Sio hivyo wala. Kuna jamii na koo ambazo watoto wakike wanawafanana mama zao na wa kiume wanawafanana baba zao.
Pia kuna koo zina damu nyepesi sana kupotezwa zile awe mama awe baba watoto hawatomfanana. Hizi ndizo pekee mzazi atachagua uzuri wa mwenza na akapatia kwa asilimia kubwa.
Kuna koo zenye damu nzito watoto wa kike na wa kiume wanawafanana baba zao, yani hawa unakuta baba mweusi na mama maji ya kunde wa asili yule kibongobongo wanasema mweupe ila mtoto wa kike anazaliwa mweusi ti. Baba kama ana kipara, mtoto wa kike anazaliwa ana bonge la komwe. Baba kama ana kichogo, mtoto wa kike anazaliwa na kichogo. Na unakuta ukoo mzima mabinti wanafanana baba zao.