Anaitwa Roma: Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki

*ROMA MSOMI WA MWITUNI ANAYEIMBISHWA ASICHOKIAMINI!*

_Na Mwamba wa Kaskazini_

Nimefuatilia akaunti za wasiotaka maendeleo ya Tanzania wote na kundi lao linaloumia kuona maendeleo yanayopigwa-akina Maria Sarungi, Sufiani na wengine. Nimebaini kitu.

Wote hawa wamekuwa wakiushangilia wimbo mpya wa Msanii Roma ambaye kaimbaimba vitu viiiingi ambavyo hata yeye binafsi naamini ukimuuliza vingi hawezi kukwambia kwa nini kaimba. Hoja za kushikiwa.

Lakini ukweli ni kwamba wimbo huu si wake ni mkakati wa usaliti kwa nchi yake-umefadhiliwa. Tutamwonesha madhara ya kutumiwa, kusaliti yalivyo mabaya kwa mtu na hata kizazi chake.

Na waliopenyezewa fedha za ufadhili ndio walikuwa wa kwanza kuibuka kujifanya kama ndio wameuona kumbe wanaujua na walikuwa hata studio kuratibu mashairi. Ujinga sana huu.

Roma anaonekana kuingia katika propaganda iliyofeli-analalamikia demokrasia katika nchi ambayo hivi sasa yeye mwenyewe anazunguka nchi nzima kwa amani katika Tamasha la Fiesta akiwa na amani na kufanya muziki wake pamoja na kutukana sana viongozi majukwaani.Anataka nini zaidi?

Ni Msanii anayeimbishwa kasumba na propaganda asizozijua akiagizwa, kwa kujua au bila kujua, alilie demokrasia na uhuru wa kujieleza katika nchi ambayo yeye mwenyewe hivi karibuni kazunguka redio zaidi ya 20 kwenda kuutangaza wimbo wake alioimba na Stamina "Kijiwe Nongwa." Kote kaongea ya uongo na kweli na sasa anaendelea na bata la Fiesta. Ghafla mtu huyo huyo ataibuka kukwambia hakuna uhuru wa kujieleza!!

Namuona Roma aliyeshikiwa akili kabisa eti analilia demokrasia katika nchi ambayo hata yeye ameruhusiwa kuwa na akaunti ya Insta anaweka nyimbo zenye matusi lukuki kwa viongozi. Naona bado anaweweseka na walimteka.Asitjmie hii kisiasa, aseme nani walimteka.

Haya ndio madhara ya vijana wanaojiona wasomi lakini wasiojielewa- wanajiita wanafalsafa kumbe ni mazuzu tu yanayotumika. Hajui siku wanaomtumia hapa yeye ni kwao, siku pakiwaka, wale watarudi kwao yeye atakwenda ukimbizini!

Unamsanii Roma anayelilia demokrasia kutoka upande mmoja, halili kubanwa demokrasia ndani ya Chadema ambako kuna kiongozi kawa Mfalme wa Wafalme, kuna wabunge wa upinzani wanaoburuzwa na kuchukiwa hata wanaposhukuru tu kwa majimbo yao kupata maji.

Roma mpigania haki hasemi chochote kuhusu akina Maria Sarungi, Kigogo na wanaharakati wengine wanaoongoza kuwablock watu wenye maoni tofauti na yao. Roma hayaoni haya.

Roma haoni athari za demokrasia kwa baadhi ya vyama kama ACT, kila uamuzi lazima auridhie Ayatollah badala ya vikao vya Chama. Haoni shida.

Shida yake kubwa anaumia kuona Serikali imefufua shirika la ndege sasa watanzania wanasafiri kwa bei nzuri na uhakika.

Roma na wanaomtuma wanaumia kuona tunaongeza mapato, tunazidi kuelekea kujiregemea, tunatoa elimu bure, vituo vya afya vimejengwa, hospitali za wilaya na mikoa zimemalizika na anaumia zaidi kuona ujenzi wa reli ya kisasa na mradi wa umeme Rufiji vyote kwa fedha za ndani.

Roma haba raha kuona mabarabara, flyovers, kuona walimu zaidi ya laki 1.24 wamepandishwa madaraja mwaka huu, shule zinaboreshwa. Hataki na inamuuma.

Roma anaona demokrasia ni watu kuachwa wafanye ghasia- waandamane bila mpango, wapore vitu vya watu, wazuie watu kufanyakazi n.k.

Ni ajabu sana kwamba Roma haoni chochote katika nchi yake-haoni, haoni, haoni. Ila si bure, macho anayo vizuri.

Siku mtakayojua nguvu inayowapotosha hawa vijana mtashangaa na mtabaki mnasaga meno. Lakini wajue Tanzania ni imara sana kuliko wanavyodhani.

Nasisitiza, Roma hana ushujaa wowote, ni pandikizi lisilojielewa, ni msaliti kwa nchi na Taifa lake kwa vipande flani alivyopewa ambavyo bado haijafahamika ni vya fedha au fedheha.

Pole yako Roma, endelea kuimbishwa tu. Kitaeleweka.
NDUGU NAKUONA KAMA MSOMI ILA SIAMI KAMA UMEELIMIKA ,INAWEZEKANA ULIENDA SHULE LAKINI SHULE UKAIACHA SHULENI .Hauwezi kusema Roma katumwa wakati wewe uko hapa nchini unao Kila kinachoendelea kwani Roma alikaa na Watendeji wa Waka na kuwapatia maeelekezo ya kutopitisha wagombea wa upinzani nchi nzima da anyway ngoja niachie hapo
 
Like moja haitishi naomba nikuongeze na nyingine 100
Wewe ukiwa huru kujieleza alafu wenzako hawana uhuru wa kufanya hivyo. Je utasema kuna uhuru wa kujieleza?

Embu amka kwenye ndoto za kijinga hizo. unaandika kama mwendawazimu bhana.

Wewe kama unaona kuwa kuna uhuru wa kujieleza. Nawe kaimbe na uende kila chombo cha habari ukaipe promo. Kisha Ukale bata Fiesta au Wasafi Festival. Kwani nani alikukataza?

Lakini wewe unataka kumkataza ROMA ambaye kwa upande wake anaona hakuna uhuru wa kujieleza. Huoni kitendo tuu cha kutaka kumzuia ROMA asiende kuelezea hayo maoni yake ni Udikteta na sio Demokrasia.

Sina uhakika kama unajua maana ya Demokrasia. Sina uhakika kama unajua principles za demokrasia.

Ungezijua Principle za Demokrasia ungeelewa huyo ROMA anazungumzia nini. Hata hivyo sikukatazi kuwa Mjinga ikiwa umeamua kuwa hivyo. Maana nayo ni Demokrasia.

Kwa kukusaidia tuu.
Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo watu ndio huchagua serikali itakayowaongoza. Kwa hiyo watu ndio huamua nini kiwe na kipi kisiwe kwenye serikali walioichagua.

Tuje kwenye Principles za Demokrasia
● CITZEN PARTICIPATION (USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI AU RAIA)
Mwananchi au raia katika nchi zenye demokrasia anapaswa kushiriki na kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya kitaifa kama uchaguzi, Upigagi wa kampeni na mambo ya kisiasa, Kulipa kodi, Kupewa taarifa ya mambo yanayoendelea katika nchi n.k.

Sasa kama Wapinzani hawapewi ruhusa ya kufanya siasa wakati demokrasia inawaruhusu kufanya shughuli hizo huoni kwamba tayari demokrasia imesiginwa. Hilo huoni.

Kama mtu anataka kugombea uongozi lakini anawekewa figisu figisu bado useme kuna demokrasia. Labda uwe mwendawazimu wa kuzaliwa ndio unaweza kufikiri kwa namna hiyo.

● EQUALITY (USAWA)
Kwenye demokrasia raia wote ni sawa. Na wanapaswa kutendewa kwa usawa kabisa bila uonevu.
Lakin taifa letu lipo kundi linayoruhusa ya kufanya siasa wakati kundi jingine halina haki ya kufanya hivyo.
Suala la vyeti feki tuu. Wapo walioondolewa kwa kuwa na vyeti Feki hilo ni jambo jema lakini kitendo cha kuwaacha wengine kama akina Bashite kumeifanya Demokrasia kusiginwa. Hakuna usawa.

Suala la kubomolewa nyumba. Kama utakumbuka Jpm alisema wazi kabisa watu wa Mwanza wasibomolewe nyumba kwa kuwa walimpigia kura. Wakati huo watu wa DSM wakilia na kusaga meno. Wewe Bado unamuona ROMA haimbi anachokiamini.

● POLITICAL TOLERANCE (USTAHIMILIVU/ UVUMILIVU WA KISIASA)
Demokrasia inawataka watu wawe wastahimilivu kwenye siasa. Ukisikia mwenzako anakupiga kijembe au anatoa hoja ziwe za msingi au ziwe za hovyo unapaswa uvumilie tuu maana nawe anakuvumilia.

Lakini hili kwenye nchi yetu halipo kama ulikuwa hujui. Mhe. Rais kila mara ameshuhudiwa akitukana watu na kuwaita majina yasiyo na stara kwa mfano Wapumbavu, Vilaza, majizi(wakati hajapeleka hata mmoja jela) n.k. Yeye watu wanamvumilia lakini yeye akiitwa Dikteta Uchwara anahaha. Akitajwa kwa majina yasiyo yaheshima anahaha. Hana ustahimilivu wa kisiasa.

Matokeo yake ndio utasikia Lema kawekwa ndani, utasikia Tundu Lisu kapigwa Risasi, Utasikia Mbowe Kawekwa ndani, akina Halima Mdee na wenzake.

Utasikia Nani katekwa, Sijui fulani kakutwa kwenye Kiroba.

Alafu useme ROMA hajui akiimbacho. Sema wewe ndio umeshindwa kuelewa maudhui ya wimbo huo na kuyaoanisha na Mazingira.

● ACCOUNTABILITY AND TRANSPARENCY (UWAJIBIKAJI NA UWAZI)
Nchi isiyo na Demokrasia huwezi kuona watu wakieajibika au kuwajibishwa. Au kuwa na uwazi. Ishu tuu utekaji na mauaji yaliyokuwa yanaendelea katika nchi hii. Viongozi kadhaa walipaswa wawajibike mathalani Kangi Lugola. Waziri wa mambo ya ndani asingepaswa kubaki madarakani ikiwa anajitambua kazi yake.

Masuala ya Korosho, Sijui Upotevu wa 1.5T ni mambo ambayo yangepaswa kuwekwa wazi lakini hayo hayapo. Na ukiyaongea upo katika hatari ya maisha.

● ACCEPTING THE RESULTS OF ELECTION
(KUKUBALIANA NA MATOKEO YA UCHAGUZI)
CCM mara kadhaa wamekuwa wakitumia mabavu kutangaza matokeo ambayo ni ya uongo. CCM wakishindwa kwenye uchaguzi mara nyingi huiba au kutumia nguvu kumtangaza Mgombea wao. Usijesema sina mifano; Kule Zanzibar hakuna asiyejua kilichotokea. Seif alishinda lakini CCM wakatumia Mabavu kufanya uchaguzi urudiwe. Kule kwa Kafulila na Wasira walitumia figisu figisu nyingi.

Bado useme ROMA hana chakuimba. Kama wewe sio mwendawazimu utakuwa ni nani?

Sishangai kusikia wewe ni mtu mzima tena huenda unashahada ya fani fulani. Demokrasia pia ni pamoja na kuchagua kuwa mjinga hivyo ni haki yako.

Zipo Principles nyingi sana za demokrasia. Nimekupa kwa uchache sana.

Hivyo ukisikia mtu akisema habari za demokrasia usifikiri anaongelea jambo moja au mawili kama miguu ya ndege. Hapo yanazungumziwa masuala mbalimbali.

Wewe umekalia Fiesta sijui uhuru wa kujieleza. Angekuwa na uhuru wa Kujieleza angetekwa? Mbona hilo hulizungumzii.

Hivi hii nchi ingekuwa na demokrasia unafikiri mpaka sasa watumishi wangekuwa hawajaongezwa mishahara?

Hivi hii nchi ingekuwa na demokrasia leo hii watu wangetekwa na kuuawa?

Hivi hii nchi ingekuwa na demokrasia unafikiri Akwilina angeuawa?

Hivi hii nchi ingekuwa na demokrasia unafikiri JPM angekuwa madarakani?

Hivi nchi hii ingekuwa na Demokrasia unafikiri Polisi kama Yule wa Dodoma angeongea sijui watapigwa Wachakae ilhali familia yake inategemea mshahara anaopewa na hao hao watu?

Niishie hapo maana mjinga naye anauhuru wake.
 
*ROMA MSOMI WA MWITUNI ANAYEIMBISHWA ASICHOKIAMINI!*

_Na Mwamba wa Kaskazini_

Nimefuatilia akaunti za wasiotaka maendeleo ya Tanzania wote na kundi lao linaloumia kuona maendeleo yanayopigwa-akina Maria Sarungi, Sufiani na wengine. Nimebaini kitu.

Wote hawa wamekuwa wakiushangilia wimbo mpya wa Msanii Roma ambaye kaimbaimba vitu viiiingi ambavyo hata yeye binafsi naamini ukimuuliza vingi hawezi kukwambia kwa nini kaimba. Hoja za kushikiwa.

Lakini ukweli ni kwamba wimbo huu si wake ni mkakati wa usaliti kwa nchi yake-umefadhiliwa. Tutamwonesha madhara ya kutumiwa, kusaliti yalivyo mabaya kwa mtu na hata kizazi chake.

Na waliopenyezewa fedha za ufadhili ndio walikuwa wa kwanza kuibuka kujifanya kama ndio wameuona kumbe wanaujua na walikuwa hata studio kuratibu mashairi. Ujinga sana huu.

Roma anaonekana kuingia katika propaganda iliyofeli-analalamikia demokrasia katika nchi ambayo hivi sasa yeye mwenyewe anazunguka nchi nzima kwa amani katika Tamasha la Fiesta akiwa na amani na kufanya muziki wake pamoja na kutukana sana viongozi majukwaani.Anataka nini zaidi?

Ni Msanii anayeimbishwa kasumba na propaganda asizozijua akiagizwa, kwa kujua au bila kujua, alilie demokrasia na uhuru wa kujieleza katika nchi ambayo yeye mwenyewe hivi karibuni kazunguka redio zaidi ya 20 kwenda kuutangaza wimbo wake alioimba na Stamina "Kijiwe Nongwa." Kote kaongea ya uongo na kweli na sasa anaendelea na bata la Fiesta. Ghafla mtu huyo huyo ataibuka kukwambia hakuna uhuru wa kujieleza!!

Namuona Roma aliyeshikiwa akili kabisa eti analilia demokrasia katika nchi ambayo hata yeye ameruhusiwa kuwa na akaunti ya Insta anaweka nyimbo zenye matusi lukuki kwa viongozi. Naona bado anaweweseka na walimteka.Asitjmie hii kisiasa, aseme nani walimteka.

Haya ndio madhara ya vijana wanaojiona wasomi lakini wasiojielewa- wanajiita wanafalsafa kumbe ni mazuzu tu yanayotumika. Hajui siku wanaomtumia hapa yeye ni kwao, siku pakiwaka, wale watarudi kwao yeye atakwenda ukimbizini!

Unamsanii Roma anayelilia demokrasia kutoka upande mmoja, halili kubanwa demokrasia ndani ya Chadema ambako kuna kiongozi kawa Mfalme wa Wafalme, kuna wabunge wa upinzani wanaoburuzwa na kuchukiwa hata wanaposhukuru tu kwa majimbo yao kupata maji.

Roma mpigania haki hasemi chochote kuhusu akina Maria Sarungi, Kigogo na wanaharakati wengine wanaoongoza kuwablock watu wenye maoni tofauti na yao. Roma hayaoni haya.

Roma haoni athari za demokrasia kwa baadhi ya vyama kama ACT, kila uamuzi lazima auridhie Ayatollah badala ya vikao vya Chama. Haoni shida.

Shida yake kubwa anaumia kuona Serikali imefufua shirika la ndege sasa watanzania wanasafiri kwa bei nzuri na uhakika.

Roma na wanaomtuma wanaumia kuona tunaongeza mapato, tunazidi kuelekea kujiregemea, tunatoa elimu bure, vituo vya afya vimejengwa, hospitali za wilaya na mikoa zimemalizika na anaumia zaidi kuona ujenzi wa reli ya kisasa na mradi wa umeme Rufiji vyote kwa fedha za ndani.

Roma haba raha kuona mabarabara, flyovers, kuona walimu zaidi ya laki 1.24 wamepandishwa madaraja mwaka huu, shule zinaboreshwa. Hataki na inamuuma.

Roma anaona demokrasia ni watu kuachwa wafanye ghasia- waandamane bila mpango, wapore vitu vya watu, wazuie watu kufanyakazi n.k.

Ni ajabu sana kwamba Roma haoni chochote katika nchi yake-haoni, haoni, haoni. Ila si bure, macho anayo vizuri.

Siku mtakayojua nguvu inayowapotosha hawa vijana mtashangaa na mtabaki mnasaga meno. Lakini wajue Tanzania ni imara sana kuliko wanavyodhani.

Nasisitiza, Roma hana ushujaa wowote, ni pandikizi lisilojielewa, ni msaliti kwa nchi na Taifa lake kwa vipande flani alivyopewa ambavyo bado haijafahamika ni vya fedha au fedheha.

Pole yako Roma, endelea kuimbishwa tu. Kitaeleweka.
Kwamba hujaskia popote katika wimbo wa ROMA alipoisifia serikali kwa kuongeza mapato na kuiomba serikali iboreshe mazingira ya maaskari na walimu.

Acheni kumtisha Roma,Mimi nafrkir Roma alitakiwa ayasemee maovu yote yanayofanywa na SERIKALI,sambamba na kuisifia pale atakapoona....
 
Jamaa limeandika insha ya kumjibu roma [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
nyoooo naona hili jimbo limetembea kwenye mishipa yako yote wewe. Hao walimu mmewapandisha madaraja kwa huruma au kwa sheria ya kazi? Je, ni madaraja ya barua tu au madaraja na barua na stahiki zake? Vipi annual increment ya walimu hao, sio wamedhulumiwa tangu 2015 ili haki yao hiyo itumike kununulia madege ambayo wao hawayapandi. nadhani roma anatimiza wajibu uliokuwa ukitimizwa na akina, FAROUK TOPAN wa Tamthiliya ya MFALME JUHA, MUHAMED S. KHATIBU wa DIWANI YA WASAKATONGE, na hata akina THEOBALD MVUNGI wa DIWANI YA MASHAIRI YA CHEKACHEKA.
 
Back
Top Bottom