Anaomba ushauri: Alimuacha mke kwa miaka 9 (bila kumpa talaka kwa ndoa ya kiislamu), sasa anataka warudiane wakati mke alishaolewa!

Mimi ni kijana nina miaka 37, nimeoa ndoa yangu ina miaka 12 sasa, kuna kipindi nilipata mwanamke mwingine, niliondoka na kwenda kuishi naye, kweli nilimuacha mke wangu na watoto wawili na sikuwa nikihudumia kwakua kipato kilikua cha shida, lakini sikumpa talaka kwani sisi wote ni waislamu. Kwa miaka kama tisa hivi nilikua sijakanyaga nyumbani nilianzisha familia nyingine nikawa naishi na huyo dada, sikuhudumia si kwakua sikutaka bali kwakua sikua na kazi.

Mwaka jana huyo mwanamke niliyekua nikiishi naye alimua kuniacha, aliondoka na kwenda kuishi na mwanaume mwingine. Aliniacha kwa dharau na matusi nikaona kwakua hatukufunga ndoa basi niondoke, aliondoka na wanangu wawili na mpaka sas ahataki hata nihudumie watoto. Kwanza niliona aibu kurudi nyumbani lakini baada ya kuongea na marafiki zangu walinishauri nirudi kulea familia. Mimi kwetu ni shinyanga na huyo mwanamke niliyekua naishi naye alikua akiishi Mwanza.

Nilirudi nyumbani lakini cha ajabu niliambiwa kuwa mke wangu alikua kaondoka mua mrefu kaondoka na watoto wangu. Roho iliniuma sana, kwani alikata mawasiliano kabisa na ndugu zangu na walikua hawajui kama yuko wapi? niliamua kwenda mpaka kwao, Moshi Kilimanjaro, mke wangu yeye ni mpare, nilienda na kuongea na ndugu zake, kwanza walinishangaa na kuniambia kuwa mke wangu alirudi nyumbani na kuwaambia kuwa nimempa talaka, alianza maisha na sasa anishi Dar anafanya kazi.

Baada ya kuondoka kwetu nilipokua nimemuacha alirudi akawaacha watoto nyumbani kwao akaenda kusoma chuo kwani wakati nilimuoa alikua na Diploma. Alimaliza Digrii na sasa hivi anafanya kazi kwenye benki moja ni mtu mkubwa tu. Niliamua kwenda dar kumtafuta, niliwaambia ndugu zake ninachotaka mimi ni kuwaona watoto wangu basi. Nilienda nikamfuata ofisini, alinipokea vizuri tu na kuniruhusu kuwaona watoto lakini hakuruhusi niende kwake. Tatizo nikuwa mimi nimejirudi, nataka kurudiana na mke wangu lakini yeye alikua hataki.

Amefunga ndoa na mwanaume mwingine wakati mimi bado nilikua sijampa talaka, nimeuambia hata anipe mtaji ili nimuache nimpe talaka lakini hataki hata kunisikia. Naomba kuuliza hivi sina haki zozote kwa mke wangu? Je mimi sitambuliki kama mume halali wakati sikumpa talaka?

Una kichaa wewe......! Miaka 9 huna uchungu, Leo hauna uchungu.
 
Pole Sana mkuu.

Jitahidi uanze upya na utafute MTU mzuri wa kukusaidia kukushauri na kukupa insight.

Kwa MTU mpambanaji na mwenye malengo ambaye hajapata tatizo lolote la Afya ya mwili na akili . miaka tisa hawezi kushindwa kupambana na kufanikiwa.

Pole Sana jitahidi uanze upya kwa kutafuta watu wa kukujenga Akili.
 
Tatizo lako kubwa kwenye maisha yako ni kwamba huna msimamo,hujui unataka nini kwenye maisha,ndio maana ukamkimbia mkeo na watoto wako na kwenda kwa hawara,

Ndio maana unasema kua shida yako ni kuona watoto tu ila hapo hapo unataka akupe mtaji pia!
Ulipata Mke mwenye roho nzuri sana hata akakupokea vizuri tu baada ya miaka 9 na kukuruhusu kuona watoto ila ndio basi tena umeshampoteza,

We live in the era of Smart phone and stupid people.
 
Mimi ni kijana nina miaka 37, nimeoa ndoa yangu ina miaka 12 sasa, kuna kipindi nilipata mwanamke mwingine, niliondoka na kwenda kuishi naye, kweli nilimuacha mke wangu na watoto wawili na sikuwa nikihudumia kwakua kipato kilikua cha shida, lakini sikumpa talaka kwani sisi wote ni waislamu. Kwa miaka kama tisa hivi nilikua sijakanyaga nyumbani nilianzisha familia nyingine nikawa naishi na huyo dada, sikuhudumia si kwakua sikutaka bali kwakua sikua na kazi.

Mwaka jana huyo mwanamke niliyekua nikiishi naye alimua kuniacha, aliondoka na kwenda kuishi na mwanaume mwingine. Aliniacha kwa dharau na matusi nikaona kwakua hatukufunga ndoa basi niondoke, aliondoka na wanangu wawili na mpaka sas ahataki hata nihudumie watoto. Kwanza niliona aibu kurudi nyumbani lakini baada ya kuongea na marafiki zangu walinishauri nirudi kulea familia. Mimi kwetu ni shinyanga na huyo mwanamke niliyekua naishi naye alikua akiishi Mwanza.

Nilirudi nyumbani lakini cha ajabu niliambiwa kuwa mke wangu alikua kaondoka mua mrefu kaondoka na watoto wangu. Roho iliniuma sana, kwani alikata mawasiliano kabisa na ndugu zangu na walikua hawajui kama yuko wapi? niliamua kwenda mpaka kwao, Moshi Kilimanjaro, mke wangu yeye ni mpare, nilienda na kuongea na ndugu zake, kwanza walinishangaa na kuniambia kuwa mke wangu alirudi nyumbani na kuwaambia kuwa nimempa talaka, alianza maisha na sasa anishi Dar anafanya kazi.

Baada ya kuondoka kwetu nilipokua nimemuacha alirudi akawaacha watoto nyumbani kwao akaenda kusoma chuo kwani wakati nilimuoa alikua na Diploma. Alimaliza Digrii na sasa hivi anafanya kazi kwenye benki moja ni mtu mkubwa tu. Niliamua kwenda dar kumtafuta, niliwaambia ndugu zake ninachotaka mimi ni kuwaona watoto wangu basi. Nilienda nikamfuata ofisini, alinipokea vizuri tu na kuniruhusu kuwaona watoto lakini hakuruhusi niende kwake. Tatizo nikuwa mimi nimejirudi, nataka kurudiana na mke wangu lakini yeye alikua hataki.

Amefunga ndoa na mwanaume mwingine wakati mimi bado nilikua sijampa talaka, nimeuambia hata anipe mtaji ili nimuache nimpe talaka lakini hataki hata kunisikia. Naomba kuuliza hivi sina haki zozote kwa mke wangu? Je mimi sitambuliki kama mume halali wakati sikumpa talaka?
Sijajua kwa upande wa dini ya kiislam imekaaje ila kwa akili ya kawaida tu huyo mwanamke yupo sahihi.
 
Unavuna ulichopanda, Kwa miaka mingi mkeo na watoto wameteseka huku wewe ukila mema ya nchi na kimada halafu bila aibu Unaenda kumwomba mtaji mkeo wa zamani. Bro ni zamu yako kupitia machungu aliyopitia mkeo na watoto. Pambana utafte mtaji wako acha kulialia mtoto wa kiume.
 
Inawezekana alikwenda omba talaka kwa Mufti(mahakama ya kadhi). Kumbuka huyu mke ulimtelekeza kwa miaka 9 sasa unataka akusubiri tu?. Maneno yako umesema unataka akupe mtaji ndio utowe talaka sasa shida yako mtaji au mke?.
Nimekosa majibu, ikabidi nilete kwa wajuvi wa mambo huku
 
Huku nikikutukana nitafungiwa ila we jamaa ni MPUUZI sana..!!Hio Ndoa ya 12 ni ipi ni hiii hii Uliemuacha mwanamke miaka 9 kwasababu ya Hawara..?Umerudi kwasababu kule umeachwa so bila kuachwa bado ungebaki kule MPK kifo chako..!Huna Adabu Umeleta mada ya kunikera usiku huu Nitakutukana mseng* wewe…
Dio mimi, mimi messenger tuuu.. ila nikipokea tusi ntamtukana pia
 
Back
Top Bottom