Anaomba ushauri: Alimuacha mke kwa miaka 9 (bila kumpa talaka kwa ndoa ya kiislamu), sasa anataka warudiane wakati mke alishaolewa!


Una kichaa wewe......! Miaka 9 huna uchungu, Leo hauna uchungu.
 
Pole Sana mkuu.

Jitahidi uanze upya na utafute MTU mzuri wa kukusaidia kukushauri na kukupa insight.

Kwa MTU mpambanaji na mwenye malengo ambaye hajapata tatizo lolote la Afya ya mwili na akili . miaka tisa hawezi kushindwa kupambana na kufanikiwa.

Pole Sana jitahidi uanze upya kwa kutafuta watu wa kukujenga Akili.
 
Tatizo lako kubwa kwenye maisha yako ni kwamba huna msimamo,hujui unataka nini kwenye maisha,ndio maana ukamkimbia mkeo na watoto wako na kwenda kwa hawara,

Ndio maana unasema kua shida yako ni kuona watoto tu ila hapo hapo unataka akupe mtaji pia!
Ulipata Mke mwenye roho nzuri sana hata akakupokea vizuri tu baada ya miaka 9 na kukuruhusu kuona watoto ila ndio basi tena umeshampoteza,

We live in the era of Smart phone and stupid people.
 
Sijajua kwa upande wa dini ya kiislam imekaaje ila kwa akili ya kawaida tu huyo mwanamke yupo sahihi.
 
Unavuna ulichopanda, Kwa miaka mingi mkeo na watoto wameteseka huku wewe ukila mema ya nchi na kimada halafu bila aibu Unaenda kumwomba mtaji mkeo wa zamani. Bro ni zamu yako kupitia machungu aliyopitia mkeo na watoto. Pambana utafte mtaji wako acha kulialia mtoto wa kiume.
 
Inawezekana alikwenda omba talaka kwa Mufti(mahakama ya kadhi). Kumbuka huyu mke ulimtelekeza kwa miaka 9 sasa unataka akusubiri tu?. Maneno yako umesema unataka akupe mtaji ndio utowe talaka sasa shida yako mtaji au mke?.
Nimekosa majibu, ikabidi nilete kwa wajuvi wa mambo huku
 
Dio mimi, mimi messenger tuuu.. ila nikipokea tusi ntamtukana pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…