Anaitwa Roma: Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki

Kundi kubwa la hadhira hawataki kusikia vitu kama hivi wanapenda anasa musik tu
 
"Anitwa Roma nani wakumnyamazisha"
 
Missile of the Nation,
Imefika wakati sasa watambue kuwa vitisho na maguvu yanayokandamiza uhuru wa kujieleza na free press yanauongezea nguvu sana kuliko kuunyamazisha.

Watambue kabisa kwamba huu wimbo wa Roma ni kielelezo cha mtu aliyenyimwa uhuru wa kujieleza ndiyo maana kwa leo una trend sana. Kila aliyekandamizwa anaona wimbo wa Roma kama ni ukombozi kwake.

Wao wanapoteza muda kuwanunua akina Harmonize na Nandy kupiga manyimbo ya kuwasaidia kwa kuwapa hela au kuwaahidi kugombea ubunge. Hiyo ni kazi bure kwa kuwa sanaa huja automatically, hainunuliwi.

Meko aambiwe kuwa kadri anavyozuia uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari kwa kuogopa kukosolewa ndiyo anazidi kujenga nyongo ya chuki kwa Watanzania. Bora uwaache watu wajisemee, wakukosoe ili ujue unakosea wapi na ujisahihishe kuliko kulazimisha vyombo vya habari kukusifia kuanzia asubuhi hadi usiku.

Anayosema Roma ndiyo ukweli na anawakikisha maoni ya watu wengi, tunahitaji afya, elimu, maji safi kuliko huko kwenye mabombadier alikojielekeza
 
Nyimbo za ukombozi zinahitajika sana kwa nchi zinazoendelea kama TZ. Ukombozi huu ni wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii.

Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na matatizo kibao, na sanaa ni zana mojawapo ya kuibadilisha jamii, lakini wasanii wa sasa wao ni kuimba mapenzi na raha raha tu, wakati matatizo kibao!
 
Itapendeza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…