Habari wana jf? natumai mko wazima.Niende moja kwa moja,Mzee Juma michael ni mzaliwa wa mkoa wa mtwara,wilaya ya masasi.Miaka ya 1978s aliwahi kufanya kazi kama askari magereza wilaya ya Musoma,katika gereza la musoma.Miaka hiyo hiyo alipata kuoa Mama mmoja(Mnyiramba)-singida na alibahatika kuzaa nae mtoto alikuwa anaitwa ANNA.Kwa bahati mbaya mke wake huyu hatukupata jina lake kamili,ila alikuwa anajulikana kama mama ANNA.KWenye miaka ya 1982s alipata mtoto mwingine kwa mama mmoja mwenyeji wa Musoma Vijijini na alikuwa anaitwa MONIKA(Huyu alizaa naye tu hakumuoa),akawa amepata mtoto wa kiume.Mwaka 1983 inasadikika aliacha kazi na kuanzisha karakana yake binafsi hapo musoma ya ufundi seremala.Badae alirudi kwao kwenye miaka ya 1985.Mwaka jana nilianza kuleta hapa mada hii na nilipata ushirikinao mkubwa sana toka kwa members wa jf,isipokuwa kwa wachache huwa hawakosi kuvuruga,ASANTENI.
KWA NINI ANATAFUTWA? Kiufupi kijana wake ambaye alimzaa na mama wa musoma vijijini(ANGALIA HAPO JUU) ndo anamtafuta kwani hamjui na pia anaitaji kumuona baba yake ili kama yuko hai hamsaidie.Kwa mjibu wa huyu mama wa ndugu yangu(anayemtafuta mzee juma/baba yake),mzee alikuwa anatamka mara kwa mara kuwa wazazi wake walihamia mtwara kutokea wilaya ya masasi.
TULIPOFIKA KATIKA KUMTAFUTA YEYE AU ATA UZAO WAKE(WANAE);Awali tulipata mawasiliano wa member wenzetu kuwa alikuwa wilaya ya mbozi na tulifatilia kila kitu lakini hatukumpata,kwani hakuwa siliasi(alitaka tu pesa),pili tulifika kwa mwajili wake alipokuwa akifanya kazi awali, pia kwa maelezo yao hatukweza pata data za miaka hiyo,pia tumeshafika kijiji cha ziwani-mtwara pia alituelekeza mtu kuwa kuna mtu ananyefanana jina na mzee,pia hatukumpata.Zaidi pia kuwa rafiki yetu yuko wilaya ya msasi alifika kijiji cha LUSATO pia tulialifiwa kuwa anaweza patikana lakini hatumkumpa.
OMBI KWA WANA JF:Tunaomba tena kwenu kuendelea kusaidia kumsaka mzee wetu,pia hata kama hayupo hai watoto wake ambao naamini kufikia miaka hii ni watu wazima kama huyu ANNA,ambaye ndiye ametajwa kuwa ndiye mwanae mkubwa anaweza jitokeza ili tuwasiliane KWANI YEYE ANA AU WATOTO WAKE WENGINE kama aijaliwa tena waneza kuwa members humu wakasoma hii mada na kuielewa.PIA kwa yeyote ambaye atapata kumjua huyu mtu baada ya maelezo ya hapo juu anaweza kutusadia.Mawasiliano 0762364740.MUNGU AWABARIKI.