifikisha mwaka mmoja utawakabidhi kwa baba yao.
Nne baada ya kukabidhi mtoto/watoto hautoruhusiwa kisheria na kibinadam wewe ndugu zako au rafiki zako kuwaona mtoto/watoto kwa namna yeyote kipindi chote cha maisha yenu hapa duniani.
Tano hautoruhusiwa kuwa na mahusiano ya aina yoyote na baba wa watoto kabla na baada ya kujifungua mtoto/watoto.
Sita awe tayari kulea ujauzito akiwa jijini dar es salaam.

SIFA ZA MWANAMKE/MSICHANA ANAEHITAJIKA.
Moja awe na afya nzuri, asiwe na magonjwa ya akili, pili asiwe na magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.
Pili awe mtanzania kutoka kabila na dini yeyote.
Tatu awe mrefu, mrefu sana atapewa upendeleo.
Nne awe mwembamba, akiwa mnene isiwe unene mkubwa sana.
Tano awe na umri wa kati ya miaka 25 hadi 35.
Sita awe mweupe au maji ya kunde asiwe mweusi sana.

Asanteni.
Pia kwa mwana Jamii Forum mwenye ndugu, rafiki au jirani mwenye hizo sifa naomba mnisaidie kusambaza hili tangazo.
Asante tena.

Vigezo na masharti kuzingatiwa
Surrogacy haikubaliwi kwa msichana! Lazima awe ashazaa angalau mara moja mkuu
 
Sina hakika wawe 100% sawa, unaona yale mayai ya kisasa? Tunayala lkn wakati wa kuyavunja yana shombo moja balaa, hata ukivunja kwenye chombo cha plastic unatamani hata ukitupe
[emoji38] [emoji23]
Kwa hiyo watakuwa kama kuku wa kizungu hata kukimbia hawawezi daa

Kwa kweli wengine tuna hofu sana ila wao wanajitahidi kuvumbua kila kitu hata kama wanafeli ila hawaonyeshi mpaka wwfanikiwe ndio tunajulishwa

Utakuta yalitoka mazombie kwanza
 
[emoji38] [emoji23]
Kwa hiyo watakuwa kama kuku wa kizungu hata kukimbia hawawezi daa

Kwa kweli wengine tuna hofu sana ila wao wanajitahidi kuvumbua kila kitu hata kama wanafeli ila hawaonyeshi mpaka wwfanikiwe ndio tunajulishwa

Utakuta yalitoka mazombie kwanza
Sijui waliyatestia wapi maana mh ni kizunguzungu ukijua umetotolewa🤣🤣🤣🤣
 
Kwani hata akitumia langu lazima litolewe nje liwe fertilized ndo wapandikize.
Me na offer kumbeba tumboni for 9months na kumtoa kumleta duniani
Tatizo mnacheza na hivi vitu! Kwa kawaida i natakiwa aliyebeba kiumbe tumboni aka jifungua asione huyo mtoto. Na ndiyo maana kuzaa kwake ni lazima operation
 
Back
Top Bottom