ROMA: KWETU BIMA YA AFYA NI BORA KULIKO IZO NDEGE.
"Yuda usimuharibie Dani ili umfurahishe Mtukufu, Sisi sote wanao kwa nini unampenda Yusuph.
Yakobo Baba Pesa Madaraka Umaarufu Ona umewapatia vijana wanakosa Hekima na Utu.
Wapunguzie Vifungo, Wafungwa wasio na hatia, Wengine walifata mkumbo kiukweli hawakuwa na Nia.
Nasikia Jimbo la Ubungo kuna mtu amelipania, Hizi tungo ni zaidi ya Waraka wa Waebrania.
Chama kilishawatimua Wanasiasa mlio wanunua, Yaani mnapiga Bomu Mochwari halafu mnajisifu mumeua !
Tuliombe Taifa tuwaombee Viongozi wetu, Nchi ina miiba sio tuwavishe viatu walioko peku.
Tusilete Uchama kwenye ishu za Kitaifa, Uongozi ni kuacha Alama Chanya na kuwajibika, Kutekana kuuana sio sifa ya Mtanganyika.
Hongera Baba kwa ukusanyaji wa Mapato Kedekede, ya kodi, Na Flyover ndo hizo kanyanga Twende, Kwetu Bima ya Afya ni Bora kuliko izo Ndege.
Atafanya yote Tumuombee yesu Nibebe, Watu wametumbuliwa kabla ya mwezi mmoja kustaafu, Walimu wamesahauliwa mapato yao, Halafu, Polisi mishahara yao hadi tuwapige tafu, boresha Mahospitalini tupunguze idadi ya Wafu."-Roma Mkatoliki.
#AnaitwaRoma..