Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Kwako huenda sio rahisi, usiwasemee watu ndgu.

Kuna dada alijifungua na akamnyonga mtoto wake ili akaendelee kujiuza(au hujaisikia hii habari). Vipi hujaisikia ile mama kaua watoto wake wawili kwa kuwanyonga?? Vipi hao walibeba miezi mingapi mkuu??
Sasa hao wawili watashindwa kuzaa na kupewa M25??
Hayo yanaendana na tatizo LA akili!! Shida mtoa mada hataki mwenye tatizo la akili.
 
IVF kirefu chake ni In Vitro Fertilization.
IVF ni jambo la kurutubisha kwa kuunganisha mbegu za uzazi za mwanamme na yai la uzazi la mwanamke maabara, baada ya hapo zoezi linalofatia ni kupandikiza ujauzito kwa mwanamke kwa njia ya sindano kisha ujauzito utaendelea kukua kama kawaida kwa mda wa miezi tisa kisha mwanamke atajifungua kawaida.

IVF haihusishi kukutana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume bali mwanaume anatoa mbegu kwa kujichua au punyeto na mwanamke anatolewa yai lililopevuka maabara na wataalamu baada ya hapo ndio ujauzito unapandikizwa kwa mwanamke,
Ni njia safi na salama na haihusishi operation kubwa na haina hatari yeyote kwa mwanamke.

Sasa anahitajika mwanamke au msichana katika zoezi hilo,

MALIPO
Moja malipo ni milioni 25 ambayo yatasainiwa kisheria mahakamani na ustawi wa jamii.
Pili kila mwezi atalipwa milioni moja kama malipo ya motisha kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito, malipo hayo ni nje ya ile milioni 25.
Tatu kila siku atalipwa elfu ishirini kama gharama ya chakula kulea mimba kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito.
Nne atalipwa shilingi elfu hamsini kila siku kama gharama ya chakula baada ya kujifungua kwa mda wa mwaka mmoja kipindi ananyonyesha.
Tano gharama zote za hospital kwa mama kipindi cha ujauzito, mama na mtoto baada ya kujifungua zitagharamiwa na baba wa mtoto/watoto

MASHARTI
Moja ujauzito utalelewa sehemu aliyopo baba wa watoto.
Mbili hauruhusiwi kisheria kutangaza kwa mtu yeyote kama una ujauzito labda wazazi wako tu, na wazazi wakiambiwa nao wataelimisha kuhusu hili sharti.
Tatu baada ya kujifungua, mtoto/watoto wakifikisha mwaka mmoja utawakabidhi kwa baba yao.
Nne baada ya kukabidhi mtoto/watoto hautoruhusiwa kisheria na kibinadam wewe ndugu zako au rafiki zako kuwaona mtoto/watoto kwa namna yeyote kipindi chote cha maisha yenu hapa duniani.
Tano hautoruhusiwa kuwa na mahusiano ya aina yoyote na baba wa watoto kabla na baada ya kujifungua mtoto/watoto.
Sita awe tayari kulea ujauzito akiwa jijini dar es salaam.

SIFA ZA MWANAMKE/MSICHANA ANAEHITAJIKA.
Moja awe na afya nzuri, asiwe na magonjwa ya akili, pili asiwe na magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.
Pili awe mtanzania kutoka kabila na dini yeyote.
Tatu awe mrefu, mrefu sana atapewa upendeleo.
Nne awe mwembamba, akiwa mnene isiwe unene mkubwa sana.
Tano awe na umri wa kati ya miaka 25 hadi 35.
Sita awe mweupe au maji ya kunde asiwe mweusi sana.

Asanteni.
Pia kwa mwana Jamii Forum mwenye ndugu, rafiki au jirani mwenye hizo sifa naomba mnisaidie kusambaza hili tangazo.
Asante tena.

Vigezo na masharti kuzingatiwa
Kukilea kiumbe tumboni, kumnyonyesha hadi hapo kutakua na muunganiko mkubwa sana kati ya huyo mtoto na huyo mama. Mwenye anaweza kufanya hivi basi awe hajui nin maan ya kubeba kiumbe tumboni.
Na awe kimaslai zaid na zaid.
 
Yes Hii sheria kuna sehemu kama niliona hivi

Je mtoa mada amejipangaje?
Hawa vijana wanaongea tu! Hii kitu si mchezo. Ni uhai wa binadamu na kuna mwanamke ambaye ni binadamu anayebadilika kila kukicha! Ninao watato wa hivyo mie. Nakueleza Watoto wa IVF wana akili ajabu na ni wazuri. Hawaugui ovyo kama hawa wengine, hii hutamanisha masurrogate na kuanza kusumbua. Mtoto wa kwanza mke wangu alilazimisha surrogate awe mtoto wa ndugu yake, ila cha moto anakipata
 
Labda umpate ambae hajawahi kabisa kuzaa ila kwa ambae amewahi sio rahisi
Kuna bond flani hivi mama anaipata akishajifungua mwanae,na hukua zaidi kipindi cha mwaka 1 anapomnyonyesha!
Sasa wakati ile bond iko very strong wewe ndo unataka uifute gafla,that is psychological trauma na ml 25 haiwezi saidia hapo!
Na akimpeleka mahakani mama anashinda kesi
 
Back
Top Bottom