Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Hili wazo jipya ndugu, nimetafakari sana na kufurahi kwa ujasiri wako.
Ila kwa kifupi haitowezekana kwa sababu tayari mtoto atakua damu yangu hivyo inaweza kuleta sintofahamu baada ya miaka.
Ninaweza kukupa wazo kwamba kama una sifa nilizotaja, fanya kwanza mpango wangu halafu badae mimi nitakusaidia kulipia gharama kufanya IVF kupata watoto wewe na mbegu za mtu mwigine.
Aseee [emoji848][emoji848]

We nadhani uko kwenye strategies zako kinda like unaifanyia promo IVF

I'm convinced there's something fishy going on[emoji21][emoji21]
 
Basi ww utakuwa dalali,kama huelewi hata ninacho kieleza.

Swali jepesi tu kwanini utumie ivf kupqta mtoto?
Sasa kama ana mke ambaye both tumbo la uzazi na ovaries zimeharibika. Afanye nini apate mtoto bila ya kutembea nje ya ndoa? Hujui hapa amemheshimisha sana mkewe?

Lakini kama situation ni hii, better option ni kwamba angemwomba shemeji yake wa kike a donate yai halafu apate surrogate mother abebe mimba. Mkewe angemtunza mtoto kwa mapenzi kama wake.
 
Sasa kama ana mke ambaye both tumbo la uzazi na ovaries zimeharibika. Afanye nini apate mtoto bila ya kutembea nje ya ndoa? Hujui hapa amemheshimisha sana mkewe?

Lakini kama situation ni hii, better option ni kwamba angemwomba shemeji yake wa kike a donate yai halafu apate surrogate mother abebe mimba. Mkewe angemtunza mtoto kwa mapenzi kama wake.
Nini maana ya kuwa na mke zaidi ya mmoja
My friend huyu jamaa mleta mada anakazwa don't loss your time kumtetea unatetea lipunga la town.
 
IVF kirefu chake ni In Vitro Fertilization.
IVF ni jambo la kurutubisha kwa kuunganisha mbegu za uzazi za mwanamme na yai la uzazi la mwanamke maabara, baada ya hapo zoezi linalofatia ni kupandikiza ujauzito kwa mwanamke kwa njia ya sindano kisha ujauzito utaendelea kukua kama kawaida kwa mda wa miezi tisa kisha mwanamke atajifungua kawaida.

IVF haihusishi kukutana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume bali mwanaume anatoa mbegu kwa kujichua au punyeto na mwanamke anatolewa yai lililopevuka maabara na wataalamu baada ya hapo ndio ujauzito unapandikizwa kwa mwanamke,
Ni njia safi na salama na haihusishi operation kubwa na haina hatari yeyote kwa mwanamke.

Sasa anahitajika mwanamke au msichana katika zoezi hilo,

MALIPO
Moja malipo ni milioni 25 ambayo yatasainiwa kisheria mahakamani na ustawi wa jamii.
Pili kila mwezi atalipwa milioni moja kama malipo ya motisha kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito, malipo hayo ni nje ya ile milioni 25.
Tatu kila siku atalipwa elfu ishirini kama gharama ya chakula kulea mimba kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito.
Nne atalipwa shilingi elfu hamsini kila siku kama gharama ya chakula baada ya kujifungua kwa mda wa mwaka mmoja kipindi ananyonyesha.
Tano gharama zote za hospital kwa mama kipindi cha ujauzito, mama na mtoto baada ya kujifungua zitagharamiwa na baba wa mtoto/watoto

MASHARTI
Moja ujauzito utalelewa sehemu aliyopo baba wa watoto.
Mbili hauruhusiwi kisheria kutangaza kwa mtu yeyote kama una ujauzito labda wazazi wako tu, na wazazi wakiambiwa nao wataelimisha kuhusu hili sharti.
Tatu baada ya kujifungua, mtoto/watoto wakifikisha mwaka mmoja utawakabidhi kwa baba yao.
Nne baada ya kukabidhi mtoto/watoto hautoruhusiwa kisheria na kibinadam wewe ndugu zako au rafiki zako kuwaona mtoto/watoto kwa namna yeyote kipindi chote cha maisha yenu hapa duniani.
Tano hautoruhusiwa kuwa na mahusiano ya aina yoyote na baba wa watoto kabla na baada ya kujifungua mtoto/watoto.
Sita awe tayari kulea ujauzito akiwa jijini dar es salaam.

SIFA ZA MWANAMKE/MSICHANA ANAEHITAJIKA.
Moja awe na afya nzuri, asiwe na magonjwa ya akili, pili asiwe na magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.
Pili awe mtanzania kutoka kabila na dini yeyote.
Tatu awe mrefu, mrefu sana atapewa upendeleo.
Nne awe mwembamba, akiwa mnene isiwe unene mkubwa sana.
Tano awe na umri wa kati ya miaka 25 hadi 35.
Sita awe mweupe au maji ya kunde asiwe mweusi sana.

Asanteni.
Pia kwa mwana Jamii Forum mwenye ndugu, rafiki au jirani mwenye hizo sifa naomba mnisaidie kusambaza hili tangazo.
Asante tena.

Vigezo na masharti kuzingatiwa
Naomba tuwasiliane kama bado hamjapata
 
Mimi mlongo honestly nimewazaa nimejikuta navaa viatu vyake nimetumia mnoooo...Lau ningeweza ningemzalia tu!!!inauma jamanii
Dunia ina mambo, mkumbuke kuna sacrifice,

Mwanaume akiwa na ndoa kama anataka mtoto atazaa nje na siyo kwa style hii.

Kuna kitu kimejificha hapo kwenye sadaka ya damu, ndio maana lazima mtoto awe damu yake otherwise wangekuwa wanateka Watoto hovyo mitaani, lakini kafara linataka mtoto wako.

Tafuta movie ya Nigeria Billionaires club utajionea kafara ya damu ya Watoto wachanga.
 
Umenichekesha sana, kwako itakua ngumu sababu ni damu yako lakini yai langu litakua rahisi kukuachia sababu...sio damu yangu au?

Haya siku ukiwa tayari utanicheki msimamo wangu utaendelea kua huo.
Hivi mnashindwa kuelewa kinachotafutwa hapo hasa ni nini?

Kinachotafutwa ni damu siyo mtoto.
 
Asante kwa maono hayo, ila kwenye tangazo nimeandika kwamba makubaliano yatasainiwa mahakamani na ustawi wa jamii ili kuepusha mtazamo wa aina hiyo
Pamoja na hayo Kuna ushetani ndani yake huwezi kugeuza mtoto kuwa kama mbuzi nna shaka na usalama wa mtoto atakaezaliwa kutokana na Masharti yako kwa Nini Mama asimuone mtoto Tena maisha yake yote?unataka uwafanye Nini hao watoto?acheni mambo yenu ya kimasonic uchwara hapa bongo
 
HATA YULE WANAUME MREFU ZAIDI TANZANIA AMETANGAZA KUWA ANAUZA MBEGU.
JAMAA NI MREFU ILA HAJATOA MASHARTI.
NIMEIPENDA IDEA YAKE MAANA MBEGU HUWA ZINAPOTEA TU. HII TA KUHITAJI MWANA MKE NDIO NAISIKIA HAPA NILIJUA NI ULAYA TU.
MBONA HUJAWEKA IQ. UNAWEZA PATA WATOTO LOW IQ WA AJABU SANA.
 
Huu utamaduni ni mgeni kwa bongo.
Ni sawa na mtu unemkodisha shamba. Akaweka miundombinu ya umwagiliaji pamoja na pembejeo anachotegemea ni mavuno msimu ukifika. Sasa akija kuvuna vipi uumie roho wakati kila kitu kafanya yeye na malipo ya kukodi shamba alishakulipa? Madada wa kihindi hua wanazichangamkia hizi fursa. Ila kwenye terms zako ingeongeza na funeral insurance.
 
UCHAGUZI WA GENES NI KITU WAZUNGU WANAKIZINGATIA SANA. JAMAA KAWEKA MASHARTI YAKE ANAANDAMWA.
UPANDIKIZAJI WA MIMBA NI TEKNOLOJIA ISIO MPYA ISPOKUWA WAAFRIKA HUWA TUPO NYUMA SANA.
HIZO DINI WALILETA WAZINGU NA HIZI TEKNOLOJIA WANALETA WAZUNGU, WEWE MWANA JF UNAEPINGA UMELETA NINI HAPA DUNIANI?
ANGALIENI DOCUMENTARY ZA FUTURE HUMAN.
KILA FAMILIA KATIKA FUTURE ITABIDI IAMUE IFANYE GENES MODIFICATION AU IBAKI PRIMITIVE.
IMAGINE WENZIO WANAWAMODIFY WATOTO WAO WANAPATA GENES YA NDEGE YA KUOTA MBAWA, WATOTO WAKO WANABAKI NA MIGUU. DO YOU THINK WATOTO WAKO WATA COMPETE?
IMAGINE WENZIO WANAPATA GENES ZA HIGH IQ KUTOKA KWA WATU WENYE IQ KUBWA WEWE UNABAKI PRIMITIVE NA URITH WA IQ DUNI.
IMAGINE WENZIO WANAAMUA WATOTO WAO WAWE NA KIMO KIASI GANI WEWE UNATEGEMEA NATURE.
EVRYTHING WILL BE MODIFIED IN FUTURE!
ELON MUSK TAYARI ANAANZA KUTUPELEKA KWENYE FUTURE KUTUFANYA TUWE CYBORG ROBOT. IMAGINE ELON BRAIN CHIP INAKUPA UWEZO WA ACCESS YA INTERNET DATA AT INSTANT I.E CLOUD DATA, IMAGINE UNAKUWA SEHEMU YA MTANDAO, YAANI WEWE UNAKUWA BRAIN YA MTANDAO!
WAAFRIKA TUACHE KUDUMAA AKILI IPO SIKU TUTAJIKUTA KAMA WAHAZABE.
KINACHOFUATA WAHAZABE WANATOWEKA TARATIBU POPULATION YAO INAPUNGUA KISA WAMEIKATAA TEKNOLOJIA, BORA MASAI,MANGATI WAMEAMUA KUJA KU ADOPT MODERN LIFE.

KWA HIO MTOA MADA YUPO SAWA NA WAKATI ILA KUNA WATU WENGI WAPO NYUMA YA MUDA.
SHIDA ILIOPO AFRIKA HUWA HATUNA NAJUKWAA YA KUELIMISHA JUU YA MABADIRIKO YA KITEKJOLOJIA BALI TUNASUBIRI TEKNOLOJIA IJE ITUBADIRISHE.
SASA HIVI TUNAKWENDA INDUSTRIAL 4....
KAMA SIJAKOSEA.. KILA KITU KINAKWENDA KUBADIRIKA.
TEKNOLOJIA ZA BOT KAMA CHAT GPT, CLOUD COMPUTING, QUANTUM COMPUTING, HUMAN ROBOT, DRIVER LESS CAR, HOME SCHOOOLING, GENETIC ENGINEERING, ULIMAJI USIO NA UDONGO (VERTICAL FARMING) WEWE BADO UNAWAZA KULIMA KWENYE UDONGO WENZIO WANAHAMA HUKO..
NYIE WOTE MNAOPINGA PINGA MTASWAGWA NA TEKNOLOJIA NI SUALA LA MUDA TU.
 
MNAPOPINGA MKUMBUKE NA MIMBA MLIZOTUPA, WATOTO MLIOTUPA, MAYAI MNAYOUA NA VIDONGE VYA MAJIRA.
WATOTO MLIOTELEKEZA WENGINE WAPO VITUO VYA KULELEA WATOTO WA MTAAANI.
WANAWAKE WANAJIFANYA HAPA WANAHURUMA UTADHANI HATUJUI MIENENDO YENU.
HATA MLIOMO HUMU WENGI WENU MMEISHA FANYA UOVU MWINGI SANA HUKO GIZANI ILA DUNIA IMEWAFICHIA SIRI. HAKUNA BIKIRA MARIA HUMU, MNATUCHOSHA TU.
 
Pamoja na hayo Kuna ushetani ndani yake huwezi kugeuza mtoto kuwa kama mbuzi nna shaka na usalama wa mtoto atakaezaliwa kutokana na Masharti yako kwa Nini Mama asimuone mtoto Tena maisha yake yote?unataka uwafanye Nini hao watoto?acheni mambo yenu ya kimasonic uchwara hapa bongo
Unajua hapo ameona Mama akiruhusiwa kumuona Mtoto ni tatizo pengine ataanza kumnangania Mtoto na Hela ameshalipwa, atatoa Siri , yapo mambo mengi kama binadamu atayanfa tofauti.
 
Back
Top Bottom